Nimekosea Wapi?

duh,,,, kuna familia ziko kama wanyamya.......wajua nguruwe kamwe hawezi mpanda dadake au hata mama..........hiki kizazi kigumu sana.....sijui heshima imehamia wapi.....anyway ndio utamaduni wenu...dumisha....
 
duh,,,, kuna familia ziko kama wanyamya.......wajua nguruwe kamwe hawezi mpanda dadake au hata mama..........hiki kizazi kigumu sana.....sijui heshima imehamia wapi.....anyway ndio utamaduni wenu...dumisha....
Kwa kabila na utamaduni wetu its okay wala sio tatizo..
 
Vineno neno ni sehem ya maisha, sasa kuliko aolewe na ndugu wa familia si bora shemeji? Mpe uhuru ajihukum mwenyewe
 
Pole kwa changamoto za maisha na hongera kwa kuonesha msimamo wao bila kuficha ...lakini hiyo ndio namna ya kukua.
Katika maisha yetu ya kila siku, huwa tunakabiliwa na changamoto, tunazikabili, tunazitatua, tunakuwa wazoefu wa maisha na hatimaye tunajenga uwezo zaidi wa kupambana na changamoto zingine kwa siku zijazo.

Ningekuwa kwenye nafasi yako, ningefanya kama wewe, tena ningefanya zaidi.... ningelaani na kukemea kwa nguvu zangu zote. Nisingekubaliana kabisa na wazo hilo la shemeji na mdogo wangu kufunga ndoa. Simamia kile unachokiamini na kipiganie kwa nguvu zako mpaka mwisho, kuna siku watakuelewa hasa mdogo wako. Anaweza asikuelewe leo lakini kuna siku moja atakuja kukushukuru kwa msimamo wako huo. Usifanye mambo au usiache mambo yaharibike kwa sababu unataka kuwafurahisha wengine.. waache wakasirike kuna siku watakuelewa. Kumbuka wewe umepewa dhamana ya kuwa 'Mlezi Mama', yaani wewe ni zaidi ya dada, hivyo una jukumu la kupambana na kulinda maadili na maslahi ya mdogo wako.

Unakumbuka tulipokuwa wadogo kuna mambo mengi tulitamani kuyafanya tukiamini yangetupa furaha sana lakini wazazi wetu walituzuia na tulikasirika sana, na hata wakati mwingine tuliwachukia, lakini baadaye tulikuja kuwaelewa na kuwashukuru kwa maamuzi yao ambayo kwa wakati huo tuliyaona mabaya. Kwasababu wao walisimamia kwenye ukweli. Wewe umesimama kwenye ukweli, endelea kusimama hapohapo hata kama unapingwa na kuchukiwa na watu wako wa karibu. Inapofika mahali unatetea 'damu' yako, usimumunye maneno hatakama 'hubby' wako na shemeji hawaoneshi furaha, achana nao wataizoea hali lakini wewe endelea kusimamia kile unachoamini.

Hii ni hoja nzito na tete, inahitaji mjadala wa hoja na sio kutishana wala kununiana miongoni mwa wanafamilia, kama kweli wana nia ya dhati kwa hicho wanachotaka kufanya waambie waelete hoja yao mezani, muijadili kwa hoja. Sio kwa kutishana kwamba eti, 'unamuharibia mdogo wako', hiyo sio hoja, hata mtu anapoamua 'kutoonesha furaha yake kwako' ni aina ya udhaifu, kwani kama ana hoja ya kweli anapaswa aiweke mezani. Waneleta na kufanya yote hayo ili wewe ushindwe hoja yako, ili wao waendelee.

Hata kama huko mbeleni watafanya ujanjaujanja na labda wakafanikiwa nia yao ovu, ni muhimu sana wewe uoneshe msimamo wako sasa kwamba hukubaliani na hilo, ili hata yakitokea ya kutokea huko mbeleni utabaki na heshima kwamba msimamo wako haukutetereka.
 
Ni jambo zuri unalofanya kumuonya mdogo wako!
Kiuhalisia sio jambo nzuri wote muolewe sehemu moja!

Ila wasi wasi unajua mpaka inafika kupropose ishu ya kuoana kunakuwa Kuna mengi sana ambayo yanakuwa yakiendelea behind the scene baina ya hao wawili!!
Sasa sijui kama walishafika mbali kwenye mahusiano yao unaweza kuwazuia!

anyway Mungu akusaidie ufanikiwe kumshawishi huyo mdogo wako
 
Ushampa ushauri unamuacha aamue mwenyewe sasa. Ni rahisi zaidi kumzuia mtu kwamba usito.mbwe/ Kuto.mba fulani kwasababu hii ama ile- lakini ni vigumu zaidi kumzuia mtu asiolewe / kuoa mtu fulani( kumbuka huenda hayo umeyafahamu baada ya wao wahusika kuwa ktk mahusiano kitambo tu pasi na ww kujua)
 
Baba Ni Mu Oman tabia zake niza Kiarabu kupitiliza,mkuu hakuna kitu hawa watu utawaeleza wakuelewe zaidi yakutumia force,kitu najivunia au kinachonisaidia jina langu nimepewa jina na Bibi mzaa baba na Dad humwambiii kitu kwa mamake
sasa mimi nikisema kitu hua ananisikiliza sana na najua ananipenda,na anajua kua nikiongea kitu hua mara nyingi sana nampa sababu,na kama kwenye hili yeye pia amesema sawa wewe ndio unamlea na ndio unajua nini kizuri kwake, kuna siku tuliwapeleka watoto hospital wa bro wana pumu balaa hakuna mwenye afadhali dr akasema sio vizuri kuoana familia moja,duu dr alichambwaaa mpaka nikaona aibu..
 
Naheshimu maamuzi yake ila ntajitahidi nimshawishi manake sio sawa...
 
Toa uongo wako hapa kanda ya ziwa kabila gani wanaoana kama wanyama kindugu ndugu hivyo usituaingizie mkuu.
 
Mmmh kwa mwanamke atakuwa ameenda sana umri aisee!
au kawaida kwa jamii yenu?
Kuolewa hakuna haraka mda ukifika ataolewa tuu inshallah muhimu asome ajue future yake anaipangaje kujisaidia ki maisha,wanaume wapo na wanawake wapo asome kwanza..
 
Toa uongo wako hapa kanda ya ziwa kabila gani wanaoana kama wanyama kindugu ndugu hivyo usituaingizie mkuu.
Sijasema uongo na siwezi kuwasingizia!
Nimeishi na wakurya mda mrefu na Shemeji zangu kabisa!!
najua nini nasema na nina uhakika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…