Edson Carrington
JF-Expert Member
- Oct 30, 2022
- 216
- 634
Habari wakuu,
Mapenzi ni moja ya nguzo muhimu sana ya maisha yetu ya kila siku, na haijalishi ni aina gani ya mapenzi mtu aliyonayo as long as mapenzi basi ni strong emotion inayoweza kumuongoza mtu kufanya jambo fulani. Haswa na zaidi ni mahusiano ya kimapenzi.
Yupo mtu mmoja aliyewahi kusema mapenzi yana nguvu zaidi ya lori lililobeba tani nyingi za mzigo. Ikimaanisha mapenzi yana nguvu ya kufanya vitu vingi duniani tofauti na ilivyo kawaida kwa binadamu. Takribani miaka 80 iliyopita wanafunzi wa Harvard university walikuja na conclusion kuwa mapenzi ni chanzo kikuu cha furaha ya mwanadamu na wala sio pesa, urembo, umaarufu nk.
Lakini Changamoto kuu na kubwa ya mapenzi haswa ya mtu na mtu ( me na ke ) ni moja tu, kwani ni WIVU. Always mapenzi huja na wivu. Na pia kiwango cha mapenzi kinavyoongezeka na pia kiwango cha wivu kinaongezeka.
Hakuna mapenzi ya kweli yasiyokuwa na wivu, na wala hakuna asiekuwa na wivu kwenye mapenzi pale atakapoona mambo yanaenda tofauti.
Bali tofauti kubwa ni reaction ya mtu fulani juu ya suala hilo.
Mapenzi yana thamani sana kama unavyoona pesa na mali nyingine mbalimbali. Ndio maana watu wapo tayari kutoa mpaka utajiri wao kwa wanaowapenda. Mtu anapokupa moyo wake hakuna tofauti na mwajiri anaempa mwajiriwa wake kampuni kubwa kwa ajili ya kuisimamia na kuiendesha. Na inapotokea umefanya usaliti kwa penzi la mtu ni sawa na kufanya usaliti kwenye mali ya kampuni hiyo. Huu ndo mfano hai wa dhamana ya mapenzi.
Kiukweli nimejifunza mengi kuhusiana na mapenzi kutoka kwa walionitangulia lakini kwa hili nimeshindwa kuwaelewa hata kidogo. Je, inakuaje uondoe wivu kwa yule unaempenda?,
Sawa wivu ni kidonda, lakini je nawezaje kuishi bila kuwa na wivu kwa yule niliemweka moyoni?!
Kiukweli sijawahi kupata suluhisho katika hili.