Aah basi Tu nimejikinai nishaona hakuna dalili za kutoboa nimeridhikiwa nimeona niishie level hii hii inanitosha.mahitaji ya msingi ni malazi,mavazi na chakula mengine sitaki tutawasindikiza ndotoni usiku.
Maana nimeona wananipa pressure wanadamu kwamba ooh unakunywa pombe huwezi kutajirika sasa Mimi nimechoka makelele hayo nataka niwe huru yaani nisiutake sasa huo utajiri kwa maana dunia haiwezi kubadilika chochote Mimi nisipofanikiwa kumiliki millions.
Ungekuwa nao, ungeutaka zaidi na zaidi, huku along the way, ukijikuta uki abuse huo utajiri kwa kuwatesa wanadamu wenzako. Unajikuta ukija kufa tu, ndani ya mwaka mmoja, mali zote zimetapanywa na dunia haikukumbuki tena.