Nilianza safari ya Youtube mwaka mmoja uliopita. Wiki iliyo pita nimefikisha 4000+ watch hours na subscribers zaidi ya 1000!
Mpaka nakua monetized nlikua na jumla ya public videos 44 zenye wastani wa dakika 20 (kuna nyingine zina 8min nyingine 1hr)!
Mambo niliyo jifunza.
1. Quality, informative content is KEY! ni bora utengeneze na ku upload video moja yenye ubora kwa wiki kuliko ku upload video saba kwa wiki zisizo na ubora.
2. Usitumie watu meseji kwenye mitandao ya jamii/watsapp na kuomba wasubscibe. Kutafuta viewers sio jukumu lako ni jukumu la Youtube kupitia recommendation!
3. Tittles ni kitu cha muhimu. Hapa simaanishi uandike "clickbait" tittles... fanya SEO then andaa title iliyo human friendly!
4. Thumbnail ni muhimu sana. Ukiwa na clicm through rate ndogo na thumbnail mbovu jua kabisa video yako haiendi mahali!
5. Viewers Retention ni muhimu sana kuhakikisha video yako ina rank! Unaweza kuwa na title nzuri, thumbnail nzuri ila ukiwa retention ndogo video yako haifiki mahali!
NB 1: Sijaitaja SEO japo ni ya muhimu sana lakini hata usipo jaza keywords kwenye description na title na video yako ikawa na clickthrough rate nzuri, thumbnail nzuri na retention ya viewers nzuri jua kabisa its just a matter of time before youtube haijaanza ku recommend video yako kwa viewers wengi zaidi!!
NB 2: Natumia English japo ya kuunga unga ila naeleweka!! Niliamua kutumia english maana nlitaka kufikia viewers wengi zaidi na sio hapa Tz tu.
NB 3: Viewers wangu wengi kwa siku 28 zilizo pita ni kutoka India, USA, Ethiopia, Turkey na Philipines!
Yangu ni hayo!! Tuendelee kupambana.
View attachment 2106169View attachment 2106170