Nimefurahishwa na polisi wa Burundi

Nimefurahishwa na polisi wa Burundi

pocha2

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2014
Posts
890
Reaction score
396
Hamna virungu, ngumi, makofi, kurushwa kichura (kiflog), risasi na zaidi mabomu ya machozi ni kwa mbali saana! Wanajitahidi kuzuia maandamano kwa style ya Ulayani au Marekanini!

Nawapongeza sana kwa ustaarabu wao sijui wamejifunzia wapi, sehemu zingine miguu ingevunjika, n.k.

Nadhani mnajua ninachokisema wadau.
 
So far warundi 16 wamekufa kwenye hizi vurugu. tueleze walikufaje
 
Tena jana ITV taarifa ya habari nimeona afande wa kike akichezea kichapo cha nguvu kutoka kwa wananchi

attachment.php
 
Namimi nimeona clueless Membe akisema atakwenda Burundi. Sijui watasuluhishaje bila kumuambia dogo aache kugombea ?
 
So far warundi 16 wamekufa kwenye hizi vurugu. tueleze walikufaje

Idadi hiyo ni kubwa, ila kwa kweli polisi wa burundi wanajitahidi sana kutotumia nguvu nyingi sana, kama wangekuwa ni hawa wa kwetu tungekuwa tunaongelea mamia ya vifo, hapa watu wanaandamana tu kuhusu jambo dogo tu wanauawa watatu, sembuse kumkataa Rais???? na hata mwanzoni mwa maandamano kuliibuka tuhuma kuwa wanajeshi walikuwa wana wazuia polisi kuwaua raia.
 
naona kwa column ya watu 16 huyu dogo nkurunziza ameshagonga mlango wa ocampo the Hague! Haiwezekani unakuwa rais unashindwa kutoa matamshi ya kuzuia haya yasitokee kisa unatamani madaraka??
 
Wewe mtoa mada si Mtanzania. Lengo ni kuisema TZ ukumbuke waandamaji wa TZ hupewa viroba ili walete vujo na kuiba mali za watu.
 
Fujo ziko mjini tu, ila Kuna sehemu Bunjumbura panaitwa Buyenzi fujo huwa hazitokeagi.
 
wakimataifa Utanzania wangu hauna shaka mkuu, haya maandamano yalete hapa Dar halafu ukahesabu majeruhi bila kusikiliza taarifa ya maalumu. Tukubali matukio ya vipigo hayapo au hayaoneshwi kwenye luninga,.

Brutality ya hawa wakwetu saa zingine mtu unajiuliza kwa nini? Ubinadamu zero. Ukweli ndiyo huo.
 
Last edited by a moderator:
Hakuna fujo Burundi, ni misunderstanding kidogo tu iliyopo.
 
Sehemu kubwa ya askari unaowaona ni watusi hawana la kufanya kwa sababu ni kazi ila mioyoni hawako tayari kutumia nguvu dhidi ya watusi wenzao ambao ndiyo wanaompinga Nkurunzinza.
 
Sehemu kubwa ya askari unaowaona ni watusi hawana la kufanya kwa sababu ni kazi ila mioyoni hawako tayari kutumia nguvu dhidi ya watusi wenzao ambao ndiyo wanaompinga Nkurunzinza.
huo ndiyo ukweli
 
Namimi nimeona clueless Membe akisema atakwenda Burundi. Sijui watasuluhishaje bila kumuambia dogo aache kugombea ?

Wanapoteza muda wao tu.. Nkurunzinza na wagombea wengine 7 wameahapelek fomu tume ya uchaguZi na uchaguzi upo kama kawa
 
Lazima useme hivyo nyie si ndo wazee wa maandamano yakitokea na polisi wakirusha mabomu ya machozi hamkosi chochote cha kuiba, hapa tz mtapigwa tuu..!!
 
Askari wa kike akila kichapo toka kwa waraia huko burundi
 
Attachments

  • 1431506914926.jpg
    1431506914926.jpg
    45.7 KB · Views: 930
Namimi nimeona clueless Membe akisema atakwenda Burundi. Sijui watasuluhishaje bila kumuambia dogo aache kugombea ?

mbona walishaenda wakaonana nae na jamaa kagoma msimamo wake upo pale pale anagombea, sasa naona ndio wanakaa tena, kama diplomatic way kagoma basi violence itumike
 
Alishakwenda na si yeye tu ila pamoja na mawaziri wa Africa mashariki wenye wadhifa kama wa Membe.

Kilichowapeleka ni kutaka kujua msimamo wake na kumuachia maswali 3 kama si 4, anbayo yanalenga mustakabali wa Burundi kwa siku za usoni kutokana na mkataba wa Arusha.

Pamoja na hilo leo viongozi wa jumuiya ya EAC wanakutana na mwenyekiti wao hapa Tanzania kuangalia nini kifanyike dhidi ya huyo jamaa nkurunzinza.
Namimi nimeona clueless Membe akisema atakwenda Burundi. Sijui watasuluhishaje bila kumuambia dogo aache kugombea ?
 
Back
Top Bottom