Nimesoma posts zote, zimenifurahisha sana, yaani jinsi mnavyokumbukia utoto wenu (enzi za utoto) shuleni, nyumbani n.k.
Mimi nina mengi sana ninayoyakumbuka........nilikuwa na wadogo zangu, tulikuwa tunapenda sana mpira wa miguu, kwa vile tuliishi jirani kabisa na uwanja wa kumbukumbu ya Karume, pale ilala, tulikupenda sana kwenda kuangalia mecchi pale. Baba na Mama hawakupenda kabisaaaa kusikia habari za mpira, hivyo hatukupewa hata SENTI TANO za kiingilio. Matokeo yake tulikuwa tunaruka ukuta, nakumbuka tulikimbizana sana na polisi wenye farasi na mabomu ya machozi yalitutesa sana, maana si sisi tu tuliokuwa tunaruka ukuta. Tukirudi nyumbani sasa..... si unajua kuparamia ukuta ni lazima uchubuke, bakora za baba na makofi ya mama, utakoma.....cha ajabu hatukuacha kwenda mpirani hata siku moja, si ajabu leo hii kukosa mechi pale uhuru stadium au national stadium ni nadra sana (ila siparamii ukuta siku hizi si ulikuwa utoto tu, nimekua nimeacha)
Ila naomba kuwauliza wanaJF wenzangu, malezi au maisha tuliyokuwa nayo wakati ule na hivi sasa tumekuwa wakubwa tuna familia na watoto wetu, Je yamekusaidia? Yaani kwa mfano baba yetu alisisitiza sana elimu na akapigania hadi watoto wake wote (tuko saba), walipata elimu hadi ya vyuo vikuu, alitulea vizuri kiasi kwamba najivunia malezi yake. Pia baba yetu alikuwa mkali sana, kiasi kwamba hata kwa mtoto wa kiume kama mimi nikirudi nyumbani saa 2 usiku naulizwa nilikuwa wapi, nikishindwa kujibu ni kichapo tu! Hii iliendelea hadi nilipoanza kazi nikiwa naishi kwa wazazi (kula kulala). Kwa kweli sijutii malezi yale maana naishi vizuri na watu kila ninapokuwa. Huwa naukumbuka kwa furaha wimbo wa DDC Mlimani Park:
"NAWASHUKURU WAZAZI WANGU WAKATI WOWOTE,
USHAURI WAO UMENILETEA MAFANIKIO MEMA,
SASA NAISHI NA WATU VIZURI......................."