Nimejiridhisha kuwa nina sifa na vigezo, nitagombea 2025

Sep 13, 2023
35
46
Wapendwa,

Kwa muda sasa nimekua na ziara ya muda mrefu kujifunza, kusoma ramani na kupima upepo wa kisiasa, kuskiza maoni, mitazamo, ushauri na kwakweli kusaidiana na wananchi wa Jimbo la chemba na actualy ndio nyumbani kwetu, katika kutatua changamoto ndogo, za kati na kubwa kadiri nilivyojaaliwa.

Kwasasa nipo nashughulika na kufuatilia kwa karibu zaidi swala la mgogoro wa ardhi baina ya mamalaka za serikali za uhifadhi misitu na kijiji cha handa kwa upande wa jimbo hili la chemba mkoani dodoma na baadhi ya vijiji katika wilaya ya ikungi mkoani Singida.

Kuna wananchi wamethirika na mzozo huu phisically, ninawaombea Mwenyezi Mungu awajalie uponyaji wa haraka, uvumilivu, ustahimilivu na moyo wa subra wakati serikali kuu ikijaribu kutafuta suluhu ya kudumu ya jambo hili.

Ndugu zangu, jambo moja ninaloliomba kutoka kweni ni maombi.
Haya mengine kwa neema na baraka za Mungu nitayamudu.

Changamoto ni nyingi mno jimboni, hakuna mtetezi, hakuna wa kuwafuta machozi wananchi, kuna hali ya kukata tamaa sana miongoni mwa wananchi.

Kutokana na changamoto kua nyingi nimeawiwa kujitokeza kuwasaidia wananchi hawa wanyonge katika kutatatua matatizo yao mtambuka.

Nitaanza na vipaumbele vitatu muhimu sana: MAJI, AFYA NA ELIMU.

Hii ni kwa awamu ya kwanza,na baada ya hayo tutaendelea na mengine kadiri ya vipaumbele kwa wakati muafaka.

Nimekata shauri kwa moyo wa dhati kabisa, nakuja kuwafuta machozi, nakuja kuwatetea, nakuja kuwasemea nakuja kuwasaidia.

Mipango, maelezo na maelekezo mengine nitayabainisha wakati muafaka. kwasasa ni hayo tu. Wito wangu kwenu ninaomba mnipokee kwa pamoja na kwa umaja wenu tutashinda.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Asante.
 
Hv Chemba si ndo pana sehemu inaitwa Soya 🤔, eb eleza plan yako jinsi unaenda kutatua changamoto ya upatikanaji huduma ya maji, migogoro ya ardhi
 
Hv chemba si ndo pana sehemu inaitwa soya 🤔, eb eleza plan yako jinsi unaenda kutatua changamoto ya upatikanaji huduma ya maji, migogoro ya ardhi
Kutatua changamoto ya maji au atakavyoenda kuiomba serikali itatue changamoto ya maji??
 
Wapendwa,

Kwa muda sasa nimekua na ziara ya muda mrefu kujifunza, kusoma ramani na kupima upepo wa kisiasa, kuskiza maoni, mitazamo, ushauri na kwakweli kusaidiana na wananchi wa Jimbo la chemba na actualy ndio nyumbani kwetu, katika kutatua changamoto ndogo, za kati na kubwa kadiri nilivyojaaliwa...
All the best comrade
 
Sasa utatue migogoro ya ardhi wakati wewe sio mtaalamu🤣
We ni Kama babu tale😂
Unatafuta ulaji tu
Angalia mbunge aliyepo asijekuloga
 
Back
Top Bottom