Baada ya kufanyiwa kazi
fulani na kukamilika nilipatiwa namba na wafanyakazi hao ili nimtumie
bosi wao malipo kwa njia ya M-pesa, kwa bahati mbali walinipatia namba
ya mtu mwingine kwa makosa na hivyo fedha kumuendea mtu huyo. Baada ya
kuwasiliana na Vodacom huduma kwa wateja walinijulisha kuwa huyo
niliyemtumia hizo fedha ameshazitoa toka kwa wakala.
Baada ya mtu niliyemtumia fedha kutokuwa hewani kwa muda mrefu hatimaye
aliwasha simu na nikaweza kuongea naye, alikubali kupokea fedha hizo na
kuzichukua lakini aliniahidi kunirudishia. Pamoja na kumtaka achukue
kiasi cha sh. elfu kumi(Tsh 10,000/- kutoka ktk fedha hizo kwa usumbufu
alioupata, hata hivyo amekuwa akinibabaisha na kuzima simu yake muda
mwingi na hivyo nimeona ananikwepa, Hivi kuna namna nyingine yoyote ya
kuzipata fedha hizi au ndio basi tena! naomba mawazo yenu.
Huu usajili wa namba kwenye mambo kama haya sijui kwa nini haujatusaidia!!kuna rafik yangu alitumiwa pesa kwa mpesa kimakosa kwenye simu yake million 1 jamaa alichofanya kutoa pesa fasta na akaichana line,sasa hiv ana line nyingine mpya yuko kwa mtaa
Huu usajili wa namba kwenye mambo kama haya sijui kwa nini haujatusaidia!!
Kwa nini wasidhibiti mpaka kwenye matumizi ya line zingine? Hivi huwa hawawezi kujua mpaka simu inayotumia line fulani? Kwa mfano Maulid kasajili line kwa kutumia kimchina chake, hawawezi kurekodi hiyo line na hicho kimchina ili kama Maulid ataweka line nyingine kwenye hicho kimchina chake ajulikane mara moja?
Tutaendelea kulizwa tu kila uchao!!

Unakoseaje na jina linatokea pale?inabidi tuwe kamini na pesa wana JF wenzangu;maana hadi upate line na ku report,unakuta alietumiwa na njaa za sikuhizi anakuwa ameshaitoa inaanza lawama sasa,tujaribu kuwa makini sana,maana jina linatokea kabla kuthibitisha na pesa kutoka kwa mtumaji!nakubali kukosea kupo ila tujitahidi kuwa makini kwa confirm jina kwanza maana linatokea pale na una muda kuhakikisha unaemtumia!
mi nimewahi kosea ila bahati nzuri nilipoenda mpesa WALIFANIKIWA kunirudishia. ila hii huduma ya simu pesa niliona haiko salama kabisa.inatakiwa watafute utaratibu wa kuwashitaki watu wanaotoa pesa zisizo zao. pia hawa mawakala wa simu pesa wengi hawana elimu, wanafikiri utaratibu wa vitambulisho ni mbwembwe kumbe una maana yake. pole sana ndugu kama hujapata hela yako
Mkuu,tatizo la mpesa,hawakuletei uthibitisho wa jina la mtu unayemtumia,tofauti na tigo pesa ambao wanakupa uthibitisho kwa jina la mtu unayemtumia,jina ni rahisi zaidi kwa watu walio wengi kuliko namba pekee,voda warekebishe hili.
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums