nimeitoa cheka na kitine.

nimeitoa cheka na kitine.

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,650
Reaction score
21,014
Mume kaingia duka la nguo na kamnunulia my waif wake chupi dazani moja zote za rangi moja, akaenda kumzawadia. Mupenzi akashukuru lakini alipogundua kuwa zote rangi moja si akalopoka.
MAI WAIF: Sasa umeninunulia chupi zote rangi moja, watu si watadhani nina chupi moja tu sibadili................................... Hapo ndipo zogo kuu lilipoanza

MUME:Watu gani hao? Leo utanambia'

​
 
Mtoto: Mama leo tulipokuwa kwenye daladala na baba, si akaniambia nisimame nilipokaa kusudi akae Anti.
Mama: Safi sana mwanangu, baba yako anakufundisha adabu nzuri, kwa hiyo kumbuka kila mara wakubwa wakija unawaachia kiti.
Mtoto: Sikuwaachia kiti, baba alikuwa amenipakata ndio akaniambia nisimame Anti akae.
Mama: Hebu rudia tena sijasikia vizuri
​
 
Binti alirudi kijijini baada ya miaka 5.
BABA: We mwanaharamu umeondoka hapa kwa miaka mitano hukutaka hata kutuandikia barua wala kutuma salamu unajua ulimtesa sana mama yako?
BINTI: Baba niliona niwe kimya nilikuwa nafanya kazi ya umalaya
BABA: Ayaaaaaa umetia aibu kubwa familia yangu lohh, ntatembelea wapi mimi? Kijiji chote watanicheka, kanisa litanitenga, loh jamani jamani. Ondoka hapa kijijini haraka sasa hivi
BINTI: Sawa baba, lakini nimemletea mama sanduku la nguo na kanga 20 na pesa, na hii hapa ni hati ya kiwanja nimemnunulia. Na wewe baba nimekununulia hilo Fuso nililokuja nalo na nimekufungulia akaunti benki, ina pesa utaweza kulima vizuri na kujenga nyumba nyingine ya kisasa, mwaka kesho nakuletea trekta.
BABA: Ulisema ulikuwa unafanya kazi gani?
BINTI: Umalaya
BABA: Unajua nilisikia vibaya nilidhani ulisema Uyaya, pole na kazi mwanangu
 
Mke alikwenda kulalamika kwa mumewe kuwa kuna jamaa mgeni jirani kamtukana kuwa ana mdomo kama tairi la trekta. Mume akapandisha na kuapa kutoa adhabu kali sana atakapokutana na huyo mshenzi. Siku walipokutana mume kanywea maana jamaa alikuwa baunsa wa ukweli;
MUME: Mambo jirani?
JIRANI: Mbona poa sana tu
MUME: Jirani nasikia ulimtukana mke wangu kuwa ana mdomo kama tairi la trekta
JIRANI: Ndio
MUME: Ahahha, tairi la mbele au la nyuma?
JIRANI: La nyuma
MUME
: Ahaa nilidhani ulisema la mbele, inaonekana mimi na wewe tunawaza sawa, ila tu sijamwambia wife, si unajua akina mama wanavyoweza kupanik.
​
 
photo.php.jpg
 
MDADA: Bebi sizioni siku zangu
MKAKA: Kwa hiyo mie nimekuibia? mie mwizi sio? Yaani umeona sasa ndio unidharau kabisaaa. Hebu beba kilicho chako na usepe
 
MGENI: Dah mbwa wenu mbona ananiangalia sana ninapokula?
DOGO: Labda kwa sababu unatumia sahani yake anayotumiaga kula​
 
Wababa watatu wamekutana bar, ulevi ulipowazidia wakaanza kuongea kuhusu binti zao,
BABA 1: Kuna siku niliingia chumba cha binti yangu nikashanga kukuta kichungi cha sigara wakati najua havuti
BABA 2: Mi nilikuta chupa tupu ya bia wakati binti yangu hanywi
BABA 3: Wangu ndo ya ajabu zaidi, mi nilikuta kondom ya kiume imetumika chumbani kwake wakati yeye mwanamke.
 
.Dah jamaa mmoja alipita mbele ya nyumba yangu mkononi amebeba mtoto, kutokana na mvua za jana kuna madimbwi hapa, jamaa amejaribu kuruka dimbwi moja bahati mbaya kateleza na kuishia mzima mzima kwenye dimbwi, nimemsifu sana alivyojitahidi mtoto asiumie, ila yeye mwenyewe tope tupu na anachechemea. Mtoto ndio amefanya wengi tuliokuwepo hapo tukimbie tukachekee pembeni maana mtoto kang'ang'ania, 'Baba baba rudia tena'
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom