Nimejiridhisha ana chuki binafsi juu yangu, hatua gani ifuate?

Sheikh23

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
1,128
1,842
Habari za muda huu, nitafupisha stori ila mwisho wa yote naomba ushauri maana jukwaa hili lina wadau wengi ambao pia huenda yashawakuta au yamewakuta ndg, jamaa, rafiki wa karibu au pia hata kuwahi kusikia haya nitakayoyaeleza.

Iko hivi, nina staff mate wangu ambaye anapenda kuvalia njuga bahati mbaya zangu za kiofisi na nje ya ofisi, amekuwa akiniombea mabaya kwa style ya utani na kujichekesha as if ni utani kweli japo wasiwasi wangu ni utani huo kujirudia mara kwa mara.

Ofisi zetu seniors na juniors tunafanana maisha, sioni kuwa cheo kinaweza kuwa sababu ya hili, nasema hivyo kwasababu ki_ protocol anawajibika kwangu kazini.
Sihitaji kukubalika kwake ila mwamba hanikubali, hata kwa ishu ambayo the whole staff watatoa kongore kwangu na idara nayofanyia kazi yy hajawahi kuwa sehemu ya kupongeza.

Nimekua msaada mkubwa wa magumu ya familia yake japo huwa haji direct kwangu, jamaa humtumia wife wake aje kwa wife wangu kumlilia shida na wife hunishirikisha na huwa nampa wife go ahead awasaidie/kuwakopa.

Ilifikia sehemu akianzisha mada hasi juu yangu nikawa "namchana makavu" hata mbele ya kadamnasi ila mbinu hii nimeona imefeli kwa 100%,mwamba mshipa wa aibu ushachomoka!

Mpaka naandika bandiko hili sina kumbukumbu ya ubaya ambao nilishawahi kumfanyia, iwe kwa kudhamiria au kutokudhamiria.

Narudi kwenu wanajamvi watu wa namna hii, snitches, naysayers, backbiters huwa mnadili nao vipi?
 
Mkuu katika maisha lazima wawepo watu ambao nikikwazo kwako so jua bado uko sehemu sahihi__mwanaume hakimbii tatizo (kwenye tatizo ndipo kwenye funzo ndani yake so usitumie nguvu nyingi kwenda nae sawa)

Wewe ishi nae tu hivyo hivyo kwakua tayari ushajua uzaifu wake uko wapi__watu wahivyo karibia kila sehemu wapo hasa hizi kazi zakuajiriwa inakupasa kutumia akili nyingi la sivyo anaweza hata kutengeza mchongo wamagendo then msala ukakutwa nao ww mwisho ofici ama kampuni ikakupoteza uraiani so be strong
 
Masuala ya kuajiliwa ni shida sana mtu anaweza kukuchukia hata bila sababu yoyote na iko tayari kukufanya mbaya.......niliacha kazi za watu hiyo ikiwa sababu moja yaku.
Kwaio huko ulipo sasa hivi hakuna wanaokuchukia?

Na waliotayari kukufanyia mambo mabaya...?
 
Snitches get stitches! We endelea kuvunga mpka aje akumalize ndo uanze kung'aa macho. Hapo ni kelebu moja kubwa ikifuatiwa na katafunua moja hatari kwisha habari yake.

Mkuu, in this life, the law of the jungle (eat or be eaten) applies everywhere. Kama umethibitisha ana chuki binafsi usingoje sana.

Mmalize mapema.

He who throws the first punch has an advantage.
 
Snitches get stitches! We endelea kuvunga mpka aje akumalize ndo uanze kung'aa macho. Hapo ni kelebu moja kubwa ikifuatiwa na katafunua moja hatari kwisha habari yake.
Mkuu, in this life, the law of the jungle (eat or be eaten) applies everywhere. Kama umethibitisha ana chuki binafsi usingoje sana. Mmalize mapema. He who throws the first punch has an advantage.
Mkuu,hapo kwenye "the law of the jungle" tupo pamoja
 
Bro kuhusu kuchukiwa jambo la kawaida na mtu anakuchukia jua kabisa kuna kitu umemzidi na wewe una akili timamu ambae hachukiwi ni kichaa pekee maana hana athari katika maendeleo yake binafsi

Katika ofisi ukiachan na tabasamu la usoni hakuna usalama kweny mioyo ya staffs wenzio better huyo anaonyesha direct je hao wasengenyaji kuwa makini maana maslahi na maisha mnafanana so dharau kawaida na chuki kikubwa jiweke mbali na pia huchangiwa na mazoea ya ovyo mkisha zoeana dharau ndo huanza
 
Bro kuhusu kuchukiwa jambo la kawaida na mtu anakuchukia jua kabisa kuna kitu umemzidi na wewe una akili timamu ambae hachukiwi ni kichaa pekee maana hana athari katika maendeleo yake binafsi

Katika ofisi ukiachan na tabasamu la usoni hakuna usalama kweny mioyo ya staffs wenzio better huyo anaonyesha direct je hao wasengenyaji kuwa makini maana maslahi na maisha mnafanana so dharau kawaida na chuki kikubwa jiweke mbali na pia huchangiwa na mazoea ya ovyo mkisha zoeana dharau ndo huanza
Ubarikiwe Mkuu
 
Nakusikitikia unadeal na mtu ambae huitaji chochote kwake na unaweza kuishi bila yeye,Kumbuka unapoteza muda bro.

Mi watu wa hivyo huwa natumia mbinu moja huwa nahakikisha Tunagombana tena ugomvi mkubwa nahakikisha hatotamani kuongea na mimi tena!

Kumbuku huyo ni mtu mmoja kati ya watu zaidi ya milioni moja wanaokufahamu,We sio malaika kila mtu uelewane nae...Nina mengi ya kukwambia ila naishia hapo,

Hao watu wapo na hawataisha kwa sababu jinsi ulivyopata wewe kazi mnatofautiana sana wengine ni watoto wa wakuu hapo.
 
Sio bure.
Inawezekana mke wake alikusifia kwa wema wako ndio ikawa tabu.
Wanawake wakigombana na waume zao hua yanawatoka maneno Kama
"Mbona hujifunzi kwa baba Fulani, au mbona wewe unakunywa mipombe mbona baba Fulani hanywi au mbona hututoi out Kama baba Fulani anavyofanya"??
 
Masuala ya kuajiliwa ni shida sana mtu anaweza kukuchukia hata bila sababu yoyote na iko tayari kukufanya mbaya.......niliacha kazi za watu hiyo ikiwa sababu moja yaku.
Niliwahi pitia hali hii , makazini kuna watu wanaroho za ajabu sana
 
Jua kuwa jamaa hakuheshimu. Haiwezekani mtu unamsaidia kwenye shida zake halafu anakuanzishia mada hasi mbele za watu. Hapendi ufanikiwe nk. Hapo tatizo siyo chuki, tatizo ni hakuheshimu. Anakuona boya mmoja hivi. Na hata maonyo uliyompa alikuona mjinga fulani. Muonyeshe vitendo. Kata huo msaada unampa. Yeye na wewe iwe kazi tu. Jiheshimishe. "Bora kuogopwa kuliko kupendwa."
 
Siku mkoromee mpaka mashetan yapande.. .si unajua kila MTU anashetani wake...mi nikifura at the maximum aisee sitamaniki....omba huyo shetan wako akipanda asiwe wa muuaji maana hatoacha alama sekunde tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom