Nimekumbuka zamani

Haya maisha asiyewahi kuishi haoni raha yake,. Maisha ya kwa bibi ni raha sana aisee inakeraga ile wiki ya mwisho mda wote mnawaza mnajua safari ya kurudi imewadia
 
Yeah mkiwa wengi kila mtu na kitu chake😃😃😃,. Hujai kuenjoy Ps like seriously??
 
Mkuu; Hebu fikiria maisha yalivyo sikuizi; halafu inakuja "Kampuni" sukari kg.1 ni siku mbili tu imeisha na kati ya hao walokuja hakuna aliyeleta hata nusu kilo ya sukari. Ni gharama aisee.
Sema sijui hawa wazee hela walikuwa wanatoaga wapi?,. Maana kwenye suala la kula kuanzia asubuhi mpaka usiku na wanalisha wajuu na wanafamilia kibao aisee walijitahidi
 
Tv zile za chogo mkuu,. Hahhah 🤣🤣🤣mapera naa zambarau zilikuwepo ( kwanza zilivyokua zinaweka madoa kwenye nguo )
 
Siku zinasogea saaana aisee,. Ila maisha ya kuishi ndugu wengi pamoja ni raha sana
 
Ila hii nayo ni zuri watoto wanajifunza kazi mapema
 
Nyie mlikuwa wajukuu wa kishua. Mambo ya CD na snacks.

Sisi mizecho yetu ilikuwa kombolela, na kuiba kamba za bibi tunafunga bembea zile za kwenye mti . Halafu kuna kwenda kuogelea mtoni huko na kula vimatunda pori.
Sana yaan 🤣
 
Kama nakuona kombolela unae da jificha na crush wako alafu anaanza kukuchungulia kama umevaa chupi 🤣🤣🤣🤣
 
Sema sijui hawa wazee hela walikuwa wanatoaga wapi?,. Maana kwenye suala la kula kuanzia asubuhi mpaka usiku na wanalisha wajuu na wanafamilia kibao aisee walijitahidi
Halafu hao Wazee waliolisha familia kibao, walikuwa na maisha ya kawaida tu, siku hizi mtu ana nyumba ya ghorofa yenye vyumba kibao, magari na biashara, lakini kwake hataki mgeni zaidi ya mke wake, house girl/houseboy na watoto tu 😁 Leejay49
 
Wewe ni kavivu😆
Siku mbili tu baada ya kufunga shule ilikuwa ni safari ya kutoka Moro to Dar hata kwa kutoroka kwenda kwabibi Mwananyamala Komakoma so huku hakukua na Ng'ombe zaidi ya kujimix na vijana wa uswazi na kupiga dili tu za pesa
 
Halafu hao Wazee waliolisha familia kibao, walikuwa na maisha ya kawaida tu, siku hizi mtu ana nyumba ya ghorofa yenye vyumba kibao, magari na biashara, lakini kwake hataki mgeni zaidi ya mke wake, house girl/houseboy na watoto tu 😁 Leejay49
Sometimes huwa nahisi ni uchoyo tu na ubinafsi hakuna kingine
 
Tunawinda kwa manati, tunafora monjo ukutani, kombolela, ukuti na mnazi, kuruka kamba, tunacheza kibaba na kimama n.k harafu uwe watoto kwenye Nyumba za laini hivi mfano NHC watoto jioni tumejaa kwao na flani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…