hahaha lakini mtambuzi ukimwi unaweza kuambukizwa kwa miswaki kukaa pamoja kweli ???ikiwa kila mtu anapomaliza kuswaki anasafisha mswaki wake na maji
mwingine anaweza akajijuwa kuwa muathirika, na kama una ubaya nae..njia rahisi ya kukumaliza anatumia mswaki wako kwa kuuweka tone za damu yake
so wakati wa ww kupiga, ukijeruhi fizi zako imekula kwako!!
Aisee mi hiyo kitu siiwezi....hata kushea dawa na mtu naonaga kazi
duhhh wangu pia unakaa bafuni na bafu letu tunatumia wawili tu mimi na dada sijui nihamishe ingawa haikai pamoja
Ku share dawa gani mkuu
ukimkorofisha huyo dada ana usugulia choo huo mswaki!!!
Dawa ya meno......huwa najisikia vibaya yan sipendi kabisa kuchangia
![]()
Hii nimekutana nayo mahali na ni nyumba ambayo inaishi wapangaji, sina uhakika kama ni miswaki ya familia moja.
Namna hii ya kuhifadhi miswaki imenifikirisha kidogo. Tunaambiwa kwamba maradhi kama Ukimwi unaweza kuambukizwa kwa kuchangia pamoja na vitu vingine lakini pia miswaki imetajwa. Ukiangalia namna miswaki hii ilivyowekwa naona ni sawa tu na kuchangia miswaki.
Labda tu niwaulize tu wenzangu, je huwa mnaweka miswaki yenu hapo nyumbani kwenu namna gani?