Hii inaitwa kujiendekeza, naona ajabu hata shetani hujamsingizia pia,
Katika dunia hii ukitaka Kila kitu kisikupite basi ndio chanzo kikubwa cha kumuasi mungu,
Kuna kipindi nilitaka kukaribia rekodi zako kwa mbali, Lakini niliwahi kustuka, hatua nilizofanya Kwanza siendi sehemu yyte ambayo itanikutanisha na wanawake hovyo, nilifuta social media zote situmii, fb, insta, badoo, na nyingine nyingi zinazoleta sababu ya kuchat na wanawake hovyo,
Pia nilipoowa nikaamua kuridhika na mke wangu tu,
Kwa sasa nina miaka mingi sana nimeweza kucontrol hali hiyo,
Kingine lazima ujenge tabia ya kuwahi kurudi home, usigawe namba yako hovyo, jitahidi sehem nyingi ukitoka kwenda kwenye starehe beba mkeo muende wote,
Jiwekee ahadi ya kutokulala nje hata kama ukichelewa kurudi home Lakini rudi tu na ulale home, kama utakuwa mji wako,
Ondoa kabisa list ya marafiki wenye akili kama ulizonazo sasa,