Nimekataa kumpongeza Mrisho Gambo

Kamwe Lowasa hatawatoka wana CCM kwenye vinywa vyao.Bila kumtaja Lowasa kikao au mkutano hauwezi kumalizika salama.Ni kwa nini?Mbona yeye hana habari nanyi kabisa.Naamini ataendelea kuwatesa kwa muda mrefu sana.Ni muda tu tusubiri.
 


Hivi umesema hii picha inatufundisha nini vileee?
 
MRISHO MASHAKA GAMBO,Kumbe uhasibu Arusha inatoa viongozi????? au ilikuwa ya zamani?
 
nasikitika kuona mbunge mzima una akili kama ya mtoto wa chekechea.

Sasa wewe mwenyewe umeshasema humjui vizuri alafu unammwagia sifa kibao na kumwamini kabisa ukksema hatakuangusha.

Hii imekaaje sasa

Ukiona hivi, tambua mara moja kuwa hizo ni porojo na uongo tu wa kufurahisha jamvi!!

Ninachoweza kusema kuhusu Juliana Shonza ni kuwa, she is good but not the best in propaganda!!

Amesahau kuwa ni huyu huyu Mrisho Gambo ndiye aliyewatukana wanawake wote wasomi wa sampuli yake Juliana kuwa vidigrii (shahada) zao hizo wamezipata kwa kuvua vyupi vyao!!.

Sina hakika kesi ilishaje dhidi ya huyu bwana maana alishitakiwagwa kwa kauli yake hii!!

Maana na tafsiri ya hiyo ni kuwa, hata shahada ya ...........aliyonayo Juliana Shonza hakuipata kwa halali bali kwa kuvua ovyo nanihi yake!!

Je,Juliana Shonza ana maana ya kuwa UJASIRI na UJEURI na KUJIAMINI (KUTOKUOGOPA) alionao huyu ndugu yake ni huu wa kutumia lugha chafu dhidi ya watu anaowaongoza na viongozi wenzake?...Hii ndiyo sifa bora ya kiongozi?
 
amesema "ameambiwa" kuhusu Gambo so probably atakuwa amepewa maelezo na akina lizaboni
 
Usitishike na neno Ulokole kiongozi maana hawa ndio wanaongoza kwa matendo machafu bora hata mtu asiye na dini lkn akaamini tu Mungu yupo
 
Na cha ajabu vijana hao hao wanaosifiwa kulelewa vizuri ndo waliouza Mali za chama kule iringa teh teh teh! Chama hiki hakiishi mikosi
Kati ya chama chako na CCM KIPI kina mkosi?!CCM ndiyo dume lako upende usipende na uukileta fyoko kina uwezo wa kukufanya kitakavyo chagadema ww!
 
Sijaelewa hata nini huyu dada anataka kukiwakilisha kwenye bandiko lake
Kwamba UVCCM na CCM kwa hujumla ndiyo inayotakiwa kupongezwa kwani imefanikisha kupatika kijana Gambo. Hata hivyo kama kweli Tume ya maadili kama inafaile lake la tuhuma na huyo mwanasheria amemfungulia kesi, hapo nadhani hilo ni doa kwa UVCCM na CCM kwa ujumla.
 
Kwa Katiba iliyopo tupo sahihi kwa kila jambo.
Kujitosheleza haitoshi je knaheshimiwa? Ndo maana nimekwambia ukaidadavuzi mkuu ili ikibidi iendane na kasi yenu kasi ya matamko, kila siku as if matamko yanaendeshe serikali badala ya katiba kuendesha serikali na nchi kiujumla
 
Na iyo kesi haitokuja kwisha kama mapka leo ni miaka na hukumu yake bado inatafutwa!
 
Hakika,umenena kweli.CCM bado itaedelea kutoa viongozi mbalimbali wa nchi hii kwa karne nyingi zijazo...na hata kwa upande wa upinzani wataendelea kupata wagpmbea wa nafasi mbalimbali kuanzia mashinani hadi uraisi kutoka CCM...hili halina ubishi.

Kama CCM inajiamini mbona wanaiba kura? Wenye kujua viongozi mahiri ni wananchi na siyo CCM kujigamba yenyewe.
 
Hahahahah si kwa kujikomba huko lakin jitahidi anaweza kutenguliwa mwingine!!!!
 
Oneni majibu ya wana UKUTA! Eti haya wanayo jibu hapa ndio mawazo yao mbadala wa ccm.
Huo ni uono wako hafifu si kila anayekupinga ni mpinzani, kuna muda mwingine watanzania tuache unafiki wa kumng'ong'a mtu kisogo, akiwepo unamkubali akigeuza kichwa tu unaanza manung'uniko! Si kila anayechangia hapa ana interest na UKUTA jifunze kusema ukweli binafsi na sio ukweli wa chama
Nyie ndo kina Mkuu wa mkoa wa Rock city nyie
"Tutayafanyia kaz maagizo ya Rais hivyo hivyo yalivyo, hatutaongeza akili zetu" Aug.17,2016
 
Kati ya chama chako na CCM KIPI kina mkosi?!CCM ndiyo dume lako upende usipende na uukileta fyoko kina uwezo wa kukufanya kitakavyo chagadema ww!
Bahati mbaya umenielewa ndivyo sivyo! Aliyekwambia mimi Nina chama ni nani? Usikimbilie vitisho na kutukana jibu hoja hawajaiba? Kwaiyo tumuamini nani wewe au wale waliotangaza kuwa iringa kumeibiwa hahahaaa mimi sina chama ndugu yangu ni mbena kwa asili ya kabila langu naizungumzia iringa yangu sasa huko chagadema ndo wapi mkuu!?
 
Ni kweli Juliana Shonza, nakubaliana na wewe 100% CCM ni chama pekee cha kuzalisha viongozi bora nchini mwetu
Viongozi bora kwa kutumia vigezo au kipimo gani? Sio huyo RC wa Dar es Salaam aliyempiga mzee Warioba? Sio huyo mteule Rc wa Arusha aliyekuwa na kesi bwerere tume ya maadili ya umma ikiwemo ya kumtukana mwanasheria wa halmashauri kuwa ana digrii ya chupi? Mapungufu ya mamlaka ya uteuzi msiitumie kuhalalisha kuwa ndani ya CCM kunazalishwa viongozi bora. Na kwa uhakika, naomba hili ulichukue-kuna viongozi ndani ya CCM ambao wanatambulika kwa uadilifu wao, kama ndio wangekuwa na mamlaka ya uteuzi hao mnaoshangilia kuteuliwa kwao hata kwenye "reserve" wasingegusa! Endeleeni kushangilia staili hii ya uteuzi wa watu wasio na chembe hata ya maadili ila mjue CCM ndio inazidi kuizamisha nchi kwa habari ya maadili, muda utasema!
 
Huyu Binti nilifikiri matatzo yake yameisha kumbe bado..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…