nimelia hadi nimechoka ....... hii ni fair jamani?

mbabu anazeeka vibaya msamehe bure,kakasirika sababu kakupa masifa mazuri mazuri halafu hata jero hajaambulia.
sikuwa nayo sis..... huyo king unamshusha lini bwana ... tired kuwait banaaa.................
 
Smile Pole, Huyo Mzee Msamehe BureHiyo ni njia tu ya kukuomba Hela
 
Achana naye. kauchauri wakati wa kuondoka acha buku mbili hapo home waambie wampe. hautapungukiwa kitu.
 
Ungempa pesa angeondoka na kutangaza kuwa ama umemhonga kwa kuwa unamtaka au umempa dili ka kukutafutia mme.
 
Achana Naye wala Usichukie ni mwehu

Nipo kijiji nimepata kalikizo masaa kadhaa nimekuja kumuonamgonjwa
Nimekaa home kidogonikaona nitoke niende kanisani nikafanye maombi kidogo kanisani ni mita kadhaa toka home hapa .
Barabarani sasa,
Mara katokea huyu mzee kava tishert yake ya ccm
Nadhani ndo mtu pekee aliebaki wa ccm hapa kijiji maana navojua kijiji hiki…….
Nikamsalimia ,shkamoo mzee Fulani…. Ajaitika katoa macho kwa mshangao akaachia na tabasamu kali akaanza
Smile,smile,smile mwanangu ua la asubuhi leo nitacheka mpaka mwaka kesho yaani jana tu nilimuuliza baba yako uko wapi maana kila siku nakukumbuka mwanangu,ujue siku mama yako anakuzaa mimi ndo nilimpeleka hospt kujifungua.nakwambia ulizaliwa na kilo 4 .5 , mtoto mzuri haijawai kutokea kijiji hiki ..........
Nilijua utakuwa tu mtoto mjanja kama babu yako ,ujue babuyako alikuwa……….. haitokaa itokee bahati mbaya wewe hukumkuta
Yaani wewe mtoto sio kama hao wengine wanaenda mjini wanarudi wamevaa yeboyebo kama watotowa mamananihii hapo(akataja mtu)
Tena kuna Yule mtoto wa balozi nanihii kaka yangu Yule ameniomba nimtafutie mke hapa kijijini yaaningoja nimpigie sasa hivi (akatoa simu-akapiga piga ) ooh naona imezimwa ,badaenitamwambia hili jambo .wewe mtoto lazima tukuchukue …wewe …. Naapa hatukuachi…

Akaendelea
Sasa smile… hebu nipe elfu kumi moja hapo nikapate moja motomoja baridi….. nikwamwambia sina
Basi fanya elfu tano………………………………………………………………………………………………nikamwambiasina
Basi elfu 2……………………………………………………………………………………………………………..nikamwambiasina
Hata ka elfu au mia tano tu……………………………………………………………………………………….nikamwambia sina


Akaniambia wewe mtoto ni mjinga mjinga kama shangazi yako ,na ndo maana nilimuacha akaenda kuolewa na lizee huko…….
Huko mjini wala huna lolote ,kwanza baba yako ndo anakutumiavihela hela vya kutumia si urudi tu hapa kijijini?
Huna akili yeyote nilijua tu huna lolote.mjinga mjinga tukama kaka yako ndo maana mke kamkimbia (sina hata bro alokimbiwa na mke jamani)
Kaolewe tu huko porini… nani anaoa wajinga hapa kijijini …kafie mbali huko… mnajifanya jina kubwa kumbe hamna lolote wapuuzi tu…

Kaishia zake bado anatukana

Sijui ni mfanyeje huyu mzee jamani?
Huu ni uungwana?
Huu ni utu?
ngoja nilale kidogo ......
 
Smile,

Pole sana mama kwa yaliyokupata, i know how bad you feel when u have a big burden halafu anatokea chizi mwingine anakuongezea zigo lisilo na maana. But just know this,
Siku hizi mvi hazimaanishi busara
Age isn't a thing but a number
Everybody in this world is insane ila tu viwango ndio tunatofautiana

so ukiona mtu anakwambia kitu ambacho we unaona kabisa cha kichizi kiache kitokee sikio la pili na undelee na mambo yako never let them hurt you
 
mtumie mzee wako hela bwana aache matusi na tshert ya chama uliompa imeisha
hahaah...ungekutana na mzee wangu ungekuja hapa kusimulia, cuz angebadilisha maisha yako kabisa!!
pamoja na uzee wake but ni noumer!!!
 
hahaah...ungekutana na mzee wangu ungekuja hapa kusimulia, cuz angebadilisha maisha yako kabisa!!
pamoja na uzee wake but ni noumer!!!
teh teh... nipe no yake basi .....
 
OTIS space bar yake ina mushkeli kidogo usijali.:tape: Smile pole....alianza kukusifia umpe hela sasa hukumpa akakuponda...usijali ndio mambo ya vijijini hayo...wale hata mia tano wanaridhika...next time weka mia tano tano za kutosha kwenye pochi...

uandishi wako Smile
OTIS
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom