Nimeingia choo cha kike! ....(1)

HorsePower

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
3,612
2,566
Nikiwa ni mwingi wa mawazo na kukumbuka miaka 3 nyuma nilivyotendwa na mdada ambaye sintamsahau maishani mwangu,
Naingia ofcn kwa kishindo nikiwa na uchovu wa kimwili na akili. Walinzi ambao pia ni waosha gari langu wananidaka kwa maneno mengi ya furaha na utani na kunipa misifa nisiyostahili kwa ajili ya visenti vichache ninavyowapa kila mara! Sikutamani kuwaangalia mara mbili kwa ule uchovu, na pia nilielewa fika kuwa misifa yote hiyo ni kutaka kuniomba vijisenti vya kunywea chai!

Nikiwa nimepoteza mtazamo; Najaribu kupandisha ngazi bila uangalifu kuingia ofcn kwangu, ghafla nagongana na binti aliyebeba makabrasha huku akiongea na simu. Anayumba sana, na alipojaribu kapata balance kwa kupapasa sehemu ya kujishikiza kwenye ngazi, anajikuta akinipa kibao kikali shavuni! “Samahani pole sana!” Sauti ilimtoka. Binafsi kwa jinsi alivyo mrembo na ulaini wa mikono yake, sikusikia hata tone la maumivu! Cha kushangaza nilitamani hata aniongeze kofi lingine!

HP jamani hukuniona? Aliuliza lakini ghafla nikajikuta nimemjibu “Mawazo dada, nahisi nimekuwa mwehu!”, heee kwa nini unasema hivyo? Aliuliza “si mwehu tu, nafikiri unaweza kuniita kichaa au mwendawazimu, hata ukiniita taahira nitaridhika. Ebbo? Aling’aka kwa mshangao! Uzuri wako ndiyo ulionifanya niwe hivi ” Niliropoka

“HP sikutarajia” alisema. “Unaonekana mpole na mstaarabu, kwa nini umeanza haya mambo?” Sina utani na sijawahi kufanya utani na nafsi yangu, ni kweli tupu ninayokwambia, sijiwezi kwako niamini, moyo wangu umezizima” niliropoka. Aliniangalia, hakujibu.

Wakati najibizana naye, ki-ukweli sikujielewa maneno yote niliyoyasema niliyapata wapi, kutendwa miaka 3 iliyopita ilinifanya niwachukie wanawake kupita kiasi, na sikuwahi kufikiria kama ningeweza kutumbukia kwenye haya mambo kirahisi namna hii.
Aliinama kwa haraka na kuokota karatasi zake na kuanza kushuka ngazi kwa kasi. Ghalfa nilijikuta nikianza kuongea “Ohh please, naomba ….” Kabla sijamaliza, aligeuka na kuniangalia kwa upole, “unataka nini zaidi?” aliuliza, akanikonyeza

Sifa zake za utulivu na tabia njema zilizagaa kwenye shirika letu hili lisilo la kiserikali. Nilishawahi kusikia vijana wenzangu mara kadhaa wakimsimulia binti huyu kwa jinsi alivyo na misimamo thabiti ya kimaisha na kuonyesha tabia njema. Ingawa ……

****** Itaendelea kesho, ngoja nimalizie kazi za ofisi ***** :A S embarassed:
 
dah! Kweli we kichaa! Utamaliza kesho? U cant be serious? Unafaa kuwa shigongo lakini!
 
Du!Umeanza vizuri sana kwa kweli,ila umetuacha njia panda wakati bado tunataka kuendelea kujua kilichojiri.
 
Nikiwa ni mwingi wa mawazo na kukumbuka miaka 3 nyuma nilivyotendwa na mdada ambaye sintamsahau maishani mwangu,
Naingia ofcn kwa kishindo nikiwa na uchovu wa kimwili na akili. Walinzi ambao pia ni waosha gari langu wananidaka kwa maneno mengi ya furaha na utani na kunipa misifa nisiyostahili kwa ajili ya visenti vichache ninavyowapa kila mara! Sikutamani kuwaangalia mara mbili kwa ule uchovu, na pia nilielewa fika kuwa misifa yote hiyo ni kutaka kuniomba vijisenti vya kunywea chai!

Nikiwa nimepoteza mtazamo; Najaribu kupandisha ngazi bila uangalifu kuingia ofcn kwangu, ghafla nagongana na binti aliyebeba makabrasha huku akiongea na simu. Anayumba sana, na alipojaribu kapata balance kwa kupapasa sehemu ya kujishikiza kwenye ngazi, anajikuta akinipa kibao kikali shavuni! "Samahani pole sana!" Sauti ilimtoka. Binafsi kwa jinsi alivyo mrembo na ulaini wa mikono yake, sikusikia hata tone la maumivu! Cha kushangaza nilitamani hata aniongeze kofi lingine!

HP jamani hukuniona? Aliuliza lakini ghafla nikajikuta nimemjibu "Mawazo dada, nahisi nimekuwa mwehu!", heee kwa nini unasema hivyo? Aliuliza "si mwehu tu, nafikiri unaweza kuniita kichaa au mwendawazimu, hata ukiniita taahira nitaridhika. Ebbo? Aling'aka kwa mshangao! Uzuri wako ndiyo ulionifanya niwe hivi " Niliropoka

"HP sikutarajia" alisema. "Unaonekana mpole na mstaarabu, kwa nini umeanza haya mambo?" Sina utani na sijawahi kufanya utani na nafsi yangu, ni kweli tupu ninayokwambia, sijiwezi kwako niamini, moyo wangu umezizima" niliropoka. Aliniangalia, hakujibu.

Wakati najibizana naye, ki-ukweli sikujielewa maneno yote niliyoyasema niliyapata wapi, kutendwa miaka 3 iliyopita ilinifanya niwachukie wanawake kupita kiasi, na sikuwahi kufikiria kama ningeweza kutumbukia kwenye haya mambo kirahisi namna hii.
Aliinama kwa haraka na kuokota karatasi zake na kuanza kushuka ngazi kwa kasi. Ghalfa nilijikuta nikianza kuongea "Ohh please, naomba …." Kabla sijamaliza, aligeuka na kuniangalia kwa upole, "unataka nini zaidi?" aliuliza, akanikonyeza

Sifa zake za utulivu na tabia njema zilizagaa kwenye shirika letu hili lisilo la kiserikali. Nilishawahi kusikia vijana wenzangu mara kadhaa wakimsimulia binti huyu kwa jinsi alivyo na misimamo thabiti ya kimaisha na kuonyesha tabia njema. Ingawa ……

****** Itaendelea kesho, ngoja nimalizie kazi za ofisi ***** :A S embarassed:
nakumbuka miaka ilee,wakati huo utamaduni wa kusoma riwaya za mapenzi ulikuwa juu sana....btw umejitahadi kuitunga japo hujaimalizia.
 
Mtunzi mzuri lakini nimekukubali ila mimi nakuwaga mvivu wa kusoma hizi riwaya za mapenzi
 
Mtunzi mzuri lakini nimekukubali ila mimi nakuwaga mvivu wa kusoma hizi riwaya za mapenzi

Guys, nilitamani mjifunze kwa yale yaliyonikuta, but it seems mmeigeuza kuwa riwaya ....
Let me find a way of dropping hii mada!
 
Kwani ukiingia choo cha kike utashindwa kukojoa?

Mwanamke akiingia choo cha kiume ndo atateseka kwani sinki la kukojolea lipo juu.
 
Kichwa cha habari kinaonyesha mwisho haukuwa wa heri pole zako.

FirstLady1, mmekuwa siyo wavumilivu wa kusubiri niwapashe yale niliyotaka kuwapasha. Inaonekana mmetanguliza mawazo yenu zaidi kuliko ukweli ya yaliyonikuta. hivyo nimeghahiri kuendelea kuwa hiki kisa ambacho kimsingi kingewapa mambo machache ya kujifunza!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom