Nimejifunza kuheshimu wanawake

Nimejifunza kuheshimu wanawake

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
9,932
Reaction score
11,849
Nilikuwa nawadharau sana wanawake niliwaona kama viumbe dhaifu wasio na akili na hii ilitokana na mazingira niliyokulia ambapo mwanamke anadharaulika na kubezwa.

Wiki iliyopita nilimpeleka mke wa kujifungua kwenye hospitali ya private ambapo hospitali hiyo ina utaratibu wa kumzalisha mwanamke mmewe wake akiwa pembeni anaangalia, aisee kuzaa ni shughuli asikwambie mtu nilitoka labour nduki mpaka sasa nikifikria kitendo kile nimeanza kuwaheshimu wanawake .

Kama hospitali zote zingelikuwa na utaratibu ule hakika wanaume tungewaheshimu wake zetu, mama zetu na wanawake wote kwa ujumla acha mama aitwe mama.
 
Kwa mara ya kwanza nilienda mwananyamala kufatilia uzazi wa wife aliyejifungia kwa operation ,asee mambo niliyayakuta kule na changamoto zao....
 
Hata hivyo ,wanaume tunachangamoto kuliko wanawake...mwanaume analea mwanamke ,mimba yake ,mtoto na kaka au dada zake ,maendeleo ya familia ,nk nk
 
Mungu alisema Mwanamke atazaa kwa uchungu na Mwanaume atakula kwa jasho, hivyo hiyo ni nature Mungu aliyoiweka. Lazima iwe hivyo.
 
Mimi nilimpeleka general dom uchungu ukakata akakaa wiki ila nilikuwa silali.Namheshimu xana mke wangu somtm akideka nmwangalia tu.
 
Mimi nikipewa kazi ya kuangalia wanawake wanapozaa hata bure nitafanya. Very Interesting...
 
Back
Top Bottom