cyrax
Senior Member
- Mar 12, 2017
- 105
- 88
habari zenu wana JF,
nimekuja tena kuomba msaada wa kibarua hali imekuwa ngumu, baada ya kuzunguka kutafuta ajira rasmi ya kufundisha kwenye shule bila mafanikio niligeukia kwenye kazi za vibarua kwenye ujenzi angalau niweze kulipa kodi na chakula hapa mjini Dar es Salaam.
Wiki iliyopita ilikuwa ngumu kwangu baada ya kupewa notisi ya mwezi mmoja kuhama ninapoishi hii ilitoka kwa wapangaji wote, balaa limekuja tena nilipotaka kufanya kazi zaidi nipate pa kukukimbilia mwili umekataa kazi, nimepata tatizo la mgongo unauma kuanzia kiunoni na kizunguzungu kikali wajuzi wameniambia inawezekana ni presha ya kushuka. Kwa sasa siwezi kufanya kazi ngumu sana kutokana na hali yangu ya afya.
Ombi langu kwenu mnisaidie kupata kibarua nipate fedha kidogo nisukume maisha huu upepo upite hali ikae sawa. Nipo dar naweza kufanya kazi yoyote ambayo hainihitaji nikae juani sana
Asanteni sana.