Nimegundua kwanini wanaJF huitana "Mkuu"

Habarini wakuu!

Kama ilivyo kawaida yetu humu ndani tumezoea sana kuitana WAKUU bila kujali unayemwita ni kweli ni Mkuu au la!
Humu ndani kuna wazee na wajukuu zao, wazazi na watoto wao, watu waliotalakiana, wenye vyeti feki na halali, misukule na watu timamu: Lakini utamaduni wetu ni huu wa kuitana MKUU.

Nimegundua Kwanin tunalitumia sana neno MKUU;
Kwanza, humu ndani wengi tunatumia ID na AVATAR feki hivyo kila mmoja ana HOFU na mwenzake. Kuchati na mtu usiyemfahamu kunahitaji Busara yaweza kuwa unacomment thread ya babu yako, au mama au boss wako kazini Ndiyo maana wengi tunatumia neno MKUU.

Pili nadhani wengi wetu tunatumia MKUU ili tusitukanwe, wengi humu ukiwaquote na kucomment vibaya wanarudisha majibu ambayo yatakuharibia Siku na mood ya kufanya kazi itaisha.

Tatu, wengi wakianzisha Uzi hasa unaohitaji mchango wa mawazo, hutumia sana WAKUU ili kuvuta watu watiririke nondo za maana na kwakuwa tumeshavimbishwa bichwa kwa kuitwa wakuu, wengi tunauvaa uhusika wa UKUU ipasavyo.

Haya WAKUU, Mimi nimegundua hayo, ongeza na lako kama lipo.
Mkuu Ramea hoja kuu ya kutumia neno mkuu ni kubalance gender, ID tutumiazo hazitofautishi KE na ME, so ili uwe katikati watakiwa kutumia neno MKUU, kwa kufanya hivyo unaepuka kaka kumuita dada, dada kumuita kaka!!
Umeelewa mkuu??
 
Habarini wakuu!

Kama ilivyo kawaida yetu humu ndani tumezoea sana kuitana WAKUU bila kujali unayemwita ni kweli ni Mkuu au la!
Humu ndani kuna wazee na wajukuu zao, wazazi na watoto wao, watu waliotalakiana, wenye vyeti feki na halali, misukule na watu timamu: Lakini utamaduni wetu ni huu wa kuitana MKUU.

Nimegundua Kwanin tunalitumia sana neno MKUU;
Kwanza, humu ndani wengi tunatumia ID na AVATAR feki hivyo kila mmoja ana HOFU na mwenzake. Kuchati na mtu usiyemfahamu kunahitaji Busara yaweza kuwa unacomment thread ya babu yako, au mama au boss wako kazini Ndiyo maana wengi tunatumia neno MKUU.

Pili nadhani wengi wetu tunatumia MKUU ili tusitukanwe, wengi humu ukiwaquote na kucomment vibaya wanarudisha majibu ambayo yatakuharibia Siku na mood ya kufanya kazi itaisha.

Tatu, wengi wakianzisha Uzi hasa unaohitaji mchango wa mawazo, hutumia sana WAKUU ili kuvuta watu watiririke nondo za maana na kwakuwa tumeshavimbishwa bichwa kwa kuitwa wakuu, wengi tunauvaa uhusika wa UKUU ipasavyo.

Haya WAKUU, Mimi nimegundua hayo, ongeza na lako kama lipo.
Na wewe pia unatumia ID na AVATAR fake kumbe?
 
Uko sawa mkuu,ila si unajua binadamu yoyote ukianza kumpa sifa kwanza ndo ueleze shida wanakuaga wepesi kujali,mfano makazini uku wadada wakiwa na shida utasikia mpenzi juma njo unisaidie apa?upotezi mda kidume umefika

Siku tupange tuonane live tufahamiane hapo tutaacha kuitana wakuu wengine watoto wa sekondari humu tunawaita wakuu siku hiyoutashangaa kamtu kafupi kama tausi wa bongo muvi ulikuwa unakaita mkuu
 
Pia neno mkuu halichagui jinsia kutokana na wengi wetu kutojulikana jinsia, umri wala kwa majina mkuu ni neno la busara na hupunguza mihemko isiyo ya lazima pale ikitokea kupishana kauli
 
Nikuite mkuu wakati avator yako ni nguruwe...so niite nguruwe mkuu..pambaafu..sijanyi huo ujinga
Bora niite mkuu pic ya mtoto
 
Mimi nina kawaida moja kubwa humu na nje, sijibu tusi kwa tusi, iwe barabarani, kwenye daladala, sokoni, JF au mahali popote pale, ukinitukana natabasamu tu halafu naendelea na mishe zangu au nakujibu asante.

Hapo hata siku moja siyo rahisi mtu kuniharibia siku kwa maneno.

Hujakutana na vichwa mbovu kama rubii
 
Back
Top Bottom