Nimekatwa laki 2 kwa kutumia ATM ya DTB

Nimekatwa laki 2 kwa kutumia ATM ya DTB

mandwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2013
Posts
1,502
Reaction score
372
Habari,

Naomba mnisaidie kwa hili mimi natumia bank ya CRDB kupata mshahara wangu mwezi wa 6 nilitumia ATM ya DTB kuchukua fedha zangu kwani ATM card yangu ya CRDB ni Visa cha kunishangaza nimekuta nimekatwa laki 2 kwenye mshahara wangu wa mwezi wa 7 nimjaribu kuuliza bank ya CRDB wamesema nimekatwa kutokana na kutumia huduma ya Visa kutoka DTB mwezi uliyopita.

Naomba mnisaidie je kutumia huduma ya Visa DTB inagharimu kiasi cha laki2?
 
Hapana mkuu, haiwezi fika laki mbili...kumbuka vizuri hiyo pesa uliitoa na ukaitumia maybe. Lak mbili noooo pls, na huyo bank officer alokwambia ni mshamba na hajui banking.
 
Habari,naomba mnisaidie kwa hili mimi natumia bank ya CRDB kupata mshahara wangu mwezi wa 6 nilitumia atm ya Dtb kuchukua fedha zangu kwani atm card yangu ya crdb ni Visa cha kunishangaza nimekuta nimekatwa laki2 kwenye mshahara wangu wa mwezi wa 7 nimjaribu kuuliza bank ya crbd wamesema nimekatwa kutokana na kutumia huduma ya Visa kutoka DTB mwezi uliyopita,naomba mnisaidie je kutumia huduma ya Visa DTB inagharimu kiasi cha lAki2?

yan hata elfu kumi haifiki ... mm mara nying natmia card yangu kwa atm zeny mastercad lkn sijawah kukatwa hata elfu tano kama charges
 
Hujasema umetoa shilingi ngapi. Kama wanakata fee kwa kutumia percent kadhaa ya hela uliotoa inaweza kufika.

Mfano kama wanakata 10% basi ukitoa 2,000,000 fee yake ni hio 200,000 nl
 
Mkuu pesa niliyotoa si zaidi ya laki2

Mfano kama wanakata 10% basi ukitoa 2,000,000 fee yake ni hio 200,000 nl

Mkuu pesa niliyotoa si zaidi ya lAki2 je hii ni haki?
 
Habari,naomba mnisaidie kwa hili mimi natumia bank ya CRDB kupata mshahara wangu mwezi wa 6 nilitumia atm ya Dtb kuchukua fedha zangu kwani atm card yangu ya crdb ni Visa cha kunishangaza nimekuta nimekatwa laki2 kwenye mshahara wangu wa mwezi wa 7 nimjaribu kuuliza bank ya crbd wamesema nimekatwa kutokana na kutumia huduma ya Visa kutoka DTB mwezi uliyopita,naomba mnisaidie je kutumia huduma ya Visa DTB inagharimu kiasi cha lAki2?

Arghhhh😡😡😡 kwa wasiojua CRDB wezii wa kuogopwa kabisa na kama jambo hili lipo ndani ya uwezo wako fuatilia hadi mwisho ukifanikiwa tupa mbali kabisa hiyo kadi yao.Hizi ATM zao ndo mkebe hasa wa kuibia watu.Yaani it's a Toolbox.😱
Ni hivi kuna mlima wa malalamishi juu ya gharama za huduma zao hasa makato kutoka kwa watumiaji wa mashine.Pili Visa card ni majanga kwa watumiaji ndani na nje ya nchi.Yaani bora wewe laki mbili,kuna wanaotumia nje ya nchi wao mpaka laki5 inapotea hivihivi :what::what:;mwanzo huanza kwa ubora lakini baadae huwa shida na mzigo kwa mtumiaji kitu kinachofanya niamini wakishagundua hii kadi inatumika nje basi ndo kilio kwako.

OK,1st kuna kitu chaitwa ledger balance.Hii kitu ukiangalia salio unakuta hela yako ipo kwenye ledger balance na available balance zero.Hapo ni bahati tu inaweza toka au ndo imepita hiyo.Na ukizubaa ndo imekula kwako kabisaa bora uwahi kuwabana.

2nd ni gharama za huduma.Crdb wana gharama nyingi na makato ya juu hata kwa huduma zipasazo kuwa nafuu au bure kabisa MF.kuangalia salio au kutoa gharama ni kubwa.Ndiyo hizo 700 za kutolea hela siyo ndogo.Kuna kichwa!

Tatu usije ukajiunga na sijui bank statements au programu nyingine,utalizwa mchana ndugu yangu.Utakuta michirizi ya makato ya ajabu tote chino ya mwamvuli wa hivi vi huduma vya nyongeza.

Nne,huduma kwa wateja ni mbovu.Hawa wana lugha ya kukejeli,dharau na maringo kwa wateja.Rafiki yangu kwenye kufuatilia suala la hela kutumwa na kutoonekana kwenye akaunti,aliambiwa yy ni mjanjamjanja na mwizi na kisha mzazi wake kutaka kutolewa na polisi baada ya kuweka bayana na kwa vielelezo kuwa pesa imetumwa lkn kwny akaunti haipo.

Tano: Overdraft
Kama hujui overdraft utaijua Crdb na kama bado hayajakukuta ipo siku utayafahamu.Hii service in kwa akaunti za biashara lkn wanaipenyeza hadi kwenye akaunti za akiba kwa wizi.Unatumia hela yako baadae unakuja kuambiwa umeover draft an in fact unadaiwa hicho kiasi ulicho overdraft.

Binafsi nimekuwa mteja kwa zaidi ya miaka 7 ila miaka mi4 ya mwisho nilikuwa nje kwa masomo na huko ndo nikapata kuwafahamu CRDB vizuri.Haya si yangu bali no mjumuisho wa malalamishi kutoka ndani na nje ya nchi na kwa kila watumiaji watatu niliokutana nao wawili wana haya malalamiko.
Tafakari Chukua Hatua.
 
Mkuu nifanyaje sasa j3 nataka niende kwenye branch yangu CRDB Holland niwaeleze je kutumia Atm ya Dtb kwa siku moja nikatwe laki2 kweli jamani mshahara wote wamechukua.Au nifanyeje jamani Wife hanielewi maana nadaiwa school fees
 
Me nakushauri nenda bank kaombe bank statement hata iwe mini statement itafaa, ukiipata angalia transactions zilizopita kwenye account yako, kama kuna changes zozote zilizopita kwenye account yako utaziona au kama ni withdraw ilifanyika pia utaiona. Ukifanikiwa kuiona hy transaction ya laki 2 then muone afisa wa bank hapo hapo crdb akufafanulie hy transaction. Nakuhakikishi hy pesa haiwez kuwa ni charge ya kutoa kupitia visa kwani charge haizidi elfu. 10 kwa pesa uliyosema umetoa.
 
Mkuu nifanyaje sasa j3 nataka niende kwenye branch yangu CRDB Holland niwaeleze je kutumia Atm ya Dtb kwa siku moja nikatwe laki2 kweli jamani mshahara wote wamechukua.Au nifanyeje jamani Wife hanielewi maana nadaiwa school fees

Kwa kawaida wanakata elfu NNE(Elfu 4) kwenye transaction za visa/master nje ya machine zao.Wahi kwenye tawi kama ulivyoshauriwa kisha omba statement yako.Angalia mlolongo wa makato yote then kama haipo hiyo laki mbili anza hapo..na kama ipo ulizia upewe charges zote zilizotozwa kutoka kwny akaunti yko.Nenda hata kwa meneja upewe maelezo ya kutosha.Ukiishia kaunta utaisikia ada bombani.Na next time usije rudia hiyo kitu mkuu.
 
nahisi ulijaribu kutoa pesa ikakataa mara ya kwanza na ulivyojaribu mara ta pili zikatoka... sasa kinachotokea ile mara ya kwanza iliyokataa kutoa pesa CRDB HUWA WANAKATA KAMA IMETOKA .. ishanitokea mara mbili.. ya kwanza wakaniibia (70 elfu) nikavumilia mara nyingine laki moja.. nikakomaa nao nikapewa claim form wakarudisha... (inatakiwa ukadai ndani ya siku 40)
 
Ukiamka nenda CRDB kuomba bank statement.Kama ni suspecious withdrawal ni kesi ya kawaida kabisa amabapo unatoa hela kama kuna tatizo la mtandao mashine ya ATM inasuspect kwamaba umetoa kumbe hujatoa.Imesetiwa hivi kwa sababu mteja anaweza kuitafuta bank lakini bank haiwezi kumtafuta mteja endapo mteja atatoa hela alafu mashine isirekodi.Sasa hapa itategemea na uaminifu wa Bank coz mimi nimefanya kazi NBC na fedha za suspecious withdrawal wateja walikuwa wnaridishiwa.Sina uhakika na uaminifu wa CRDB,bank statement ndo document ya kuanzia.Usikubali porojo za Bank officer kama humuelewi omba kuonana na meneja wa tawi husika.
 
Jamani asanteni nimerudishiwa pesa yangu baada ya kuvutana hapa na pale asanteni sana watoa huduma wa CRDB holland Branch baada ya kufatilia wakaona kuna makosa yamefanyika hatimaye pesa zimerudi jioni hii.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Braza hilo nitatizo tu la kawaida, binafsi nilishawahi kutoa hela NBC wakati natumia CRDB. Nilitoa laki moja lakini ikawa haijakatwa, pale huwa wanaihold ili baadae waikate kama system inasumbua... ilipokuja katwa nikakuta kuna difference ya laki2 na sio laki 1, nilipofuatilia vizuri iligundulika kumbe system bado ilikuwan imehold ile laki1. Kwa system ya visa inachukuaga muda kurudisha ila walinirefund... ni matatizo tu ya kimtandao ambayo ni kawaida.
 
Back
Top Bottom