Nimefuatilia ziara ya waziri Gwajima mikoani, kiukweli madudu ni mengi. Yule Ummy alikuwa anapiga siasa tu!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,150
Kila eneo analopita waziri wa afya Dkt. Gwajima katika ziara zake mikoani ni vilio tu, wananchi wanalalamikia Huduma hafifu, uhaba wa dawa nk.

Kiukweli hii wizara ina madudu mengi sana na sielewi waziri aliyetangulia Da Ummy Mwalimu na wasaidizi wake walikuwa wanafanya kazi gani!?

Chapa kazi Dr Gwajima wananchi tuko nyuma yako.

Maendeleo hayana vyama!
 
Huenda wewe ndie Gwajima au mtu wake wa karibu mno!

Ummy alifanya makubwa sana ktk sekta ya afya.

Huyu gwajima naona yupo kama yule kaka yake, ni mswahili mno, maneno ya umbea kwa sana na hupenda sana kujilinganisha na mtangulizi wake tena kwa kuponda badala ya kufanya kazi.
 
Hata Kikwete alipotoka tulisikia mengi yakiwamo kusaini mikataba ambayo hata mwenda wazimu asinge saini.

Tuombe Mungu CoviD atunusuru. Bila shaka tutasikia mengi kuhusu chattle na hata zile 1.5Tr baada ya jiwe.

Labda tu kama ana mpango wa kufuata nyayo za nduguye Mr. quarter pin.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Pana rojo la CoviD awamu ya pili. Kwa jinsi walivyo likoroga haya sasa ni maandalizi ya kuwasafisha kwa JICK kuelekea kwenye mpambano ngumu kuliko wa wakati wa Ummy.

Ambao kwa hali ilivyo ni aidha watumbuliwe au wabebwe kwa mbeleko za chuma kweli kweli kuweza kufafanua lolote kwa upande wa jiwe na serikali.

Huu ndiyo mwanzo wa propaganda wenyewe.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Kila eneo analopita waziri wa afya Dr Gwajima katika ziara zake mikoani ni vilio tu, wananchi wanalalamikia Huduma hafifu, uhaba wa dawa nk...
Huo uhaba wa dawa una zaidi ya miaka sasa. Hivi wafahamu pamoja na Serikali kujinasibu kuongeza bajeti ya dawa lakini kiuhalisia hiyo bajeti haitoki? Hivi unafahamu kwa zaidi ya miaka 2 Serikali haikupeleka pesa ya kununua dawa kutoka Hazina kwenda kwenye Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali? Hizo dawa zingenunuliwa kwa pesa ipi?

Hivi wafahamu pesa za Mfuko wa Afya (Health Sector Basket Fund) hazikupelekwa Halmashauri almost mwaka wote wa 2020? Wadhani uendeshaji wa Idara ya Afya katika mila Halmashauri ya Wilaya (CHMT) na Sekretatieti za Mikoa ( RHMT) ulikuwaje?

Serikali itimize wajibu wake wa Msingi wa kuhakikisha MSD Kuna dawa za kutosha na pesa kwenye Vituo ziwepo za kutosha Kama utaona hivyo vilio
 
Kila eneo analopita waziri wa afya Dr Gwajima katika ziara zake mikoani ni vilio tu, wananchi wanalalamikia Huduma hafifu, uhaba wa dawa nk....nk

Kiukweli hii wizara ina madudu mengi sana na sielewi waziri aliyetangulia Da Ummy Mwalimu na wasaidizi wake walikuwa wanafanya kazi gani!?

Chapa kazi Dr Gwajima wananchi tuko nyuma yako.

Maendeleo hayana vyama!
Sasa Ummy Mwalimu angetoa hela yake kununua madawa kaka angu
 
Back
Top Bottom