Nimekuwa nikijiendesha kwa hasara kwa miaka 10

incredible terminator

JF-Expert Member
Aug 1, 2016
2,229
3,525
Nawasalimu kwa jina jamhuri ya muungano,

Leo nilikuwa nafanya mapitio ya mapato na matumizi ndani ya miaka kumi (10) hivi, Nimegundua nilikuwa nikiendesha shirika la mwili wangu na viungo kwa hasara ndani ya miaka kumi. Wakuu nadhani wale wanaoshadadia hoja ya Shirika la ndege Tanzania ATCL kujiendesha kwa hasara na kugundua kulikuwa na uzembe na kutokumanikinika katika shirika hilo wanaweza kuwa pia miongoni mwa wahanga wanaojiendesha kwa hasara pasipokujua.

Kwanza itambulike maana halisi ya neno hasara ni kile kitendo cha kupokea matokeo tofauti na matarajio yaani matokeo kuwa madogo tofauti na matarajio tayari hiyo kiuchumi tunahesabu kama ni hasara.

Sasa ndani ya miaka kumi nimekuwa nikitumia zaidi ya LAKI MbILI kwa mwezi kwa kutengeneza muonekano kuhakikisha navaa Jinsi kali, kiatu kikali, Tsheti kali, Bila kusahau body spry (Perfume) kali, Kichwani vibrichi flani ivi vya kikongo na chenicheni flani ivi vya copy za diamond (fake diamond) kiufupi tu ni kwamba lengo la kufanya haya ilikuwa ni kutengeneza heshima mtaani watu waniheshimu nipate totoz kila nikipita watu wakubali wakiniona, ila chakusikitisha kabisa ni kwamba licha ya kufanya yote nilifanikiwa kuwateka watoto wadogo tu huku nusu ya wanajamii walikuwa wananiona mtu hovyo kabisa, mhuni na hata hizo totoz sikupata yaani kiufupi matarajio na matokea vilienda tofauti kabisa yaani nimekula hasara for 10 years.

Pamoja na kadegree kangu ka Udsm ila bado nimekuwa nikionekana empty head yaani sina chochote kabisa, kinachoniuma hata katika vikao vya familia nilikuwa sipewi nafasi ya kuchangia walijua nafanya fujo tu, hakika nimejiendesha kwa hasara miaka yote 10 najutia sana ila kwa kuwa ninajua huu ni msiba wa vijana wengi wenye vyeti vya elimu ya mkoloni haijaniuma sana maana msiba wawengi hauna kilio.. ila majuto siku zote hayaishi

Cha ajabu miaka miwili nyuma nilipogundua najiendesha kwa hasara nikaamua kuchukua maamuzi magumu ya kubadilisha mfumo wa kujiendesha ili kupunguza hasara, Kwanza advartise inaanza nilinyoa dongo (kipara) nikapunguza gharama za utunzaji wa nywele, pili nikaamua kwenda mtumbani nikatafuta suluali zangu za cardet na mashati ya mtumba kama matatu ghalama haikuzidi elfu 30 ambayo zamani kipindi najiendesha kwa hasara ilikuwa ni ghalama ya kununua Jeans moja aina ya SUPRIME, baada ya kuzivaa automatic nilijikuta naanza kuwapoteza washikaji ,mmoja baada ya mwingine kuna mda nafsi ilianza kunifokea kwa kujisaliti ila nikakaza kama sisikii kile kisauti cha mnong'onezo wa nafsi nikaendelea zile pamba zangu za zamani nikaanza kuzichukia na kutokuzivaa kabisa na baada ya miezi kadhaa nilijikuta nimepata washikaji wengine ambao tulikuwa tunaendana kimuonekano cha ajabu hata kimtazamo pia na hapa nikajifunza kuwa muonekano wa kimavazi na mtazamo na kimavazi havipishani "najua hapa wengi mtanibishia ila poa tu"

Struggle za mtaa zikaanza kwa kasi nikapata vijisenti nikanunua kakiwanja hapa jijini nikakaweka pending nikaendeleza struggle nikawa naweka vitofali kwa awamu vikafika 2000. Nikaweka kamsingi ka kibanda ka vyumba viwili na sebule kwa kuwa ujanja bado nilikuwa nao nikatafta mafundi kijijini ambao nilijua tutendana nao maana hapa mjini mafundi galama kubwa tukaanza kazi, Ishanlah mungu sio athmani hadi sasa najivunia kulipa kodi ya uzalendo wa majengo nikiwa kwangu,

MATOKEO, Baada ya kamda kidogo nikashangaa ile hali ya kunyoa kipara ikanizoea zamani nilikuwa nikinyoa dongo (kipara) naonekana kituko maana kichwa kilikuwa kikavu kama jiwe ila cha kushukuru mungu baada ya mda kidogo kichwa kimeota viminofu flani ivi nikinyoa ndongo vinaenda saresare maua! mungu kanijalia kakitambi flani ivi nikivaa yale mashati yangu vinaenda saresare maua, sasa hivi nikivaa zile nguo nitaonekana kituko mbele ya jamii,

Picha linaendelea baada ya mda baada ya kuhamia kwangu harsoling zikaendelea nikapata kausafiri kakutumbukia ijapokuwa mwanaume anatakiwa awe na gari la kupanda sio lakutumbukia ila ishanlah wote tunaitwa madereva no otherwise
Kwa sasa totozi zinajileta zenyewe na ni mwendo wa kuzipandishia vioo (kuzireject) na sina kabisa mda nazo, Jamii inayonizunguka nikipita hata nikiwa kwa mbali naskia salam, madogo wa rika langu wote wananita BRAZA, na katika vikao vya familia mimi ndio wa kwanza kualikwa na nikisimama kuchangia hoja wote wananyamaza kusikiliza nini nitasema japokuwa ni lastborn.
Ila yote kumi bado sijaacha kujutia miaka kumi (10)yote niliyowahi kujiendesha kwa hasara

WADAU TUPEANE UZOEFU KWA WALIOWAHI KUJIENDESHA KWA HASARA, NA ILIKUWA MIAKA MINGAPI NA ULIJUAJE NA ULICHUKUAJE MAAMUZI YA KUTOKA, HII THREAD ITASAIDIA KUWAKUZA KIAKILI WADOGO ZETU WANAOJIENDESHA KWA HASARA
 
We umeshtuka umejiendesha kwa hasara mapema, Kuna wenzio kwanza hata hawajui kama wanajiendesha.😊
 
Ni mambo ya rika katika kukua na lazima kila mtu apitie....ila miaka mi 10 ni mingi sana ambayo huwezi kuirudisha.....tumia nguvu kutopoteza tena miaka 10 mengine kwa maendeleo madogo uliyopata
 
Back
Top Bottom