Nimekuwa mtumwa wa wanawake

Mtu mzito

JF-Expert Member
May 13, 2016
1,779
3,183
Salaam ndugu zangu,

Nimeficha ficha haya mambo ila najiona kabisa naangamia hivyo ni bora leo niombe ushauri maana hapa pana watu wazima, wanasaikolojia na viongozi wa dini.

Mkasa wangu ni wa hakika na bado nipo katika mateso hata sasa.

Wakati nipo balehe nilikutana na wasichana mbali mbali waliouteka moyo wangu na nikawaeleza hisia zangu, kwa bahati mbaya nilijibiwa karaha na kutoswa sababu ya maisha yangu ya dhiki.
Hali ilikwenda hivyo kwa muda mrefu mpaka moyo wangu ukajenga chuki na wanawake, niliwaona hawana usawa na sio wa kuwa nao karibu.

Katika utafutaji wangu wa maisha ghafla mambo yakabadilika na nikawa nina pesa na kuishi vizuri na nikaanza kujenga nyumba na pia nikawa na miradi pamoja na gari ya kutembelea.

Ni hapo ndipo wasichana wakaanza kuwa karibu na mimi na kunihitaji kimapenzi, na mimi nilishajenga chuki moyoni na nikapanga kuwakomoa, nikajikuta natembea na wanawake wengi tofauti kuanzia wanafunzi, walimu, wasichana tu wa mtaani, machangudoa na wapenzi wa watu.

Nikajikuta dhaifu mbele ya wanawake yaani siwezi kulala hata siku moja peke yangu bila mwanamke na pia mda mwingine nilifanya mapenzi na wasichana wawili tofauti kwa siku moja, haswa kama huyo wa pili aliyenitafuta ni mzuri sana.

Haya mambo sipangi bali najikuta tu inatokea na kila nikimaliza najuta na kusema ndio mara ya mwisho ila punde tu naingia katika vishawishi tena, nilioa mke safi kabisa ili niepuke hali hii ila tuliachana baada ya kunifumania mara kadhaa.

Sasa nina mke mwengine na safari hii nimeoa mke wa ndoto yangu mtoto mzuri sana shombe shombe kiasi kwamba marafiki wanasema kweli mwamba umepata kifaa.

Ila bado ninajikuta natembea na rafiki zake pia wasichana wa mtandaoni kama vile Jf, Badoo, Fb nk na pia nimekuwa maarufu madanguro mengi sana mpaka naona noma.

Mara kadhaa nasafirisha mademu wakali toka mikoa tofauti na kunifuata mimi, sihongi sana na wala sijatetereka ki uchumi na wala sijaathirika ila tu najiuliza nini kipo nyuma ya nguvu hii inayonishinda kujizuia?

Kilichonifanya nijione naingia katika hatari ni kwamba, juzi kushinda jana nilikwenda guest na msichana fulani nilikutana nae juu juu tu, tukafanya mapenzi na tulipomaliza wakati tunatoka kuna jitu la miraba minne lilikuwa likituangalia sana na yule msichana akashtuka sana.

Baadae nilipomuuliza akasema yule jamaa anafanya kazi na mume wake ni FFU kitengo cha doria.

Hakika nikaona hiki ni kifo cha wazi sasa na nimefikia pabaya, haya mambo sipangi ila imekuwa kama ulevi na siwezi kuacha.

Naombeni ushauri wa kunijenga wadau
 
Salaam ndugu zangu
Nimeficha ficha haya mambo ila najiona kabisa naangamia hivyo ni bora leo niombe ushauri maana hapa pana watu wazima, wanasaikolojia na viongozi wa dini.

Mkasa wangu ni wa hakika na bado nipo katika mateso hata sasa

Wakati nipo balehe nilikutana na wasichana mbali mbali waliouteka moyo wangu na nikawaeleza hisia zangu, kwa bahati mbaya nilijibiwa karaha na kutoswa sababu ya maisha yangu ya dhiki.
Hali ilikwenda hivyo kwa muda mrefu mpaka moyo wangu ukajenga chuki na wanawake, niliwaona hawana usawa na sio wa kuwa nao karibu.

Katika utafutaji wangu wa maisha ghafla mambo yakabadilika na nikawa nina pesa na kuishi vizuri na nikaanza kujenga nyumba na pia nikawa na miradi pamoja na gari ya kutembelea.

Ni hapo ndipo wasichana wakaanza kuwa karibu na mimi na kunihitaji kimapenzi, na mimi nilishajenga chuki moyoni na nikapanga kuwakomoa, nikajikuta natembea na wanawake wengi tofauti kuanzia wanafunzi, walimu, wasichana tu wa mtaani, machangudoa na wapenzi wa watu.

Nikajikuta dhaifu mbele ya wanawake yaani siwezi kulala hata siku moja peke yangu bila mwanamke na pia mda mwengine nilifanya mapenzi na wasichana wawili tofauti kwa siku moja, haswa kama huyo wa pili aliyenitafuta ni mzuri sana.

Haya mambo sipangi bali najikuta tu inatokea na kila nikimaliza najuta na kusema ndio mara ya mwisho ila punde tu naingia katika vishawishi tena, nilioa mke safi kabisa ili niepuke hali hii ila tuliachana baada ya kunifumania mara kadhaa.

Sasa nina mke mwengine na safari hii nimeoa mke wa ndoto yangu mtoto mzuri sana shombe shombe kiasi kwamba marafiki wanasema kweli mwamba umepata kifaa.

Ila bado ninajikuta natembea na rafiki zake pia wasichana wa mtandaoni kama vile Jf, Badoo, Fb nk na pia nimekuwa maarufu madanguro mengi sana mpaka naona noma.

Mara kadhaa nasafirisha mademu wakali toka mikoa tofauti na kunifuata mimi, sihongi sana na wala sijatetereka ki uchumi na wala sijaathirika ila tu najiuliza nini kipo nyuma ya nguvu hii inayonishinda kujizuia?

Kilichonifanya nijione naingia katika hatari ni kwamba, juzi kushinda jana nilikwenda guest na msichana fulani nilikutana nae juu juu tu, tukafanya mapenzi na tulipomaliza wakati tunatoka kuna jitu la miraba minne lilikuwa likituangalia sana na yule msichana akashtuka sana.

Baadae nilipomuuliza akasema yule jamaa anafanya kazi na mume wake ni FFU kitengo cha doria.

Hakika nikaona hiki ni kifo cha wazi sasa na nimefikia pabaya, haya mambo sipangi ila imekuwa kama ulevi na siwezi kuacha.

Naombeni ushauri wa kunijenga wadau
Sikulaumu kwa unayoyafanya kwa sababu inaonekana umeathirika kisaikolojia. Ile hali ya kutoswa ukiwa huna pesa ndio inakufanya uwashushe thamani wanawake na kuona kama ni chombo cha starehe.
 
Ndugu sijui wewe dini gani, pia Mimi sio Mchungaji. Ila kuna hili jina huwa wanalitaja wanasema YESU.

Hili jina ukiliita na kusema YESU NISAIDIE NIACHE HIKI KITU nauhakika utaacha. Baada ya hapo chukua initiative za kuwatafta viongozi wa makanisa ya kilokole kwa mfano TAG, EAGT, CAG, PAG hayo hayana longo longo. Usiende yale ya miujiza unless Mungu akuongoze uingie huko kuomba msaada.

Ukitaka kuacha Fanya hili Mkuu.
 
Mkuu ni vizuri umegundua tatizo. Ukiamua na ukadhamiria kwa dhati kabisa kuacha...kwa uhakika kabisa utaacha. Kwasasa naona umekuwa ni mtumwa wa hisia zako (kwa kutii mahitaji/matamanio ya mwili wako) japo utaangamia usipochukua hatua haraka. Kama itawezekana na kama mkeo ni open minded nashauri umshirikishe. Atakuwa mtu wa msaada kwako sana...
 
Hii inaitwa kujiendekeza, naona ajabu hata shetani hujamsingizia pia,
Katika dunia hii ukitaka Kila kitu kisikupite basi ndio chanzo kikubwa cha kumuasi mungu,
Kuna kipindi nilitaka kukaribia rekodi zako kwa mbali, Lakini niliwahi kustuka, hatua nilizofanya Kwanza siendi sehemu yyte ambayo itanikutanisha na wanawake hovyo, nilifuta social media zote situmii, fb, insta, badoo, na nyingine nyingi zinazoleta sababu ya kuchat na wanawake hovyo,
Pia nilipoowa nikaamua kuridhika na mke wangu tu,
Kwa sasa nina miaka mingi sana nimeweza kucontrol hali hiyo,
Kingine lazima ujenge tabia ya kuwahi kurudi home, usigawe namba yako hovyo, jitahidi sehem nyingi ukitoka kwenda kwenye starehe beba mkeo muende wote,
Jiwekee ahadi ya kutokulala nje hata kama ukichelewa kurudi home Lakini rudi tu na ulale home, kama utakuwa mji wako,
Ondoa kabisa list ya marafiki wenye akili kama ulizonazo sasa,
 
Pole sana kwa kuwa mtumwa. La msingi ni wewe mwenyewe kuamua kwa dhati ya moyo wako kuacha na si kujidanganya mdomoni. 1. Tumia muda mrefu kukaa na watu unaowaheshimu watakusaidia kwani utaona aibu kuzungumza ujinga wako.
2. Pili, piga magoti omba msamaha kwa MUNGU na uwe nadhiri ya kuacha.
3. Ukishindwa kabisa kuwa unaongozana na shemeji yako wa kiume unayemheshimu muda unapokuwa mbali na mkeo.
 
Sikulaumu kwa unayoyafanya kwa sababu inaonekana umeathirika kisaikolojia. Ile hali ya kutoswa ukiwa huna pesa ndio inakufanya uwashushe thamani wanawake na kuona kama ni chombo cha starehe.
Hakika mkuu, yaani nateseka
 
Sioni ubaya wowote.si hela yako ndo inakuzuzua? Filisika ndo utawajua wanawake. Hata hukumbuki kwamba ulitoswa huko nyuma kwa ufukara wako.

Endelea kupiga show sana, zitakoma zenyewe kutokana na umri wako au utakapofilisika
 
Kwa kweli nimefurahi sana kusikia matatizo uliyonayo kwani hata mie nina tatizo hilo hilo.
Ki umri nina miaka 56 nina watoto na wajukuu, tatizo langu pia ni kuwa kila mara nimekuwa nikiwazia wanawake tu, kiukweli nawatamani sana hasa wanawake wenye matako makubwa na walio weupe.
Niko radhi kumfuatilia hadi nimpate, bahati nzuli ni wanawake wachache sana huwa wananikataa.
Ndugu zangu nami naomba mnisaidie mawazo nifanyeje ili niachane na kuwatamani wanawake maana umri umeisha kwenda lakini pepo wa kina mama haunitoki!!!
 
Ndugu sijui wewe dini gani, pia Mimi sio Mchungaji. Ila kuna hili jina huwa wanalitaja wanasema YESU.

Hili jina ukiliita na kusema YESU NISAIDIE NIACHE HIKI KITU nauhakika utaacha. Baada ya hapo chukua initiative za kuwatafta viongozi wa makanisa ya kilokole kwa mfano TAG, EAGT, CAG, PAG hayo hayana longo longo. Usiende yale ya miujiza unless Mungu akuongoze uingie huko kuomba msaada.

Ukitaka kuacha Fanya hili Mkuu.
Akhsante mkuu, nitafuata ushauri wako
 
Mkuu ni vizuri umegundua tatizo. Ukiamua na ukadhamiria kwa dhati kabisa kuacha...kwa uhakika kabisa utaacha. Kwasasa naona umekuwa ni mtumwa wa hisia zako (kwa kutii mahitaji/matamanio ya mwili wako) japo utaangamia usipochukua hatua haraka. Kama itawezekana na kama mkeo ni open minded nashauri umshirikishe. Atakuwa mtu wa msaada kwako sana...
Sawa mkuu, wife nikimshirikisha hataniona muhuni kweli?
 
Back
Top Bottom