Mdakuzi mkuu
JF-Expert Member
- Dec 27, 2016
- 212
- 719
Kama heading inavyojieleza, kuazimisha gari n risk kubwa sana.
Wili iliyopita, kuna rafiki yangu wa karibu sana aliomba gari yangu (kwa madai yake) aende kuwaona wazazi wake Wilaya ya jirani,umbali wa kilomita 80. Ni safari ya kwenda na kurudi kwa siku moja. Nilimpa kwa makubali hayo, aende na kurudi siku hiyohiyo.
Baadae jioni nikapigiwa simu na polisi akinieleza kwamba, jamaa yangu alifumaniwa na mke wa mtu guest house.Mwenye mke akatafuta vijana wakaanza kupiga gari kwanza na kumtandika yeye.
Gari ikavunjwa vioo vyote, taa za mbele, wakaiba sub woofer, kadi ya gari na vitu vingine vilivyokuwamo.
Baada ya kichapo hicho na kuharibiwa gari, msamalia mwema akamuona na kumpeleka polisi ili akapate PF 3 kwa ajili ya matibabu.Polisi baada ya kimhoji sana, akaeleza tu ukweli kwamba alifumaniwa akabondwa.
Mpaka sasa gari ipo polisi lakini haifai.Mm napanda daladala kwenda kazini.
"Subaru Forester"
Mbaya zaidi gari ya mkopo.Mke wangu sijamweleza mkasa mzima.
Full head ache.
Nimekoma kuazimisha gari, kama nikija kununua lingine.