Nimekubali nimefilisika, kwa sasa natuliza ubongo

Nimekubali nimefilisika, kwa sasa natuliza ubongo

Pole sana.
Ingawa imani ni nzuri ila kupeleka fungu la 10 kwa hela ya mkopo si sahii. Fungu la 10 ni hela iliyofanya kazi na faida ndio inatoa fungu la 10 sio mtaji....

All in all wish you all the best kwenye mapambano. Haina kufeli.
 
Kwenye downfall Yako hakuna gambling/kamari?

Najua ipo kwenye list ila huwezi kuisema hapa
 
Pesa ya riba unapeleka fungu la kumi ? Kubali matokea , kawaida sana .
 
Huyu ni mpuuzi sana humu ndani , hana akili kabisa ata kwa maandiko yake mengine, mtu anapitia msongo ila yeye cha kwanza anafanya masihara ili tu kumdhooifisha. Tlaatlaah wewe ni fala zaidi ya fala na unajijua vizuri.
backward Never Forward Ever gentleman,

huna haja ya kuweweseka na kuendekeza mihemko nonsense kwasababu ya uvivu wako katika kazi na unaokufanya ujikute una chuki binafsi zisizo na kichwa wala meno,

kwani backward Never Forward Ever ni nini kwako gentleman?

ni tusi?
unyonge wa kiuchumi usikufanye uwe na mihemko useless jukwaani 🐒
 
Mimi hapa muuza viat nilikua mbishi kwa kuukataa ukwel mchungu kuwa nimefirisika hatimaye nimekubal kuwa nimefirisika biashara zangu zote zimekufa.

Mwaka 2022 soko liliungua kinomanoma na mim nikiwa miongon mwa waathirika kutokana na presha kwamba labda tunaweza tukazuiwa kurud kufanya shughuli zetu ndani ya soko tukalazimika kutumia nguvu kubwa kuhakikisha tunarud na kujenga mabanda kwa haraka km zali tulifanikiwa lkn kwa upande wangu biashara hazikwenda vizur na kupelekea biashara kusinyaa mdogomdogo baada ya kula faida nililazimishwa kula mtaj huku nikijifarij ipo siku mambo yatakua sawa huku nikiendelea kuchukua hatua mbalimbali km kumwaga sana maji ya upako,kuwaleta wanamaombi na kuendelea kutoa fungu la kumi ingawaje biashara haizalishi faida.

Baada ya kupambana zaid ya mwaka unusu niliona hapa nalazimika kutia busta labda itakaa sawa nilienda bank nikakopa m30 na nikailipia fungu la kumi na mimi mwenyew nilikua sijajinunulia mahitaj kitambo nikajipendelea nafika hom waif ananishangaa mbona yey sijamkumbuka nae nikampa nageuka pemben nawaona watoto nao wananiangalia hawaongei kitu nao nikawapa nakuja kuangalia salio nimebakiwa na m18 duu! Nikajipa moyo kwa vile ina upako hakuna kitakachoharibika mzee mzima nikaingia mtumban.

Nilikomaa mpaka Feb mwaka huu kausha damu wa mule sokon wote walikua wananijua wote niliwakopa na nikashindwa kuwalipa kwa sabab biashara ilishajifia angalau ule mkopo wa bank ulilipwa kwa pesa ya kod ya kibanda na kausha damu walishindwa kukitaifisha hiki kibanda kwa sabab waif alishashtukia anguko langu kitambo akabadili jina la umiliki ktk vitu vyangu vingi tu kwa sabab niliwah kuuza daladala tatu zilikuwa zinapiga ruti ya tandika mwanagati bila kumshirikisha.

Nimekubal nimefirisika kwa sasa natuliza ubongo nadhan mwakan nitaanza tena harakat
Man himself bila kuchoka lolote linaweza tokea mpambanaji
 
Mtu anaacha kuchangia mada anakosoa herufi moja tu 🙌
nimesahihisha sijakosoa gentleman, acha upotoshaji.


kwani ni kitu kibaya kusahihisha ambacho sio sahihi jukwaani gentleman?

hujui kwamba kufirisika na kufilisika ni vitu viwili vyenye maana tofauti kimantiki katika kiswahili sanifu? Au unadhani mtoa hoja kafanya makusudi kukosea? Si na yeye ni binadamu anaweza kukosea na kusahihishwa?

huenda wew upo JF kufuata mkumbo tu au kujifurahisha tu gentleman, lakini sio kujifunza na uongeza maarifa, uelewa na ufahamu wako dhidi ya mambo mbalimbali ya kijamii, kisiasa na kiuchumi.

acha mihemko nonsense,
ukipata changamoto kwenye chochote kile unachofanya maishani mwako,

Backward Never Forward Ever, sawa gentleman?🐒
 
Kwenye hii Titanic ya kiuchumi tupo wengi sana Chief,kama nguvu ipo kidogo tafuta Bajaj used 1 jisajili bolt. Hii itakusaidia kukamata hizi elf 50-60 za kila siku kuishi wakati bado unaumiza kichwa kwa ajili ya move nyingine kubwa.
Kutoka kumiliki daladala 3.
Hadi kuendesha Bajaj ya bolt siyo kazi rahisi.
Inabidi akajaribu kutafuta mji mwingine ndipo atakuwa na ujasiri huo.
Akifanya mchezo atapata uchizi au atakuwa mlevi wa kuhitaji msaada wa tiba ya saikolojia.
 
Kwenye mambo ya biashara hivyo vitu vinatokea Sana, japo kuna vitu tunavikosea Kwa kuwa hatuna Elimu au tunakurupuka....Kwa kuwa ulivipata hivyo vitu Kwa kuanza moja basi unaweza kupata tena Kwa kuanza moja pia, Mimi nahuzunika nikiona mwanaume mwenzangu tena mfanyabiashara akifilisika kabisa maana naujua uchungu wa kurudi chini kibiashara ukoje.
 
Maisha hayajawahi kuwa rahisi hata kidogo, kuna ups na downs nyingi mno katika safari ya utafutaji

Keep hustling 💪
 
Kwenye mambo ya biashara hivyo vitu vinatokea Sana, japo kuna vitu tunavikosea Kwa kuwa hatuna Elimu au tunakurupuka....Kwa kuwa ulivipata hivyo vitu Kwa kuanza moja basi unaweza kupata tena Kwa kuanza moja pia, Mimi nahuzunika nikiona mwanaume mwenzangu tena mfanyabiashara akifilisika kabisa maana naujua uchungu wa kurudi chini kibiashara ukoje.
very hard and painful mzeee it need courage na moyo mkuu kuamka weak mind end up killing themself
 
Daah! Pole sana... kakini mkopo unatolewalaga fungu la 10?, je unatoaje fungu la kumi sehemi ambayo haizalishi? (yaani haitoi faida?), maji ya upako ndo yanazuia nini? (Hizo biashara za watu) "Mungu sio mganga wa kienyeji". Pia, ninavyojua mimi sadaka ni sehemi ya ibada sio kitu cha kubadili mawazo ya Mungu au kuzuia kitu fulani kisitokee (Mungu atabaki kuwa Mungu). Nadhani kuna level fulani ya elimu katika upande wa ulimwengu wa roho mwanadamu anatakiwa awe nayo ili aweze kupambana na chamgamoto za dunia.

By the way kama kuna mjuvi zaidi wa elimu andiko na masuala ya kiroho aje aeleze.....
 
Mimi hapa muuza viatu nilikua mbishi kwa kuukataa ukwel mchungu kuwa nimefilisika hatimaye nimekubali kuwa nimefirisika biashara zangu zote zimekufa.

Mwaka 2022 soko liliungua kinomanoma na mimi nikiwa miongoni mwa waathirika kutokana na presha kwamba labda tunaweza tukazuiwa kurudi kufanya shughuli zetu ndani ya soko. Tukalazimika kutumia nguvu kubwa kuhakikisha tunarudi na kujenga mabanda kwa haraka kama zali tulifanikiwa lkn kwa upande wangu biashara hazikwenda vizur na kupelekea biashara kusinyaa mdogomdogo. Baada ya kula faida nililazimishwa kula mtaji huku nikijifariji ipo siku mambo yatakua sawa huku nikiendelea kuchukua hatua mbalimbali kama kumwaga sana maji ya upako, kuwaleta wanamaombi na kuendelea kutoa fungu la kumi ingawaje biashara haizalishi faida.

Baada ya kupambana zaidi ya mwaka unusu niliona hapa nalazimika kutia busta labda itakaa sawa. Nilienda bank nikakopa milioni 30 na nikailipia fungu la kumi na mimi mwenyew nilikua sijajinunulia mahitaj kitambo nikajipendelea, nafika home wife ananishangaa mbona yeye sijamkumbuka nae nikampa. Nageuka pembeni nawaona watoto nao wananiangalia hawaongei kitu nao nikawapa nakuja kuangalia salio nimebakiwa na m18 duu! Nikajipa moyo kwa vile ina upako hakuna kitakachoharibika mzee mzima nikaingia mtumbani.

Nilikomaa mpaka Feb mwaka huu kausha damu wa mule sokoni wote walikua wananijua wote niliwakopa na nikashindwa kuwalipa kwa sababu biashara ilishajifia, angalau ule mkopo wa bank ulilipwa kwa pesa ya kodi ya kibanda na kausha damu walishindwa kukitaifisha hiki kibanda kwa sababu wife alishashtukia anguko langu kitambo akabadili jina la umiliki ktk vitu vyangu vingi tu kwa sabab niliwahi kuuza daladala tatu zilikuwa zinapiga ruti ya tandika mwanagati bila kumshirikisha.

Nimekubal nimefirisika kwa sasa natuliza ubongo nadhan mwakan nitaanza tena harakati
Financial discipline inaagiza kuwa hela ya mkopo, ambayo inapaswa kurudishwa na riba juu, NI MWIKO kuila.
Unakuala matunda ya kuzungusha mkopo.
Hapo umefilisika kwa kujitakia.
 
unaonae wakati unarelax ukaenda arusha kiserian au burka ukapiga harakati za saidia fundi ili ukirudi huku mjini DSM uwe umeshatuliza kichwa vizuri
 
Yaani unawapelekea fungu la 10 wachungaji wale pesa Yako na pesa Yako yenyewe ni ya mkopo !? Aisee dini kweli ni Toxic

All in all pole sana Kwa yaliyo kufika Muhimu ni kuwa umekubali uhalisia kaa chini jipange upya naamini utatoboa Tena
Hivi kumbe kapelekea wachungaji?😅
 
unaonae wakati unarelax ukaenda arusha kiserian au burka ukapiga harakati za saidia fundi ili ukirudi huku mjini DSM uwe umeshatuliza kichwa vizuri
Hana njaa ya kufikia hatua hiyo kwenda kuwa saidia fundi. Atapambana hapo hapo jijiji Dar atakomaa amelizoea, kwenda kuanza upya Arusha na kupanga ndio anapotea mazima. Ujue ana familia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom