Nimekosa title nzuri ya huu uzi, ila we soma tu.

Nimekosa title nzuri ya huu uzi, ila we soma tu.

Joeli

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2011
Posts
4,941
Reaction score
3,417
Leo nimewaza na nikaona tujadili umuhimu wa kujitunza sisi kama vijana.

Maswali mengi tu nimejiuliza kichwani, swali kubwa ni kwani sisi vijana hatuwezi kujitunza?

Dini zote zinasisitiza watu tusijiingize katika matendo ya ngono kabla ya ndoa, na hata tukioa/kuolewa tusiwe na zaidi ya mtu mmoja(isipokuwa waislamu)

Swali langu:
Je, ni vigumu kwa sisi vijana kuishi maisha bila ngono kabla ya ndoa? Kwani kuna chochote tunapungukiwa tusipofanya tendo hilo? tunapata faida gani tunapofanya tendo hilo? kwa nini tunajiingiza katika tendo hili then?

Huwa tunafikiria kuhusu mambo kama mimba zisizotarajiwa, maradhi ya zinaa na UKIMWI?

Nakosa majibu kabisaaa.

ULEVI
Vijana wengi tumejitumbukiza katika ulevi wa pombe, mimi sijui kuna nini kwenye pombe na ulevi mwingine wowote. Kuna mdau alinipa faida za pombe eti zinakusaidia kujuana na watu unapata madili, nikajiuliza kwani madili hayaji mpaka kwenye ulevi tu? Unapokuwa unatumia ulevi utataka na kutaka na kutaka, maana yake utapoteza pesa amabazo zinngekusaidia kufanya mambo ya maendeleo.

MAVAZI
Kuvaa vinguo vifupi na vya kubana sana kuonesha maungo KWA wadada na kuvaa misuruali iliyochini ya kiuno tunafaidika na nini? kwani ukivaa gauni refu au sketi ndefu itakukosesha nini?
uwa naona aibu hata kugeuka pembeni nnapoona mdada kavaa kinguo cha kubana na vijana wanshangilia....

mbona maadili yanaporomoka kupita kiasi? mfano: ukisoma thread nyingi za kuomba ushauri. watu wanaomba ushauri wafanye nini baada ya kugegedana na shemeji yake n.k

nna mambo mengi ambayo nayawaza ila natumia simu kuandika,

Nawaomba vijana wenzangu tumrudie Mungu, tuwe wasafi wa mwili na akili kwa maana miili yetu ni mahekalu matakatifu, tusiyachafue kwa vilevi, sigara wala uzinzi.

mpaka wakati mwingine, nawatakia siku njema,
nawapenda sana.
mimi C6
 
C6 asante kwa hayo ila kama unampigia mbuzi gitaa kwa vijana kwa sasa maana usopofanya hayo utaonekana wewe ni wa zamani na wakuja ambaye hauendi na wakati na bado uko nyuma ya mtandao. Muulize kijana mdogo maswali madogo tuu ya maisha yake anawez akukupa historia ambayo hata wewe hujawahi ipitia na anaweza kukuambia mambo machafu ambayo hujawahi yafanya pamoja na umri wako
 
Last edited by a moderator:
Mkuu C6 kidini wanasema vijana ndio wanashambuliwa sana na shetani kwa kuwekewa vishawishi vingi kama muziki, mavazi, ngono, ulevi nk. kwa kuwa wao ndio wana nguvu ya kushindana naye kama wataachwa na huyo shetani rejea biblia. Kisayansi wanasema vijana wapo katika muda wa kujifunza kwa hiyo ni wepesi mno wa kujifunza vitu mbali ikiwemo kuiga kutokana na makundi yaliyo karibu nao, vichochezi vya mwili kama homon pia ni sababu.
 
Mkuu C6 lazma ujue kwamb vyote ulivyotaja as vnaharib vjana,jua kwamb walioleta target yao ilikuwa kwako wewe kijana!!!!

Pia kijana asiyejielewa n rahc xana kuingia kweny mob psych,ambapo atafanya hayo pengne kwa kutaka afanane na wenzake au hakupata moral ethics ya uhakika hasa alipokuwa age btn 0-6,hivyo kuwa rahc kwake kvurutwa na immoral ethics!.

Madhara ya huyu kijana anakuja kuyapitia as yeye pia kutokana na yeye kuwa hakupata malez sathk naye ,kutokana natabia zake mbovu anaweza pata mtoto ambapo s rahc kupata moral ethcs.

Nadhan hapo mku C6 unapta chen kubwa sana yenye imral ethcs.

But what to do,kama kijana lazma ujue why u enter in a such thng?,what ua expectatio?,how make ua dream alive through pombe,wiz,umalaya?,nadhan itatsaidia xana kama kijana.

Ndio maana mkuu C6 katka thread zang nimekuwa nikiongelea sana kujiuliza maswal meng sana kabla hujaingia kwenye kila aspect of ua lyf,nadhan niishie kwa hapa!!!!
 
Last edited by a moderator:
Kila unavyokatazwa kitu ndio unataka kufanya
Kama ulikuwa boding, hukuwa unaiba mara mahindi mara mihogo??

Sasa hivi unavitamani?? Sababu una access navyo
esho tukiruhusiwa kufanya ngono tangu tuna miaka 2, wala hatutatamani tena
 
Miaka 2? hiyo ni ngono au kufanya matusi?
 
Hayo unayoyashangaa ni matokeo ya athari za kisaikologjia na kiroho kutokana na malezi ya kimahusiano na kimaadili ya wazazi kwa kutokujua au kwa kujua bilia kujali athari zake. Kisayansi na hata kiroho malezi ya tabia ambazo mzazi angependa mtoto wake awenazo hutegemea:

  • kwanza malezi ya kimahusiano kati ya wazazi na kati ya wazazi na watoto; nikimaanisha kuwa wazazi kuwaonyesha watoto wao upendo wa kina, kuwajali na kuwahakikishia usalama wao, pia kuonyesha jinsi wanavyojisikia vibaya mtoto anapokosea au kuonyesha tabia isiyo njema na kupongeza anapofanya jambo linaloonyesha tabia nzuri.
  • Pili Ukaribu wazazi na watoto; katika nafsi ya binadamu huwa kunakuwa na nafasi wazi ya mtu wa jinsia tofauti. Hali hiyo isipofuatiliwa vizuri na wazazi wakati wa malezi ya mtoto tangu anajifungua mama hadi miaka 5 huwa matokeo ya tabia mbaya ukubwani yaani kuanzia ujanani. Kwa hiyo kwa mtoto wa kiume nafasi wazi kwake katika nafsi hujazwa na upendo na ukaribu wa mama ambao ukubwani hujazwa kwa kiwango cha juu sana na mke. Vinginevyo mtoto huyo asipotendewa hayo madhara yake ni kuja kutafuta upendo kwa jitihada za juu na kwa nguvu zote akifikia kubalehe huku akichochewa na mazingira yatakayokuwepo; hali kadhalika kwa mtoto wa kike baba ndiye anayetakiwa kuwa karibu zaidi kwa upendo, kumjali, kumwonya na hata zawadi. Hivyo ni muhimu kuwa na muda mwingi wa kuwa karibu na watoto kama tunataka kupata vijana wazuri baadaye.
  • Mwisho kwa siku ya leo; Malezi ya mama wakati wa uchanga wa mtoto yaani mwaka 0-2: hapa ninamaanisha kuwa matumizi mbalimbali ya viungo vya mtoto humpa mtoto burudiko fulani. Hivyo kama atakosa uhuru wa kuvitumia wakati huo wa utoto ukubwani hutumika vibaya, kwa mfano mtoto mchanga hutumia mdomo kunyonya na hupenda hivyo na husikia raha akinyimwa kutumia hivyo ukubwani lazima atakuwa msemaji sana nanirahisi kuwa mbeya au msengenyaji, pia kizazi chake hupenda na kujisikia raha anapokojoa; kama mtoto atakuwa akisumbuliwa kwa kushituliwa kila anapokojoa mtoto huyo ukubwani atatumia vibaya viungo hivya kwa umalaya na kwa viungo vingine vivyo hivyo.

Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha ha awapo mzee...........

Ahsanteni kwa leo kwa ufupi niishie hapo.

By Mchungaji
 
Nimependa uzi. Ni muhimu kujikumbusha na kukumbushana. Nadhani vijana wengi wanapelekwa na influence ya rafiki zao, wanataka kuonekana wajanja, hawataki kuonekana wamepitwa na mambo ya mujini. Sometimes people know kabisa kua wanacho kifanya sio sawa but they still do it for fear of being rejected by the group or kwa kuogopa kuonekana mtu wa aina fulani.
This goes back to kujiamini na kua na imani na kile unacho amini kama kitu kilicho sahihi. Lazima tuwafunze watoto wetu kujiamini na kusimamia values na principles, to evaluate their actions based on that instead of what people around them want them to be.
 
Vitoto vinatoka tumboni vinajua ngono maana mama yake katoto alikuwa anawaza ngono muda wote akiwa na mimba, unategemea nini katika mazingira hayo? Mtoto anazaliwa anakua akimwona mama anavaa kaza ------ na onyesha paja ilhali baba mlevi, unategemea nini hapo? Acheni twende hivyo hivyo maana mmeruhusu wazungu wacheze na akili zetu kupitia matamthilia ya hovyo hovyo.
 
Leo nimewaza na nikaona tujadili umuhimu wa kujitunza sisi kama vijana.

Maswali mengi tu nimejiuliza kichwani, swali kubwa ni kwani sisi vijana hatuwezi kujitunza?

Dini zote zinasisitiza watu tusijiingize katika matendo ya ngono kabla ya ndoa, na hata tukioa/kuolewa tusiwe na zaidi ya mtu mmoja(isipokuwa waislamu)

Swali langu:
Je, ni vigumu kwa sisi vijana kuishi maisha bila ngono kabla ya ndoa? Kwani kuna chochote tunapungukiwa tusipofanya tendo hilo? tunapata faida gani tunapofanya tendo hilo? kwa nini tunajiingiza katika tendo hili then?

Huwa tunafikiria kuhusu mambo kama mimba zisizotarajiwa, maradhi ya zinaa na UKIMWI?

Nakosa majibu kabisaaa.

ULEVI
Vijana wengi tumejitumbukiza katika ulevi wa pombe, mimi sijui kuna nini kwenye pombe na ulevi mwingine wowote. Kuna mdau alinipa faida za pombe eti zinakusaidia kujuana na watu unapata madili, nikajiuliza kwani madili hayaji mpaka kwenye ulevi tu? Unapokuwa unatumia ulevi utataka na kutaka na kutaka, maana yake utapoteza pesa amabazo zinngekusaidia kufanya mambo ya maendeleo.

MAVAZI
Kuvaa vinguo vifupi na vya kubana sana kuonesha maungo KWA wadada na kuvaa misuruali iliyochini ya kiuno tunafaidika na nini? kwani ukivaa gauni refu au sketi ndefu itakukosesha nini?
uwa naona aibu hata kugeuka pembeni nnapoona mdada kavaa kinguo cha kubana na vijana wanshangilia....

mbona maadili yanaporomoka kupita kiasi? mfano: ukisoma thread nyingi za kuomba ushauri. watu wanaomba ushauri wafanye nini baada ya kugegedana na shemeji yake n.k

nna mambo mengi ambayo nayawaza ila natumia simu kuandika,

Nawaomba vijana wenzangu tumrudie Mungu, tuwe wasafi wa mwili na akili kwa maana miili yetu ni mahekalu matakatifu, tusiyachafue kwa vilevi, sigara wala uzinzi.

mpaka wakati mwingine, nawatakia siku njema,
nawapenda sana.
mimi C6

Kwanza kabisa nikupongeze kwa jinsi kwa thread nzuri na lugha nzuri pia, nasema lugha nzuri katika mkutadha kwamba pamoja na kuwa ni matukio yanayokusikitisha kwa pande zote mbili za kike na kiume na wewe sio mmoja wao lakini hakika umeendelea kutumia neno sisi vijana, hivyo hukujiondoa ama kujitenga na wenzako.

Hakika hili ni jambo la kusikitisha sana kwa sasa hasa ukianzia kwa jambo ambalo mimi binafsi naita dogo kama la mavazi, hakika sisi tulio wazazi tu jambo la kujibu hapa. Nasema tuna jambo la kujibu kwa sababu kuna watoto wadogo sana kwa sasa ambao unakuta wamevaa mavazi ya ovyo ambao ukiangalia hakika ni watoto ambao bado wako chini ya malezi ya sisi wazazi jambo ambalo linathibitsha kuwa sisi wazazi tumehusika moja kwa moja katika kugharimikia mavazi hayo. Na mtoto wa hivyo hata akikua ataendelea kujinunulia mavazi ya ovyo kama alivyozoezwa na wazazi wake tangu akiwa mtoto mdogo. (Mlee mtoto katika njia impasayo naye akikua hataiacha hata mzee...)

Wengine wamekuwa wakiiga mambo ya mavazi kwa wengine ukubwani, hii inaonesha pia hawa wanaoiga hawana misingi imara ya malezi toka kwa wazazi wao, maana kama wangelikuwa nayo wasingeliiga mabaya, bado mchango wa wazazi katika malezi sahihi unaguswa hapo pia.

Swala la ulevi nao na malezi mabaya na mambo ya kuiga, hivyo kila mtu kwa nafasi yake atimize wajibu wake ili kunusuru hiyo hali.
Nimalizie tena kukupongeza kwa thread nzuri, ni kweli mwili wa mwanadamu ni hekalu la bwana, tusilichafue kwa mambo ya ovyo kama uzinzi nk. Nimetaja uzinzi nk kwa sababu kuu moja maandiko yanasema dhambi zote kama uongo, kuabudu miungu nk hufanyika nje ya hekalu la Bwana (mwili) lakini uzinzi hufanyika na kulichafua hekalu la Bwana.

Na mwisho kabisa hakuna madhara yoyote kwa kijana kuishi pasipo kufanya ngono, hivyo inawezekana kabisa kusubiri hadi wakati wa ndoa.
 
it-begins-with-you-logo.jpg

Wana MMU wooooooote!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom