Nimefeli chuo, naomba ushauri

mills93

Member
May 26, 2016
60
53
Mimi ni kijana wa miaka 25. Ninapitia wakati mgumu sana kwa sasa. Nilikuwa mwanafunzi wa chuo lakini imetokea nimedisco chuo.

Nahitaji ushauri wa nini nifanye maana naona kama nimevurugwa kwa hili jambo na sijui nifanye nini ili maisha yaendelee.

Its like chuo was my only stand and now it has fallen.

Michango ya Wadau:
Hapana sio personal mkuu,Unajua Kuna kozi hata kama umedisco bado unaweza pata fursa,na pia kuna vyuo ambavyo hata kama umedisco unaweza pata fursa na kuna mwaka wa masomo ambao hata kama umedisco unaweza kupata fursa.Kumbuka Kudisco hakumaanishi kwamba wewe ni kilaza bala ni mambo ya kawaida katika maisha ambapo mlango mmoja unajifunga ili mlango mwingine ufunguke.

Ushauri wowote ambao mtu atakupa inategemea na mazingira uliyopo,hali yako ya kiuchumi/kipato na malengo yako kwani hivi ni vitu ambavyo lazima wewe mwenyewe uvitambuea na kuvikubali kabla ya kuweza kupokea ushauri au msaada kutoka kwa mtu mwingine.

Usipokubaliana na uhalisia wako ni vigumu sana kuubadlisha na kuutumia kwa faida zaidi.So it is not personal Nilitaka kukusaidia katika eneo hilo la "Tambua na kubaliana na hali yako halisi kabla ya kutafuta msaada au ushauri ili uweze kusonga mbele"

All the Best in Life
========
MAISHA BILA DEGREE YANAWEZEKANA

Mimi siku disco ila nilikosaga Ada tu , na nilikua na GPA ya kufa pipo nadhani hata nilio waacha chuoni waliitamani

Nikaona hata nikiomba watu wanichangie ninaweza kweli kufanikisha kulipa Ada lakini maisha yangelikuwaje baada ya kulipa Ada ?

Nikaona nitafeli kwa mawazo nika postpone kisha nikafanya mishe zingine nashukuru wanachuo wenzàngu wale wamekua ndiyo wateja Wa biashara zangu

Na Nina mpango Wa kuwaajiri baadhi wakimaliza huo uinjinia mwakani

Never give up
Life begins at 40
It's never too late

NEVER GIVE UP THE GANJA
========
Mimi binafsi natoa ushauri wa kuendelea mbele ili upate degree yako kihalali na kwa ufasaha upya. Kama una vyeti vya form four au vya form six kati ya hivi viwili na unaufaulu wa alama hata D zaidi ya masomo matatu, njoo Open University uanze program ya Foundation mwaka mmoja alafu ujipange upate GPA nzuri kwani ujachelewa na mwakani uanze kusoma degree ya unachotaka kujifunza na Open ukiwa unasoma degree na hauna mambo mengi hata miaka miwili unatoka unaweza kuwaacha hata waliokutangulia. Natanguliza pole na ukakamavu kijana. Amka upambane tena, nafasi zipo.

Kama upo Dar es Salaam fika Kinondoni Biafra utakuta ofisi za chuo kwa maelezo zaidi, Ilala wapo jengo la elimu ya watu wazima floor ya pili karibia na maktaba ya Taifa, na pia mikoani wapo karibia mikoa yote ulizia ofisi za tawi chuo kikuu huria cha Tanzania au Open University of Tanzania utaelekezwa, vingine unaweza google online unaweza kuApply mda wowote. Tembelea wovuti yao www.out.ac.tz
 
Tuanze

Umefeli kozi gani, Chuo gani, Mwaka wa Ngapi? Uko wapi na unafanya nini kwa sasa?
 
hzo ni personal issue! kwa maelezo ya maswali yako njoo dm..
Hapana sio personal mkuu,Unajua Kuna kozi hata kama umedisco bado unaweza pata fursa,na pia kuna vyuo ambavyo hata kama umedisco unaweza pata fursa na kuna mwaka wa masomo ambao hata kama umedisco unaweza kupata fursa.Kumbuka Kudisco hakumaanishi kwamba wewe ni kilaza bala ni mambo ya kawaida katika maisha ambapo mlango mmoja unajifunga ili mlango mwingine ufunguke.

Ushauri wowote ambao mtu atakupa inategemea na mazingira uliyopo,hali yako ya kiuchumi/kipato na malengo yako kwani hivi ni vitu ambavyo lazima wewe mwenyewe uvitambuea na kuvikubali kabla ya kuweza kupokea ushauri au msaada kutoka kwa mtu mwingine.

Usipokubaliana na uhalisia wako ni vigumu sana kuubadlisha na kuutumia kwa faida zaidi.So it is not personal Nilitaka kukusaidia katika eneo hilo la "Tambua na kubaliana na hali yako halisi kabla ya kutafuta msaada au ushauri ili uweze kusonga mbele"

All the Best in Life
 
Pole, lakini
1. sababu za kudisco wewe wazijua
2. baada ya kudisco tayari kuna kitu wafikiria
3. usikkate tamaa trhink something positive
4 usijilaumu na past history ya kudisco badala yake iwe chachu ya wewe kubadilika for better things
 
thank you very much brother
 
Kijana hutakiwi kuhofu sbb umedisco Huku kitaa asilimia kubwa hatuishi kwa kutumua elimu ya chuo kila mtu anapambana kivyake ili kufanikiwa matajir wengi huku mtaan elimu yao IPO ya kawaida au ya chini sana
 
MAISHA BILA DEGREE YANAWEZEKANA

Mimi siku disco ila nilikosaga Ada tu , na nilikua na GPA ya kufa pipo nadhani hata nilio waacha chuoni waliitamani

Nikaona hata nikiomba watu wanichangie ninaweza kweli kufanikisha kulipa Ada lakini maisha yangelikuwaje baada ya kulipa Ada ?

Nikaona nitafeli kwa mawazo nika postpone kisha nikafanya mishe zingine nashukuru wanachuo wenzàngu wale wamekua ndiyo wateja Wa biashara zangu

Na Nina mpango Wa kuwaajiri baadhi wakimaliza huo uinjinia mwakani

Never give up
Life begins at 40
It's never too late

NEVER GIVE UP THE GANJA
 
Usiogope, hiyo ni hatua ya kwanza ya mafanikio yako. Trust me wapo waliomaliza na wana mavyeti yao mtaani mwaka wa saba sasa hawajajiajiri wala kuajiriwa. Wanaishia kujitolea tu. Pambana usifeli maisha.
 
Back
Top Bottom