Nimefuatilia uchaguzi wa Zambia kumbe Wapinzani ni Watu na siyo vyama vya siasa, CHADEMA mna cha kujifunza

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,937
141,908
Kumbe hii dhana ya " vyama vya upinzani " siyo sahihi kwa sababu Wapinzani ni watu siyo vyama. Upinzani uko ndani ya mtu mmoja mmoja na kwa maana hiyo hauwezi kufa hata kama vyama vitakufa.

Kumbe ndio maana CCM siyo chama cha upinzani lakini kina wapinzani wengi tu ndani yake.

Kumbe hata msajili wa vyama vya siasa akiifuta Chadema atakuwa hajafanya jambo kubwa kwa sababu hata CUF ilipodhoofishwa watu wale wale ndio wameunda serikali Zanzibar wakisaidiana na CCM, Hakika wapinzani ni watu siyo ACT wazalendo.

Uchaguzi wa Zambia umenifunza mengi, kule wanachagua mtu wa kuleta maendeleo siyo chama.

Mungu ni mwema wakati wote!
 
Back
Top Bottom