Nimekoswa koswa, kina dada hatari sana

Keneth12

Senior Member
Oct 12, 2015
114
162
Wana Jf yani nimekoswa koswa vibaya mno, nipeni pole na si rudii tena, nina nia njema ya kuoa lakini sasa nakutana na kina dada ambao sio wazuri, kwanza masharti ya kuoa ni kwamba lazima niende kwao kujitambulisha na nitoe mahari hata kama itakuwa nusu na kuanzia hapo ndio naweza nikanunua zawadi au kumpa pesa anayohitaji na lazima iwe ndani ya uwezo wangu vile vile nitakuwa tayari kuomba papuchi, ila dada zangu wana mpango mwingine ambao sikuutegemea kabisa. Sasa ilikuwa hivi.

1. Nilikutana na dada wa kipare anaishi Moshi tukakubaliana kuoana alichonambia ni kwamba atanipeleka kwao nijitambulishe ila kumchukua rasmi awe mke lazima niwe nimesha nunua gari na nimfungulie biashara ndio atakuja kwangu dah nlichoka sana.

Niliamua kupotea kabisa pamoja na kuwa tumeshazoeana na sikuwahi kumuomba papuchi ila yeye kuomba hela ya matumizi balaa na vocha ahaha nlichoka.

2. Haya nilimtafuta mwingine ambaye anaishi Temeke Dar kwa kujitandia na swala zote yuko vizuri ukimuona utamuona kweli huyu dini anaishikilia sana yeye ni mtu wa Tabora, dah akaomba hela ya chuo nikampa laki na 60 akasema amepoteza simu nikampa tecno ya laki 260

Nikamuomba niende kwao akanipa namba ya ndugu yake eti ndio mama yake mwisho wa siku akaniblock fb, whatsapp cm zangu akawa hapokei tena, kumpigia na cm nyingine akanambia nijiheshimu na nikome kumtafuta mke wa mtu dah nilichoka

Kwanza simu hiyo haikuwa namba yake na majina yake halisi taarifa alizonipa kuhusu kwao na kabila zilikuwa za uongo. Nilichoka sana ila nilimletea noma nikamtangaza fb kiwa ni mwizi akairudisha simu maana sikuwa nimempa na risiti ila pesa ndo hivyo siwezi kuzipata

3. Sikuchoka nikamtafuta mwingine mhehe anaishi tabata tukakubaliana kumbe kadro siku zinavyoenda anaendelea kunisoma kama nina hela, kuna mitandao ya kijamii ambayo alikataa kunambia yumo pamoja na kumuuliza alisema hayupo huko kabisa,

Alikataa kunipa namba ya simu tukaendelea kuchat facebook messenger ila nikaweka mtego wa id nyingine instagram nikamkuta na vidume akisema kuwa ndio mpenzi wake na alikataa katu hana mwanaume dah nilichoka

sikumwambia, nilimuomba mshenga aende kwao akanambia nisubiri siwezi kwenda kwao haraka baada ya wiki 2 akanambia yuko shuleni mtoto wa dada yake amefukuzwa anahitaji sh 188,000 nimrushie kwa wakala yupo karibu dah nikashtuka

Akasema kwann hutaki kujali na kutunza familia yetu, nikashtuka nikamwambia lazima nije nijitambulishe na nitoe mahari kwanza ndio nitakusaidia na hata mimi siombi papuchi, dah kuanzia siku hiyo akasepa wala hataki kuongea na mm nikasema sawa nimeshtuka mapema.

4. Sikuchoka nikamtafuta mwingine mchaga hapo Moshi dah tukakubaliana nikamwambia kwakuwa unaishi mbali na unakofanyia kazi nikulipie chumba mjini halafu niende nyumbani kujitambulisha akakaa muda sana badae akasema nimpe hela aanze kununua vitu vya ndani ataviweka kwao akitaka kuhama atahama navyo

Nikasema sawa nitakupa ila niruhusu niende nyumbani kujitambulisha dah akasema bado mapema nikamuuliza kuomba hela hukuona mapemaeeee, baada ya siku 3 akaomba nimuazime laki 3 anashida atalipa taratibu nikaona huyu anacheza na akili yangu

nikamwambia mke na mume huwa hawakopeshani nikamuomba mshenga apeleke baruwa kwao akasema nimpe kwanza pesa na bada ya wiki atamruhusu mshenga baada ya siku 2 nikamuuliza kwann hutaki kuwasiliana akasema sijampa hela na anashida dah nikafuta namba yake kabisa.

Jamaniee nimekoma kabisaaa sina hamu ya kuchumbia tena labda miaka ijayo.
 
Ila mtoa mada mbona unaonesha haraka sana kwenye kwenda kujitambulisha kwanini usikae na binti mkafahamiana huku ukimsoma taratibu hadi pale utakapojiridhisha ndo uombe kutambulishwa nyumbani.
Kuomba kwenda kutambulishwa si chini ya miezi 3, kwann na yeye awe na haraka ya kyomba pesa au matumizi.
 
Niliamini kujitambulisha na kutoa mahari ni kumuwekea pingu asifanye yake tena lakini sasa duh timing ndio wanacheza nao. Kutanguliza makabila sio kwa kuyachambua makabila bali ni kumtambulisha mtu binafsi yeye kama yeye alichokifanya
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom