Airmanula
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 3,758
- 5,249
Kati ya mambo ambayo yalitia giza serikali ya awamu iliyopita ya tano ambayo hadi leo ni uchungu mkubwa kwa waliokumbwa na uonevu huo ni hili la wafanyabiashara wa mkoa wa Arusha wa maduka ya kubadilishia fedha za kigeni
Haitosahaulika hii siku ambayo ilileta maumivu makubwa kwa wafanyabiashara hao ambao walinyang'anywa fedha zao zote na maduka kufungwa kwa kile kinachodaiwa kua ETI kufadhili makundi ya kigaidi, kutakatisha fedha na sababu zingine lukuki ambazo hazikua na kichwa wala miguu kwasababu wafanya biashara hao walikua wanafanya biashara hizo kihalali kabisa na kufuata sheria zote.
Tunajiuliza zile pesa zilienda wapi? Zilichukuliwa na kupelekwa wapi au kwa nani na kwa sababu zipi? Suala hili tunashukuru limejadiliwa bungeni na nina imani serikali hii ya furaha ya awamu ya sita italitafutia ufumbuzi suala hili ambalo bado limewaweka wafanyabiashara hawa GIZANI bila kujua hatma yao na hatma za fedha zao zilizochukuliwa KIMABAVU.