Nimekoswa koswa, kina dada hatari sana

Nimekoswa koswa, kina dada hatari sana

Mkuu inaelekea wewe ni mtu wa kumwaga mapesa sana, hivi hizo hela unazichimba eeeh
 
SIO KILA MWANAMKE WA KUOA YAANI UNA HARAKA SANA NA NDOA MAANA WANAWAKE WA SASA UKITAKA UWASOME VIZURI WEKA NAO UKARIBU TU NA UNAMUULIZA MASWALI TARATIBU KAMA RAFIKI SASA WE UNAPATA LEO KESHO UNATANGAZA NDOA , LAZIMA UJUE UYO MWANAMKE ANA ASILI GANI MWINGINE ANAKUAMBIA MAMA AKE KUMBE NI UMAMA WA KUKUTANA MJINI TU.
 
Msichana wa mtandaoni akikuomba hela ujue anatafuta kitega uchumi. Ila kuna wadada wamekosa aibu!!!! Unaomba hela tu... Tena bila huruma
 
Weeeeeeee mahati haitolewi kwenye akaunti namba weeeeeee in person. Unataka kuwa kama mchaga mwingine alinambia nitume baruwa kwa njia ya posta maana anajua ntaweka na hela ya kusomea baruwa sasa nlichokifanya nlituma na sikuweka hela nasikia alimtuma kaka yake wakaichukue baruwa wamletee yeye
ha ha haaa
 
Acha ufala wa kutoa toa hela hovyo ndio maana wanakuona bwege hawa viumbe sio watu wazur hata kidogo na usimuamini hata kidogo
 
Sasa umenusulikaje wakati haujaoa? Au umesahau michepuko inavyokusubilia
 
Acha wakuchune maana kwanza unaonekana unajitangaza kama una hela. Pia Mwanamke hasa wa hapa dar haumpati leo kesho ukaomba kwenda kwao kujitambulisha. Haya mambo yanakuja "step by step and each step being better than proceeding one"
 
pole mkuu mshukuru mungu kwa hayo pengine ungeoa na ukajutia maisha baada ya kufunga hiyo ndoa kila kitu kinatokea kwa sababu ...
 
Unaonekana una pressure sana ya kuoa vp umri umesonga sana nini? au una mapungufu flani? kuwa mvumilivu ili wapate mda wa kukujua vzr kabla kufanya maamuzi ya kuolewa na ww.
 
Pole sana kaka wapo wengi washaibiwa kwa style hiyo sema tu wanapiga moyo konde kuhonga sana sio tiketi ya kufika kwny ndoa... Ungetafuta taratibu japo ht mm sijafikiria kufany ivo ... Pia upo mchezo mwingne unamwambia tukutane alaf maybe anakwambia sina nauli... Ht km hadi kwao ni mia nne anakwambia nitumie elfu 20 ndo ntakuja baba ukitoa ndo bac. Kwhy swala la kuoa ni nyeti linahitaj taratibu hasa kwa weweee ambaye unadhamira ya kuoa kabixaa...
 
Wana Jf yani nimekoswa koswa vibaya mno, nipeni pole na si rudii tena, nina nia njema ya kuoa lakini sasa nakutana na kina dada ambao sio wazuri, kwanza masharti ya kuoa ni kwamba lazima niende kwao kujitambulisha na nitoe mahari hata kama itakuwa nusu na kuanzia hapo ndio naweza nikanunua zawadi au kumpa pesa anayohitaji na lazima iwe ndani ya uwezo wangu vile vile nitakuwa tayari kuomba papuchi, ila dada zangu wana mpango mwingine ambao sikuutegemea kabisa. Sasa ilikuwa hivi.

1. Nilikutana na dada wa kipare anaishi Moshi tukakubaliana kuoana alichonambia ni kwamba atanipeleka kwao nijitambulishe ila kumchukua rasmi awe mke lazima niwe nimesha nunua gari na nimfungulie biashara ndio atakuja kwangu dah nlichoka sana.

Niliamua kupotea kabisa pamoja na kuwa tumeshazoeana na sikuwahi kumuomba papuchi ila yeye kuomba hela ya matumizi balaa na vocha ahaha nlichoka.

2. Haya nilimtafuta mwingine ambaye anaishi Temeke Dar kwa kujitandia na swala zote yuko vizuri ukimuona utamuona kweli huyu dini anaishikilia sana yeye ni mtu wa Tabora, dah akaomba hela ya chuo nikampa laki na 60 akasema amepoteza simu nikampa tecno ya laki 260

Nikamuomba niende kwao akanipa namba ya ndugu yake eti ndio mama yake mwisho wa siku akaniblock fb, whatsapp cm zangu akawa hapokei tena, kumpigia na cm nyingine akanambia nijiheshimu na nikome kumtafuta mke wa mtu dah nilichoka

Kwanza simu hiyo haikuwa namba yake na majina yake halisi taarifa alizonipa kuhusu kwao na kabila zilikuwa za uongo. Nilichoka sana ila nilimletea noma nikamtangaza fb kiwa ni mwizi akairudisha simu maana sikuwa nimempa na risiti ila pesa ndo hivyo siwezi kuzipata

3. Sikuchoka nikamtafuta mwingine mhehe anaishi tabata tukakubaliana kumbe kadro siku zinavyoenda anaendelea kunisoma kama nina hela, kuna mitandao ya kijamii ambayo alikataa kunambia yumo pamoja na kumuuliza alisema hayupo huko kabisa,

Alikataa kunipa namba ya simu tukaendelea kuchat facebook messenger ila nikaweka mtego wa id nyingine instagram nikamkuta na vidume akisema kuwa ndio mpenzi wake na alikataa katu hana mwanaume dah nilichoka

sikumwambia, nilimuomba mshenga aende kwao akanambia nisubiri siwezi kwenda kwao haraka baada ya wiki 2 akanambia yuko shuleni mtoto wa dada yake amefukuzwa anahitaji sh 188,000 nimrushie kwa wakala yupo karibu dah nikashtuka

Akasema kwann hutaki kujali na kutunza familia yetu, nikashtuka nikamwambia lazima nije nijitambulishe na nitoe mahari kwanza ndio nitakusaidia na hata mimi siombi papuchi, dah kuanzia siku hiyo akasepa wala hataki kuongea na mm nikasema sawa nimeshtuka mapema.

4. Sikuchoka nikamtafuta mwingine mchaga hapo Moshi dah tukakubaliana nikamwambia kwakuwa unaishi mbali na unakofanyia kazi nikulipie chumba mjini halafu niende nyumbani kujitambulisha akakaa muda sana badae akasema nimpe hela aanze kununua vitu vya ndani ataviweka kwao akitaka kuhama atahama navyo

Nikasema sawa nitakupa ila niruhusu niende nyumbani kujitambulisha dah akasema bado mapema nikamuuliza kuomba hela hukuona mapemaeeee, baada ya siku 3 akaomba nimuazime laki 3 anashida atalipa taratibu nikaona huyu anacheza na akili yangu

nikamwambia mke na mume huwa hawakopeshani nikamuomba mshenga apeleke baruwa kwao akasema nimpe kwanza pesa na bada ya wiki atamruhusu mshenga baada ya siku 2 nikamuuliza kwann hutaki kuwasiliana akasema sijampa hela na anashida dah nikafuta namba yake kabisa.

Jamaniee nimekoma kabisaaa sina hamu ya kuchumbia tena labda miaka ijayo.
Mkuu ulikuwa na haraka sana hili jambo lakuoa alina haraka kiivyo ila nakuomba nikuulize kila baada ya mwanamke uliyeachana nae ulikaa mda gani kutafuta mwingine?isitoshe nikupe angalizo mm binafsi ni mchagga ila sitowai diriki kutafuta mwanamke wakichaga kutoka machame,au mwnamke wa kipare ni shida tupuuuuu?????
 
Ila mtoa mada mbona unaonesha haraka sana kwenye kwenda kujitambulisha kwanini usikae na binti mkafahamiana huku ukimsoma taratibu hadi pale utakapojiridhisha ndo uombe kutambulishwa nyumbani.
Hata mm nimemsoma sna
 
Mimi mwanamke akiwa mwepesi wa kuniomba pesa hawezi kuiona kabisa pesa yangu! Lakini asiponiomba na akatoa HUDUMA, huyo atakula sana pesa yangu kupita matarajio yake!
 
Biashara ya kuuza papuchi ipo juu sana sio wanasimama barabarani ila mizinga utakimbia yaani ukiweka mawasiliano utasikia mzimga baby nina shida mara nimeishiwa ya kila aina ya shida, weka urafiki na hii jinsia ndio ujue yupo wakuoa
 
Back
Top Bottom