Nimekutana na Jini?

Nimekutana na Jini?

RRONDO

Platinum Member
Joined
Jan 3, 2010
Posts
57,806
Reaction score
129,656
Ndugu zangu mimi sio muumini wa haya mambo, sijui majini wanga siamini kama yapo. Ila leo kuna kitu kimenitokea kinaweza kubadili maoni yangu juu ya hivi viumbe.

Kama mjuavyo mwisho wa wiki huu unapilika nyingi za usiku na mimi leo nilikuwa kwenye misele ya usiku. Sasa wakati narudi mida ya saa kumi na robo hivi alfajiri hii nimeona vitu naona si vya kawaida.

Wakati narudi nyumbani niko peke yangu kwenye gari na barabarani ghafla akatokea paka mweupe anakatiza barabara . Kwa kawaida usiku huwa nakimbiza gari kidogo na ninaendesha katikati ya barabara, basi yule paka katokea upande wa kushoto anakatiza kueleke kulia.

Kwa instict za udereva nikanyunyiza breki kidooogo, nikahamia kushoto alipotoka nikamkwepa bila kashkashi. Kuangalia nyuma kwa kutumia vioo sikumuona yule paka! Kwenda mbele kama mita kumi nikamuona mwanamke wa kizungu 'blonde' kavaa gauni jeusi refu limefunika hadi viatu kasimama upande wa kulia wa barabara!

Nikamwangalia na yeye akaniangalia wakati napta macho yalipogongana mwili wote ukanisisimka! Kwa mazingira yale niliomkuta na muda huu si kawaida kukuta mwanamke kasimama peke yake awe wa kizungu au mswahili, ndugu zanguni huyu ni jini? Nimeandika hii habari kabla sijalala mkiona nipo kimya sana mjue ni athari za huyo 'jini'.

cc: mshana jr
 
Kuna watu wakija hapa wataanza kuhoji kama na wewe ni mwanaume wa Dar
Ila mimi naamin tukio hilo linaweza kutokea popote iwe kibaha au Dar
Sasa inawezekana umekutana na shumileta kweli au umenichanganya mwenyewe maisha yenyewe haya yanapagawisha usiku wenyewe mdogo hata kulala hulali va kutosha. Kuna magonjwa ya mfumo wa akili unakuta unaona maluelue.. Wengi tunakuwa ma crazy bila kujijua kajipime.. Kama upo Dar nenda pale regency hospital
 
Kwajinsi ulivomuelezea huyo mwanamke alivo huyo si binadamu wa kawaida. Huwezi kufa sali tu ulale. Nilishakuta wachawi wawili wameanguka nikasimamisha gari nikawapiga full light nikakaa kama dakika tano nawaangalia huku natafakari niwagonge niwauwe au nifanyeje. Nao wananiangalia tu. Nikaamua kuwaacha nikaenda zangu home. Huwa najiuliza ningewakanyaga kuwauwa sijui nini kingenitokea. Maana sikua mtu wa kusali kipindi hicho. Hapo nilikua nmetoka club pombe kichwani
 
Hakuna bidhaa ya aina hii katika ulimwengu halisi no something like that exist in the real world

Hofu. woga, paniki na simulizi za uwepo wa majini zilizojazwa ufahamu wako , zilizuia udadisi halisi juu ya ulichokiona.
Ukakimbilia kwenye suluhisho batili.
Katika ulimwengu wa fikra pevu, akili kubwa, great thinkers,

Ambao ndio ulimwengu wa kweli hatuna kitu kama hicho.

Kumbuka 'mawazo' huumba hivyo vitu yaelekea uliviumba au kuvibadili mambo kwa hofu Na yoga
Think twice.
 
Pole sana kwa tukio hili,mshukuru Mungu uko salama na endelea kukemea uondoe hiyo hofubuliyoipata na kufukuza kila aina ya mikosi inayoweza kukuatulia .
 
Ndugu zangu mimi sio muumini wa haya mambo, sijui majini wanga siamini kama yapo. Ila leo kuna kitu kimenitokea kinaweza kubadili maoni yangu juu ya hivi viumbe.

Kama mjuavyo mwisho wa wiki huu unapilika nyingi za usiku na mimi leo nilikuwa kwenye misele ya usiku. Sasa wakati narudi mida ya saa kumi na robo hivi alfajiri hii nimeona vitu naona si vya kawaida.

Wakati narudi nyumbani niko peke yangu kwenye gari na barabarani ghafla akatokea paka mweupe anakatiza barabara . Kwa kawaida usiku huwa nakimbiza gari kidogo na ninaendesha katikati ya barabara, basi yule paka katokea upande wa kushoto anakatiza kueleke kulia.

Kwa instict za udereva nikanyunyiza breki kidooogo, nikahamia kushoto alipotoka nikamkwepa bila kashkashi. Kuangalia nyuma kwa kutumia vioo sikumuona yule paka! Kwenda mbele kama mita kumi nikamuona mwanamke wa kizungu 'blonde' kavaa gauni jeusi refu limefunika hadi viatu kasimama upande wa kulia wa barabara!

Nikamwangalia na yeye akaniangalia wakati napta macho yalipogongana mwili wote ukanisisimka! Kwa mazingira yale niliomkuta na muda huu si kawaida kukuta mwanamke kasimama peke yake awe wa kizungu au mswahili, ndugu zanguni huyu ni jini? Nimeandika hii habari kabla sijalala mkiona nipo kimya sana mjue ni athari za huyo 'jini'.

cc: mshana jr
Una bahati weye MWe kuliona jini LA kizungu!!!!
 
My dear polee na wala usiwe na hofu siwezi kukudhuru, nilitaka kukupa sapraiz tu kuwa nipo na nakuona kila utakapokwenda
hizo sapraiz nyingine tunaweza kuuana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom