Nimekosea Wapi?

Nimekosea Wapi?

NIMPENDENANI

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2014
Posts
6,114
Reaction score
5,397
Hali zenu Waungwana,

Naomba niende moja kwa moja kwenye kile kinachoniumiza nafsi yangu..
Nna mdogo wangu she is 27, anasoma South Africa na nna shemeji amemaliza
kusoma anafanya kazi U.S.A, ndoto ya shemeji yangu huyo ilikuanikuoa mdogo
wangu au ndugu yoyote sababu anasema amevutiwa na tunavyo ishi familia yetu.
sikumchukulia serious na ukizingatia familia yetu hua sana wanaoana mtoto wa shangazi
kwa mjomba,mtoto wa mama mkubwa kwa mama mdogo,ila mimi na bro wangu hatuku
taka hayo mambo na familia kwanza walikataa ila baadae wakakubali..

Sasa shemeji yuko tayari kuoa na anataka kumuoa mdogo wangu wa mwisho mimi sijapenda why sote tuolewe kwenye same family? na kwa tabia ya familia yangu hawa wanangu usishangae tena wakaja kuowana na watoto wa mdogo wangu ikawa baba zao ndugu mama zao ndugu nikifikiria hapo hua nachoka,

Ila nimewaelezea reason zangu walonielewa ni wachache,na kuna wengine wamefikia kusema kua simtakii mema mdogo wangu wakati mimi ndio nimemlea mpaka sasaivi na she is a Daughter to me,nampenda sanaaa na ananisikiliza, hapa nyumbani kwangu hubby hana ile furaha kama ya mwanzo sababu nimesema sio sawa bro wake kumuoa mdogo wangu,shemeji nae hana ile bashasha tangu niseme hivyo anaona kama vile nimekua mchawi wake,

Nimemweleza mdogo wangu khasa kwa nini staki ila nimemwambia kua furaha yake ndio
yangu alichosema ni kua sis kama unadhani its not okay niko na wewe kwenye hili,
ila naona kama atahisi najali nafsi yangu au sitaki aolewe,ivi nikisema asiolewe na shemeji yangu ntakua nimekosea? hakuna kipindi kigumu kwangu kama hiki wakati wa maamuzi kama haya ndio hua nalia sana namkumbuka Mama,angekuwepo lingekua jambo jepesi sanaa manake yupo mshauri,

Sasa hivi kuna wakati nafanya maamuzi sina wakumwambia zaidi ya kumuomba mungu aniongoze.

Haya naomba mchango wenu wa mawazo Waungwana..
 
POLE MKUU KWANI YY ANASHINDWA KUJITAFTIA MUME WA MBALI UKIACHANA NA HUYO SHEMEJI YAKO?
 
Kisa kigumu hiki mungu akuongoze kama ni mila au tamaduni zenu kuoana kwa udugu huo usizuie isipokuwa kwa sababu nyinginezo
 
Sasa shemeji yako akimuoa mdogo wako kuna ubaya gani? Acha kucomplicate mambo! Na huyo mdogo wako lazima akuone una roho mbaya.

Sasa hao watoto wenu wataoana vipi wakati ni ndugu kabisa! Acha mdogo wako aolewe au unaona huyo shemeji yako ana hela kuliko mume wako ndo maana unaona mdogo wako atakupita kimaendeleo
 
Usikute jamaa alishamgegeda tayari mdogo wako afu wewe unaleta misimamo.Anyway Mmenishangaza sana familia yenu mnavyogegedana hovyo hovyo,yaani mimi na akili zangu hizi nioe mtoto wa mjomba,Shangazi au Mama mkubwa kweliii.

Kwa upande wangu sioni tatizo nyie kuolewa familia moja kwa sababu hakuna undugu kihivyo na sidhani kama watoto wenu watakuja kuoana labda nyinyi ndo mtake.

Tatizo langu ni kwa nini muoane mtoto wa mjomba au Shangazi isiwe tatizo ila kuolewa na ndugu wa mmeo iwe tatizo.U can't be serious
 
Muachie mhusika mwenyewe afanye maamuzi umekosea kufanya maamuzi kwa jambo ambalo si lako. Wewe ungesubiri kumshauri mdogo wako (kama angekuja kuuomba). Nahofia baadae mdogo wako atakuja kukulaumu kama maisha yake ya kimahusiano yatamuendea ndivyo sivyo huko kwingine atakapoenda
 
POLE MKUU KWANI YY ANASHINDWA KUJITAFTIA MUME WA MBALI UKIACHANA NA HUYO SHEMEJI YAKO?
Amesema mimi nafasi yangu kwake ni sawa na mama,sasa nnavyoona mimi yeye hatopinga,ila ndani ya moyo wangu nahisi kama anafanya kwakunifurahisha mimi ila niamini mkuu sina jengine zaidi ya hii issue yakuzaa watoto mama ndugu na baba ndugu,na wakati huo sijui kama ntakua hai au hata nikiwa hai kama ntakua na sauti ya kukemea jambo likasikilizwa kama sasa ivi..
 
Muachie mhusika mwenyewe afanye maamuzi umekosea kufanya maamuzi kwa jambo ambalo si lako. Wewe ungesubiri kumshauri mdogo wako (kama angekuja kuuomba). Nahofia baadae mdogo wako atakuja kukulaumu kama maisha yake ya kimahusiano yatamuendea ndivyo sivyo huko kwingine atakapoenda
Furaha yake ndio jambo la kwanza kwenye maisha yangu,ila sikubaliani na hii mambo yakuoana familia moja,mwisho wa siku mnazaa ma zezeta,ugomvi wa familia nimeyaona mengi na ndio mana staki na yeye yamkute..
 
Kumbe ni tabia ya familia yenu basi muache mdogo wako akajipatie utamu kwa shemeji yako mbona wewe unapata utamu kwa shemeji yake.
Sidhani kama ni sawa nna sababu nyingi sana za kukata,aolewe na mtu mwengine ila sio shemeji yangu hatuwezi kuolewa na familia moja..
 
Sasa shemeji yako akimuoa mdogo wako kuna ubaya gani? Acha kucomplicate mambo! Na huyo mdogo wako lazima akuone una roho mbaya.

Sasa hao watoto wenu wataoana vipi wakati ni ndugu kabisa! Acha mdogo wako aolewe au unaona huyo shemeji yako ana hela kuliko mume wako ndo maana unaona mdogo wako atakupita kimaendeleo

Mkuu naomba usome sababu za mimi kukataa,hakuna mtu anamuonea mdogo wake choyo,huyu kwangu sio ndugu ni mwanangu,mama alipo fariki alikua mdogo sana nimemlea na mimi ndio namshomesha,staki aolewe sababu family yetu
hua tunaowana mtoto wa baba mkubwa kwa baba mdogo shangazi kwa mjomba, mtoto wa mama mkumbwa na mtoto wa mama mdogo,sasa fikiria mtoto wangu mimi akiolewa na mtoto wa sister wangu mama zao ndugu na baba zao pia wanakua ndugu sasa hapo hamjazaa watoto wenye akili za nyani au maradhi ya kurithi?
Kimaendelea Alhamdulillah tuko vizuri,ila hata akinipita ni fahari yangu mdogo wangu kuolewa na mwenyenazo ila sio kwa style itakayo m cost furaha yake..
 
Back
Top Bottom