uwiiiiiiii
JF-Expert Member
- Jul 11, 2016
- 341
- 365
Habari zenu wadau wa humu,
Ushauri wa shosti wangu alinishauri kwenda katika bar mume wangu anayokaa, nikaamua kwenda kula katikati hapo na kujaribu kuwazoea kupitiliza, siku moja nikaenda nikamkuta muuza nyama amekaa na mdada kwa jinsi nilivyomzoea nami nikakaa kwenye hiyo meza Duh! Kumbe ndio mchepuko wa mume wangu.
Jamani nilichoka sana nikaishia kumuangalia tu, kwa uchunguzi niliyofanya kwanza anatembea na muuza nyama, na pia ana bwana mwingine hapo rafiki wa muuza nyama, ni mdada yule kuchukuliwa na wanaume wa bar ndio zake, niligundua ni mtu mzima sana nilishangaa na kushindwa kumuelewa mume wangu kabisa.
Wanaume hivi ni kwanini mnapenda kujidharaulisha hivyo? Kibaya bar nzima inajua, nimezidi kupoteza hisia kabisa mwenzenu.