Nimeibiwa milioni 5 nilizokuwa naficha ndani, naishi na mke wangu kwenye nyumba ya familia

xenon

Senior Member
Nov 17, 2016
130
79
Mimi ni kijana ambae nimeoa hivi karibuni na nilikua na akiba yangu kama milion5, imepotea katika mazingira ya kutatanisha yaani siioni tena nilipoieka na chumbani nakaa mimi na mkewangu tu ila nakaa kwenye nyumba ya familia, sasa nimechanganyikiwa sijui nini cha kufanya maana ndo ilikua akiba yangu yote, yani mpaka nawaza kama kuna tv asilia popote niende nimjue mwizi wangu.

Msaada tafadhali wakuu
 
Mkeo atakuwa alikuwa anakuomba mtaji ukawa unamnyima hivyo ameamua 'kuziamisha' na kwenda kuzizungusha ipo siku atakurudishia na Riba juu.
 
Nishapatwa na majanga nikakosa hata nguvu za kufanya kazi tena, ila baadae nikanyanyuka na kuendelea,

fanya kazi utapata nyingine, kuna wanaopatwa na majanga makubwa kuliko hayo so let it go, mambo ya kwenda kwa mganga utazidi ku complicate zaidi

Sema ulikuwa mzembe kufivha pesa nyingi kama hizo kwenye nyumba wakati kwenye simu unaweza ukaweka hadi milioni tano
 
Mimi ni kijana ambae nimeoa hivi karibuni na nilikua na akiba yangu kama milioni 5 imepotea katika mazingira ya kutatanisha yaani siioni tena nilipoieka na chumbani nakaa mimi na mke wangu tu ila nakaa kwenye nyumba ya familia.
sasa nimechanganyikiwa sijui nini cha kufanya maana ndo ilikua akiba yangu yote ;yani mpaka nawaza kama kuna tv asilia popote niende nimjue mwizi wangu .....msaada tafadhali wakuu
Nitakufanyia NDUMBA,aliechukua atarudisha haraka kwa maimivu yasiosikia dawa yoyote hapa duniani,ila utalipia ada kidogo tu yaani laki tano tu,kama uko tayari njoo PM.
 
Sio zile hela za michango kweli ambazo hukuziwasilisha kwenye kamati ya harusi yako
 
Pole siku nyingine weka bank usikae na hela nyingi hivo ndani
Hivi milioni tano ni pesa nyingi?.Ama kweli Magu kabana faranga.
Nishapatwa na majanga nikakosa hata nguvu za kufanya kazi tena, ila baadae nikanyanyuka na kuendelea,

fanya kazi utapata nyingine, kuna wanaopatwa na majanga makubwa kuliko hayo so let it go, mambo ya kwenda kwa mganga utazidi ku complicate zaidi

Sema ulikuwa mzembe kufivha pesa nyingi kama hizo kwenye nyumba wakati kwenye simu unaweza ukaweka hadi milioni tano
Na simu ikiibiwa je?
 
Kuhusu mganga potezea iyo ela ya kumpa mganga tumia kama wiki hivi kulewea itakusaidia kupoteza mawazo ila mganga ataongeza stress
 
Inategemea na mtu, mwingine kwake sio nyingi, ila mtoa mada kasema ni nyingi kwake so ni nyingi, kwenye simu haiwezi kuibiwa hata ikipotea una recover line pamoja na fedha
Mrembo bora umenielewesha vizuri,maana sisi wengine tulikimbia shule tukaenda kucheza gololi,mimi nilifikiri unazificha ndani ya simu zile za kizamani za kukoroga.
 
Back
Top Bottom