Elections 2015 Nimeipenda hii ya Mwigamba kwa Mwanakijiji

Mongoiwe

Mongoiwe

JF-Expert Member
523
250
kuna tatizo moja la CDM kudhani kila kitu kipo sawa kama wanavyotaka wao, hujuma wanazijua walishinda Igunga sasa walishindaje wasishinde Igunga na leo Arumeru? Hii ndiyo hoja ya Mwanakijiji.
 
Eng. Y. Bihagaze

Eng. Y. Bihagaze

Verified Member
1,481
1,225
Kwa Muda nimekuwa nikipitia Hoja za Mwanakijiji ndani Na nje ya Jamvi hili.. Hata Hoja yako unayomchambua mwigaz hapa nimeisoma Kwa makini. Sasa nashawishika kufikiria kuna agenda ya Siri ndani ya matamshi Na maandishi yako ambayo hutaki kuiweka bayana.
Majuzi tulibishana sana juu ya Mabadiliko juu ya maandiko ya Mwanakijiji. Wengine walisema ameshamezwa Na Gambaz wengine walisema ni Bomu la Mtu. si Lengo langu kukunanga Nguli wa habari kama wewe kwamba umeshachakachuliwa au si Lengo langu kukushinikiza kuandika mema ya Chama fulani Na Mabaya ya serikali Na cha Chake la-hasha, Lakini maandiko yako ya siku hizi za usoni yamepoteza mvuto wa uhalisia Wa Mwandishi mahiri. Ni kana kwamba kuna Nguvu ( nje Na Utashi wa asili yako) unayokushurutisha kuandika unachoshurutishwa kuandika Kwa mantiki ya kuibua hisia ngeni Kwa wasomaji wanaopenda nakala zako. Mathalan niliposoma andiko lako CHADEMA wakipoteza jimbo (Arumeru Mashariki ) Basi Timu nzima ya Uongozi wa juu (ambao hukuutaja Kama ni wa kitaifa au la) unapaswa Kujiuzulu. Kwangu nilisoma Kwa matarajio kadhaa, kwanza kujua kwanini umeoanisha uchaguzi wa jimbo Na viongozi Hao uliowaita wewe ambapo sikupata jibu, pili kwanini ulienda mbali Kwa kuwataka wajiuzulu Na si vinginevyo ambapo pia sikupata jibu ila top nilitarajia Basi utawataka wajiuzulu kisha utoe pendekezo mbadala Lakini hujafanya hivyo.. Ukasema tu wajiuzulu enhe kisha?!! Nani awe nani baada ya hayo.. Maandiko ambayo Hayana majibu yanalenga kuchanganya jamii Na sio uandishi mzuri Kwa Nguli wa tasnia hii Kama wewe. Mwigaz katika Kurunzi lake hili amepambanua kwenye dhima ya andiko lake kwamba Ziko sababu kadhaa si kura tu inayoweza kufanya mtoa tangazo aka tamka ushindi Kwa mgombea. Akasema kuna Kura ya mwananchi, nguvu za Dola akimaanisha Tume, Serikali, Polisi, Usalama wa T, Lakini pia kuna Mabavu, sasa Katika mchango wa majibu yako umekuwa mbishi tu, ukinukuu vifungu vyake Na kuvikosoa Na kusahau dhima ya awali ya andiko lako kuhusu kujiuzulu Kwa viongozi uliowataka jimbo wasipolinyakua.
Ndiposa Narejea kwenye wasiwasi wangu kwamba si bure Mwanakijiji naye "ameshatembelewa" Na "akatembeleka".. Kama ni kweli Basi itakuwa aibu sana kwenye utashi Wa nafsi yako Kama mzalendo..
 
Daudi Mchambuzi

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
46,376
2,000
Same topic zinazungumzia same party na same person kubali kataa mtajimaliza kwa majungu na choyo! Huyo mnaemsifia juzi kazi tu Rev Mzito K alimchana vibaya kwenye thead yake na wengi wenu mlichana pia nashangaa leo hii mnamsifia huu unaitwa ujuha!

Ifike wakati watu watambue michango ya watu ndani na nje ya vyama sio leo asemwe vibaya kesho asemwe vizuri wenye akili timamu watawaona hamnazo! Tuache fitina na majungu yanaoendeshwa na choyo!
:focus::focus::focus:
 
TIMING

TIMING

JF-Expert Member
21,844
1,250
kuna mambo inawezekana sijayasoma from MMM au kuelewa from others.... kushinda Arumeru kunawezekana, ila itakua ni kujenga nyumba kwa tofali la baragu kwani madiwani wana role kubwa ya kuplay

I may be off topic but i think Mwigamba and MMM all missed something....... the power of ignorance!!!
 
MTAZAMO

MTAZAMO

JF-Expert Member
15,541
2,000
Kwa Muda nimekuwa nikipitia Hoja za Mwanakijiji ndani Na nje ya Jamvi hili.. Hata Hoja yako unayomchambua mwigaz hapa nimeisoma Kwa makini. Sasa nashawishika kufikiria kuna agenda ya Siri ndani ya matamshi Na maandishi yako ambayo hutaki kuiweka bayana.
Majuzi tulibishana sana juu ya Mabadiliko juu ya maandiko ya Mwanakijiji. Wengine walisema ameshamezwa Na Gambaz wengine walisema ni Bomu la Mtu. si Lengo langu kukunanga Nguli wa habari kama wewe kwamba umeshachakachuliwa au si Lengo langu kukushinikiza kuandika mema ya Chama fulani Na Mabaya ya serikali Na cha Chake la-hasha, Lakini maandiko yako ya siku hizi za usoni yamepoteza mvuto wa uhalisia Wa Mwandishi mahiri. Ni kana kwamba kuna Nguvu ( nje Na Utashi wa asili yako) unayokushurutisha kuandika unachoshurutishwa kuandika Kwa mantiki ya kuibua hisia ngeni Kwa wasomaji wanaopenda nakala zako. Mathalan niliposoma andiko lako CHADEMA wakipoteza jimbo (Arumeru Mashariki ) Basi Timu nzima ya Uongozi wa juu (ambao hukuutaja Kama ni wa kitaifa au la) unapaswa Kujiuzulu. Kwangu nilisoma Kwa matarajio kadhaa, kwanza kujua kwanini umeoanisha uchaguzi wa jimbo Na viongozi Hao uliowaita wewe ambapo sikupata jibu, pili kwanini ulienda mbali Kwa kuwataka wajiuzulu Na si vinginevyo ambapo pia sikupata jibu ila top nilitarajia Basi utawataka wajiuzulu kisha utoe pendekezo mbadala Lakini hujafanya hivyo.. Ukasema tu wajiuzulu enhe kisha?!! Nani awe nani baada ya hayo.. Maandiko ambayo Hayana majibu yanalenga kuchanganya jamii Na sio uandishi mzuri Kwa Nguli wa tasnia hii Kama wewe. Mwigaz katika Kurunzi lake hili amepambanua kwenye dhima ya andiko lake kwamba Ziko sababu kadhaa si kura tu inayoweza kufanya mtoa tangazo aka tamka ushindi Kwa mgombea. Akasema kuna Kura ya mwananchi, nguvu za Dola akimaanisha Tume, Serikali, Polisi, Usalama wa T, Lakini pia kuna Mabavu, sasa Katika mchango wa majibu yako umekuwa mbishi tu, ukinukuu vifungu vyake Na kuvikosoa Na kusahau dhima ya awali ya andiko lako kuhusu kujiuzulu Kwa viongozi uliowataka jimbo wasipolinyakua.
Ndiposa Narejea kwenye wasiwasi wangu kwamba si bure Mwanakijiji naye "ameshatembelewa" Na "akatembeleka".. Kama ni kweli Basi itakuwa aibu sana kwenye utashi Wa nafsi yako Kama mzalendo..
Yamekuwa haya tena!
 
Daudi Mchambuzi

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
46,376
2,000
Nimeipenda sana makala ya Mwigamba. Bahati mbaya ni kuwa yote ambayo ameyasema juu ya kazi ngumu ambavyo wameifanya na wanaendelea kuifanya katika kushinda chaguzi mbalimbali niliyafikiria wakati najenga hoja yangu ya awali. Sina fikra za kujidaganya kuwa ni rahisi kushinda dhidi ya mashine a.k.a CCM. Lakini, kama nilivyosema awali na maneno ya Mwigamba yanashuhudia Arumeru Mashariki wanapaswa kushinda - kwa hili hajatofautina na mimi.

Anachotofautiana na mimi ni matokeo ya kushindwa. Kwamba, wakishindwa hata kihalali bado wataandamana. Binafsi naamini wakishindwa kihalali bado watahitaji KUJIUZULU. Kwa sababu HAWANA SABABU ya kushindwa Arumeru Mashariki. Sasa haitoshi kudai tu kuwa "watangazwe washindi" la hasha ni LAZIMA watangazwe washindi kwa sababu WAMESHINDA. Hatutaki kutengeneza demokrasia ya kusubiri mtu kutangazwa mshindi; tunataka demokrasia ya mshindi wa halali ndiye anatangazwa mshindi.

Maneno kama haya:Hayana msingi. Kama tukiamini ni ya kweli tunauliza ni lipi kati ya hayo ambalo CCM na serikali hayakufanya Igunga, Kiteto, Biharamulo au Mbeya Vijijini? Ni lipi ambalo halikufanyika Tarime? Sasa, haya yote si mageni na CDM wamekubali kushiriki uchaguzi! Kama yangekuwa mabaya hivyo wangejitoa kupinga lakini wameamua kushiriki kwa hili hatuwezi kuona huruma kwa kweli. Wamekubali kucheza, wamemkubali refa, wamekubali sheria, wamekubali uwanja, wawe tayari kukubali matokeo!

Anasema:Demokrasia gani hii tunataka kuipigania? Mnataka CCM wasitangazwe washindi kama wameshindwa lakini CDM itangazwe mshindi hata kama haijashinda? Haifai na si haki kujiandaa kuhakikisha kwamba "tunatangazwa washindi"! Mlitakiwa kujiandaa toka mwanzo kwamba "mnashinda ili kutangazwa washindi". CDM wasije kudai kutangazwa washindi wakati hawakushinda vinginevyo zoezi zima la kupiga kura litakuwa halina maana!

Lakini nimeyapenda maneno haya pia ambayo yanaonesha kujiamini na kujipanga:CDM haina sababu ya kushindwa Arumeru Mashariki; NONE. Haijalishi CCM na serikali inafanya nini na hiyo ndiyo msingi wa hoja yangu ya awali kabisa. Kwamba, hata tukichukulia mbinu zote chafu na kila aina ya dhulma bado naona CDM inashinda na inapaswa kushinda hasa kama ikitumia mikakati makini. Wenye kupanga na kusimamia mikakati hiyo ni viongozi wa taifa; ndio wao wanapanga bajeti na kutuma watu huko na kusimamia kampeni nzima. Ndio maana naamini kabisa kuwa haijalishi CDM wanaweza kushindwa vipi (kwa dhulma au kwa haki) bado uongozi mzima wa taifa ni lazima ujiuzulu. Na kwa vile kiongozi wa mkoa naye amesema kuwa ni lazima watangazwe washindi (natumaini ana maana baada ya kushinda) basi wakishindwa na uongozi wake wa mkoa nao ujiuzulu.

Wakiamua kuandamana kwenda Ikulu, wafanye hivyo wakiwa tayari WAMEJIUZULU! Nitawaunga mkono.
Mkuu swala la kufanya library research mwisho wake unaishia kuandika hadithi za kusadikika.
Hii ni moja Kati ya maandiko yaliyo-shake credibility ya weledi wako mzee.
Hujioni kama unalazimisha kushindana while unapaswa kujibu hoja za msingi hususani kutoka kwa mtu anayefanya field research.
Unaposingizia kuwa eti mwigamba kasema CDM wataandamana hata wakitangazwa sio washindi kihalali unadhihirisha kuwa unajilazimisha kutokuelewa hili hali unajua hicho ulichokisema hakijaandikwa wala kusemwa ktk makala hii ya mwigamba.
Mpaka sasa siamini kama haya unayoandika unakusudia au ni tatizo la kujivua ufahamu hasa ukizingatia huendi kwenye field.
Naamini ungeonyesha busara kwa kukiri kuwa si sahihi kuzungumzia maswala makubwa pasi kufanya research za maana(hasa field research).
Muungwana angefurahi kusahihishwa ili aweze kufanya kazi nzuri zaidi hapo baadaye.
Kubali hii ni challenge, ulichemka mzee.
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
32,933

Well, nasimamia kila neno nililoandika. Na 'field research' hakuna aliyefanya unless neno 'field research' limepoteza maana. Haiitaji mtu kuwa on the field kujua kinachoendelea kwenye sehemu hiyo kuna njia nyingi tu za kujua.
 
mayenga

mayenga

JF-Expert Member
4,062
2,000
Makala za Mwanakikjiji zinahitaji tafakuri kubwa,sidhani kujiuzulu anakomaanisha kwa viongozi wa chadema,ni kujiengua na kukaa pembeni.Nakumbuka maneno aliyotamka F.Mbowe wakati wa ufunguzi wa kampeni Arumeru.Alisema''Serikali ya CCM ina polisi,jeshi mgambo na kila kitu,ila CHADEMA ina nguvu ya umma''.Inatosha tu kusema juhudi za viongozi wa CHADEMA katika hili zinaonekana wazi,hivyo basi kama ni kuwajibika,wawjibike Wananchi wasiyoyaelewa mabadiliko,wawajibike Maafisa wa tume watakaopindisha matokeo ,na viwajibishwe vyombo vya usalama ambavyo vitashindwa kutenda haki na usawa.
 
OTIS

OTIS

JF-Expert Member
2,151
1,195
Nimeipenda sana makala ya Mwigamba. Bahati mbaya ni kuwa yote ambayo ameyasema juu ya kazi ngumu ambavyo wameifanya na wanaendelea kuifanya katika kushinda chaguzi mbalimbali niliyafikiria wakati najenga hoja yangu ya awali. Sina fikra za kujidaganya kuwa ni rahisi kushinda dhidi ya mashine a.k.a CCM. Lakini, kama nilivyosema awali na maneno ya Mwigamba yanashuhudia Arumeru Mashariki wanapaswa kushinda - kwa hili hajatofautina na mimi.

Anachotofautiana na mimi ni matokeo ya kushindwa. Kwamba, wakishindwa hata kihalali bado wataandamana. Binafsi naamini wakishindwa kihalali bado watahitaji KUJIUZULU. Kwa sababu HAWANA SABABU ya kushindwa Arumeru Mashariki. Sasa haitoshi kudai tu kuwa "watangazwe washindi" la hasha ni LAZIMA watangazwe washindi kwa sababu WAMESHINDA. Hatutaki kutengeneza demokrasia ya kusubiri mtu kutangazwa mshindi; tunataka demokrasia ya mshindi wa halali ndiye anatangazwa mshindi.

Maneno kama haya:Hayana msingi. Kama tukiamini ni ya kweli tunauliza ni lipi kati ya hayo ambalo CCM na serikali hayakufanya Igunga, Kiteto, Biharamulo au Mbeya Vijijini? Ni lipi ambalo halikufanyika Tarime? Sasa, haya yote si mageni na CDM wamekubali kushiriki uchaguzi! Kama yangekuwa mabaya hivyo wangejitoa kupinga lakini wameamua kushiriki kwa hili hatuwezi kuona huruma kwa kweli. Wamekubali kucheza, wamemkubali refa, wamekubali sheria, wamekubali uwanja, wawe tayari kukubali matokeo!

Anasema:Demokrasia gani hii tunataka kuipigania? Mnataka CCM wasitangazwe washindi kama wameshindwa lakini CDM itangazwe mshindi hata kama haijashinda? Haifai na si haki kujiandaa kuhakikisha kwamba "tunatangazwa washindi"! Mlitakiwa kujiandaa toka mwanzo kwamba "mnashinda ili kutangazwa washindi". CDM wasije kudai kutangazwa washindi wakati hawakushinda vinginevyo zoezi zima la kupiga kura litakuwa halina maana!

Lakini nimeyapenda maneno haya pia ambayo yanaonesha kujiamini na kujipanga:CDM haina sababu ya kushindwa Arumeru Mashariki; NONE. Haijalishi CCM na serikali inafanya nini na hiyo ndiyo msingi wa hoja yangu ya awali kabisa. Kwamba, hata tukichukulia mbinu zote chafu na kila aina ya dhulma bado naona CDM inashinda na inapaswa kushinda hasa kama ikitumia mikakati makini. Wenye kupanga na kusimamia mikakati hiyo ni viongozi wa taifa; ndio wao wanapanga bajeti na kutuma watu huko na kusimamia kampeni nzima. Ndio maana naamini kabisa kuwa haijalishi CDM wanaweza kushindwa vipi (kwa dhulma au kwa haki) bado uongozi mzima wa taifa ni lazima ujiuzulu. Na kwa vile kiongozi wa mkoa naye amesema kuwa ni lazima watangazwe washindi (natumaini ana maana baada ya kushinda) basi wakishindwa na uongozi wake wa mkoa nao ujiuzulu.

Wakiamua kuandamana kwenda Ikulu, wafanye hivyo wakiwa tayari WAMEJIUZULU! Nitawaunga mkono.

Hapa kwenye kutumia busara ndipo MM unapotofautiana sana na wapenzi wengi wa CDM
Hata pale wanaposhindwa kwa haki wao hukimbilia kusema wameshinda na kutaka kuleta vurugu.Huu sio utu na ustaarabu na dhana nzima ya kupiga kura inatoweka.
Binafsi nimeshakutana na wanachama wengi wa CDM ambao wao ni siasa ya ushindani inawashinda na kutangaza vita hapa pale panapostahili mazungumzo.
Tabia hizi ndizo zinairudisha CDM nyuma na ni wachache sana wanaoliona hili na kulifanyia kazi.
Ukishindwa kubali na mpongeze aliekushinda.
Hata wananchi wataona kuwa CDM ni chama komavu.
OTIS
 
Avanti

Avanti

JF-Expert Member
1,209
1,195
Well, nasimamia kila neno nililoandika. Na 'field research' hakuna aliyefanya unless neno 'field research' limepoteza maana. Haiitaji mtu kuwa on the field kujua kinachoendelea kwenye sehemu hiyo kuna njia nyingi tu za kujua.
Nimekupenda, una uelewa mzuri sana. Unajua, Mwigamba kuwepo kwake Arumeru basi anadhani anaelewa mambo ya hapo kuliko mtu aliyeko mbali na huko. Kwanza naamini hata makala yake ni ya kutaka kujenga hoja kwamba CDM watashinda wakati hata moyoni mwake hana uhakika huo. Mimi nilikuelewa sana ulipotumia neno "kujiuzulu" ulikuwa una maana gani. Najua hata yeye ni kiongozi wa CDM Arusha ndiyo maana imemchoma sana ile makala yako. Anyway ninachotaka kusema hapa Mwigamba namkubali kwamba ni mwandishi mzuri, lakini naye ana dosari, kama mimi, Mwkjj na mtu mwingine yeyote. Mimi naamini Mwigamba hayupo rational, yeye ni irrational kwani anataka watu wamwamini yeye tu hata pale yeye mwenyewe toka moyoni mwake hana kile ambacho anataka watu wengine waamini toka kwake.
 
Daudi Mchambuzi

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
46,376
2,000
Well, nasimamia kila neno nililoandika. Na 'field research' hakuna aliyefanya unless neno 'field research' limepoteza maana. Haiitaji mtu kuwa on the field kujua kinachoendelea kwenye sehemu hiyo kuna njia nyingi tu za kujua.
mkuu siamini kama ni wewe unaandika haya maneno.
 
M

maramojatu

JF-Expert Member
203
225
cccm mchezo mchafu acheni jamani. tuachie arumeru yetu salama
 
M

Mazindu Msambule

JF-Expert Member
6,160
2,000
Kwa Muda nimekuwa nikipitia Hoja za Mwanakijiji ndani Na nje ya Jamvi hili.. Hata Hoja yako unayomchambua mwigaz hapa nimeisoma Kwa makini. Sasa nashawishika kufikiria kuna agenda ya Siri ndani ya matamshi Na maandishi yako ambayo hutaki kuiweka bayana.
Majuzi tulibishana sana juu ya Mabadiliko juu ya maandiko ya Mwanakijiji. Wengine walisema ameshamezwa Na Gambaz wengine walisema ni Bomu la Mtu. si Lengo langu kukunanga Nguli wa habari kama wewe kwamba umeshachakachuliwa au si Lengo langu kukushinikiza kuandika mema ya Chama fulani Na Mabaya ya serikali Na cha Chake la-hasha, Lakini maandiko yako ya siku hizi za usoni yamepoteza mvuto wa uhalisia Wa Mwandishi mahiri. Ni kana kwamba kuna Nguvu ( nje Na Utashi wa asili yako) unayokushurutisha kuandika unachoshurutishwa kuandika Kwa mantiki ya kuibua hisia ngeni Kwa wasomaji wanaopenda nakala zako. Mathalan niliposoma andiko lako CHADEMA wakipoteza jimbo (Arumeru Mashariki ) Basi Timu nzima ya Uongozi wa juu (ambao hukuutaja Kama ni wa kitaifa au la) unapaswa Kujiuzulu. Kwangu nilisoma Kwa matarajio kadhaa, kwanza kujua kwanini umeoanisha uchaguzi wa jimbo Na viongozi Hao uliowaita wewe ambapo sikupata jibu, pili kwanini ulienda mbali Kwa kuwataka wajiuzulu Na si vinginevyo ambapo pia sikupata jibu ila top nilitarajia Basi utawataka wajiuzulu kisha utoe pendekezo mbadala Lakini hujafanya hivyo.. Ukasema tu wajiuzulu enhe kisha?!! Nani awe nani baada ya hayo.. Maandiko ambayo Hayana majibu yanalenga kuchanganya jamii Na sio uandishi mzuri Kwa Nguli wa tasnia hii Kama wewe. Mwigaz katika Kurunzi lake hili amepambanua kwenye dhima ya andiko lake kwamba Ziko sababu kadhaa si kura tu inayoweza kufanya mtoa tangazo aka tamka ushindi Kwa mgombea. Akasema kuna Kura ya mwananchi, nguvu za Dola akimaanisha Tume, Serikali, Polisi, Usalama wa T, Lakini pia kuna Mabavu, sasa Katika mchango wa majibu yako umekuwa mbishi tu, ukinukuu vifungu vyake Na kuvikosoa Na kusahau dhima ya awali ya andiko lako kuhusu kujiuzulu Kwa viongozi uliowataka jimbo wasipolinyakua.
Ndiposa Narejea kwenye wasiwasi wangu kwamba si bure Mwanakijiji naye "ameshatembelewa" Na "akatembeleka".. Kama ni kweli Basi itakuwa aibu sana kwenye utashi Wa nafsi yako Kama mzalendo..
Haya maneno yameishihadi sasa, uliandika tarehe 28/3/2012 ni miaka 7 iliopita, was like prophecy na imetokea kweli kwamba MMM alikua na ajenda ya siri since that time. Bahati mbaya hata Mwigamba na yeye kapotea kabisa, sio kwenye siasa tu bali hata kwenye uandishi, haonekani!
 
Forum statistics

Threads
1,425,153

Messages
35,082,647

Members
538,214
Top Bottom