Kipenzi Changu
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 58,001
- 134,195
Kwa miaka kadhaa nimekuwa nikisitasita kuandika wosia kuacha kidogo nilichonacho kwenye mikono salama.
Kwa wakati wote huu nimekuwa nikipata sababu za msingi na haja ya kuandika wosia.
Nimeishi katika migogoro kadhaa ya mirathi ama ya ndugu au jamaa na nimejionea mwenyewe umuhimu wa kuacha maandishi ukimilikisha watoto na mke na madeni.
Nimehuzunika sana hasa naposhuhudia mabinti wa kike wakidhurumiwa mali na ndugu wa marehemu. Inauma watoto waliokuwa wakiishi maisha mazuri shule nzuri wanapoanza kutangatanga baada ya baba kufariki.
Kila napokatazama kafamilia kangu kadogo mawazo haya yananiijia,hawa si watateseka sana nisipoacha wosia? Tumeanza wote maisha,Mungu amejaalia tunazo mali za kushikika,sina sababu za kuwaacha kwenye mtanziko.
Katika mirathi nyingi ndugu wamekuwa wanyama sana,tena wengine wakiwa na vipato vyao ajabu wanaangaika na mali za marehemu.
Nawashauri vijana wenzangu mtoke kwenye imani za uongo eti ukiandika wosia unajichulia kifo,hapana! Ukishakuwa na nyumba,ardhi,usafiri,akaunti na biashara,andika nyaraka itakayowazuiwa kamati ya roho mbaya kusumbua familia yako siku ikitangulia.
Naandika wosia,nataka familia yangu ifurahi siku nikifa