Hao wanaosema kuwa umeniumiza moyo wangu wapo sawa hata wanaosema umeiumiza roho yangu pia wapo sawa. Hata atakaesema umeniumiza ubongo wangu pia yupo sawa. Kwasababu hisia ya mapenzi huviunganisha hivyo vitu vitatu ndio maana, ukiona mtu kaachwa mara hufanya mambo ya ajabu kutokana ubongo umezidiwa na hisia za mapenzi. Moyo hupiga kwa kasi au kuna wengine hupata presha hii pia moyo umepata mshtuko wa hisia ya mapenzi. Na roho hapa huanza kuyachukia maisha kutokana na kukosa hisia za mapenzi. Kama utasoma hapo unaposema rafiki yako aliposema akiachwa na huyo demu ataumia sana. Hio inatokana na huyo rafiki yako amezizamisha hisia zake kwa huyo mwanamke.