Nimekwama wapendwa, nisaidieni nipate kibarua

cyrax

Senior Member
Mar 12, 2017
105
88
habari zenu wana JF,

nimekuja tena kuomba msaada wa kibarua hali imekuwa ngumu, baada ya kuzunguka kutafuta ajira rasmi ya kufundisha kwenye shule bila mafanikio niligeukia kwenye kazi za vibarua kwenye ujenzi angalau niweze kulipa kodi na chakula hapa mjini Dar es Salaam.

Wiki iliyopita ilikuwa ngumu kwangu baada ya kupewa notisi ya mwezi mmoja kuhama ninapoishi hii ilitoka kwa wapangaji wote, balaa limekuja tena nilipotaka kufanya kazi zaidi nipate pa kukukimbilia mwili umekataa kazi, nimepata tatizo la mgongo unauma kuanzia kiunoni na kizunguzungu kikali wajuzi wameniambia inawezekana ni presha ya kushuka. Kwa sasa siwezi kufanya kazi ngumu sana kutokana na hali yangu ya afya.

Ombi langu kwenu mnisaidie kupata kibarua nipate fedha kidogo nisukume maisha huu upepo upite hali ikae sawa. Nipo dar naweza kufanya kazi yoyote ambayo hainihitaji nikae juani sana

Asanteni sana.
 
Apo ndo ujue hali si shwali check uzi ulivotulia pengine kila mtu ana shida na kazi au aliyo nayo haimtoshelezi pole ndugu kukosa kazi mjini ni azabu ata ya jela ndogo
 
Nakushauri uhame dar hamia mkao wa pwani kuna viwanda vingi na Kodi Bei IPO chini ,utapata kazi na utakuja kunishukuru hapa ,anzia eneo la misugusugu pale viwanda vinawasaidia vijana

USSR
 
mkuu naomba utoe information vizuri Ili hata sisi wengine tupate Kwa kuanzia hiyo misugusugu ipo maeneo Gani?
 
Wakat unatafuta kazi naomba upitie njia hiz kama sitakukwaza, Naamn simu unayotumia inaweza uzika na ukapata hata laki moja sindio? Nenda kariakoo nunua protector za kawaida boks wanauza 5000 znakua 10 kwa kuanzia changanya changanya kutokana na brand za cm zilzo kitaan kwa wing nunua na zile za 5D boks wanauza 9000 chukua ata boks mbil mbil izo za glas na izo za 5D tafuta edfon kwa jumla wanauza 1200 wew utauza mpka 5000 chukua beg weka mgongon zunguka kwenye ma baa uez kosa mtu wa kuweka hata protector kwa cku nzma na kwa protector moja unawekea 5000 usisahau na kava za cm apo unajiongeza ww mwwnyew nn kngne cha kubeba flash 4 gb wanauza 6000 8 gb 7000 nk nakwambia utateseka kwa wik moja kujua jins ya kucheza na akil za wateja ila ukishavuka iko kipnd hutalia njaa niamn mm na kwa wik moja utakua ushakua masta
 
asante kwa ushauri mkuu umenifungua macho. shida ni kwamba kwa saivi sina source yoyote ya kupata mtaji wa kuanzia natumia laptop ya rafiki yangu kuingia mtandaoni sina smartphone, ndio sababu natafuta kazi nipate nguvu ya kuanzia.
 
habari zenu wana JF,

nimekuja tena kuomba msaada wa kibarua hali imekuwa ngumu, baada ya kuzunguka kutafuta ajira rasmi ya kufundisha kwenye shule bila mafanikio niligeukia kwenye kazi za vibarua kwenye ujenzi angalau niweze kulipa kodi na chakula hapa mjini Dar es Salaam.

Wiki iliyopita ilikuwa ngumu kwangu baada ya kupewa notisi ya mwezi mmoja kuhama ninapoishi hii ilitoka kwa wapangaji wote, balaa limekuja tena nilipotaka kufanya kazi zaidi nipate pa kukukimbilia mwili umekataa kazi, nimepata tatizo la mgongo unauma kuanzia kiunoni na kizunguzungu kikali wajuzi wameniambia inawezekana ni presha ya kushuka. Kwa sasa siwezi kufanya kazi ngumu sana kutokana na hali yangu ya afya.

Ombi langu kwenu mnisaidie kupata kibarua nipate fedha kidogo nisukume maisha huu upepo upite hali ikae sawa. Nipo dar naweza kufanya kazi yoyote ambayo hainihitaji nikae juani sana

Asanteni sana.
Waweza kueleza kwa kifupi;
1. Ujuzi ulionao
2. Elimu na experience yako
3. Eneo ulipo
 
Pole cha punguza mawazo ili presha hyo ikae sawa .
 
Roho imeniuma sana kweli una nia ya dhati mwenye uwezo atakusadia inshallah
Kwani unaonekana mchapakazi ila mi binafsi nimepitia kipind kama icho mpaka nimejiweza bahati mbaya limekuja jamaa kutoka kijijini limekimbilia getto kwangu mwezi sasa eti nikitafutie ajira likiamka ni kuchat na mademu kuwasha tv inauma sana

Ila wewe mungu akusimamie
 
Waweza kueleza kwa kifupi;
1. Ujuzi ulionao
2. Elimu na experience yako
3. Eneo ulipo
asante mkuu, nina degree ya Ualimu masomo ya History na Kiswahili, nina experience ya Mwaka mmoja na miezi miwili kwenye fani ya ualimu. Baada ya kufanya kazi za kujitolea kwenye shule za sekondari niliamua kuacha maana ningekufa njaa. Kwa sasa ninaishi dar es salaam.
 
asante mkuu. naamini kila kitu kitakuwa sawa. ni swala la wakati Mungu ataweka sawa huu upepo utapita.
Asante kwa kujali mkuu.
 
ni
Apo ndo ujue hali si shwali check uzi ulivotulia pengine kila mtu ana shida na kazi au aliyo nayo haimtoshelezi pole ndugu kukosa kazi mjini ni azabu ata ya jela ndogo
kweli mkuu hali sio nzuri sana kwa watu wengi inahitajika kufunga mkanda kweli. Tuendelee kuombeana.
 
Dah tatizo la Ajira inaumiza mno hakika maumivu yake na mm napiTia okay anyway naamin mungu ataTufanyia wepeSi TUSEME AAMIN...
INSHAALLAH..
 
habari zenu wana JF,

nimekuja tena kuomba msaada wa kibarua hali imekuwa ngumu, baada ya kuzunguka kutafuta ajira rasmi ya kufundisha kwenye shule bila mafanikio niligeukia kwenye kazi za vibarua kwenye ujenzi angalau niweze kulipa kodi na chakula hapa mjini Dar es Salaam.

Wiki iliyopita ilikuwa ngumu kwangu baada ya kupewa notisi ya mwezi mmoja kuhama ninapoishi hii ilitoka kwa wapangaji wote, balaa limekuja tena nilipotaka kufanya kazi zaidi nipate pa kukukimbilia mwili umekataa kazi, nimepata tatizo la mgongo unauma kuanzia kiunoni na kizunguzungu kikali wajuzi wameniambia inawezekana ni presha ya kushuka. Kwa sasa siwezi kufanya kazi ngumu sana kutokana na hali yangu ya afya.

Ombi langu kwenu mnisaidie kupata kibarua nipate fedha kidogo nisukume maisha huu upepo upite hali ikae sawa. Nipo dar naweza kufanya kazi yoyote ambayo hainihitaji nikae juani sana

Asanteni sana.
Waweza kueleza kwa kifupi;
1. Ujuzi ulionao
2. Elimu
3. Eneo ulipo
asante mkuu, nina degree ya Ualimu masomo ya History na Kiswahili, nina experience ya Mwaka mmoja na miezi miwili kwenye fani ya ualimu. Baada ya kufanya kazi za kujitolea kwenye shule za sekondari niliamua kuacha maana ningekufa njaa. Kwa sasa ninaishi dar es salaam.
Pole sana Mkuu..

Nimekutumia namba za mtu inbox, wasiliana nae ana shule Kigamboni na Kisarawe. Try your luck, all the best
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom