Uchaguzi 2020 Nimefanikiwa kushawishi ndugu zangu kumpigia kura Tundu Lissu

kikiboxer

JF-Expert Member
Dec 22, 2017
3,076
8,131
Salaam,

Kama kichwa cha habari kisemavyo hapo juu binafsi nimefanikiwa kuwashawishi watu kadhaa kuongeza ushindi kwa Tundu Lisu.
Nilianza na mke wangu ambae yeye kajiandikisha hapo kiwalani nikamweleza ameelewa na kuahidi atampigia kura.

Nikarudi kwa mama mdogo wangu huyu yeye alikuwa na biashara nzuri tu kipindi cha mkwere akajenga na kajumba na kufanya mambo kadhaa yeye mwenyewe ila wakati huu biashara hakuna na huwa anaomba nimpige tafu kwenye ada ya mwanae mmoja yeye nimemwambia unaona tofauti ya awamu iliyopo na ile ya mwanzo kasema ndio mwanangu nakusikiliza wewe.

Nikarudi kwa mama wakwe zangu wawili huwa wananipiga vizinga mara kwa mara na wao nimewaambia msipopiga kura kwa Tundu tusijuane wameelewa nao.

Mama yangu yeye hana noma kabisa nataka kumalizia kwa wadogo zangu wawili na baba nimalize kazi kwa upande wa ndugu.

Lengo la kuleta huu uzi ni kuwapa moyo vijana wenzangu tuwashawishi wanaotuzunguka na ccm waache kutubeza kwamba tunashinda mitandaoni huku sisi sio wapiga kura na hatuna ushawishi huko vijijini.

Ombi: naomba mniunge mkono wakuu kwa pamoja tutaweza kuangusha CCM.
 
Kwa maneno mengine umewashawishi wapinge maendeleo.

CCM itashinda tuu.
 
Mimi hiyo nimeshaifanya mkuu kitambo tu. Na kwa upande wangu ilikuwa ni ngumu kuwalainisha hawa watu kwa sababu ni wafaidika moja kwa moja kutoka kwenye Chama cha wakata mabuno lakini nimeweza.kuwasomesha..
Mkuu umefanya vyema sana. Watu tulio kwenye mitandao ndio hao hao tunao ushawishi huko vijijini pia. Tuongeze nguvu
 
Mm pia mkuu nikewapigia ndugu, jamaa, marafiki na ukoo wangu wote. Nikawaambia kwamba mkimchagua tena huyu john mtaweka viraka mpk kwenye chui na boksa zenu. Hali itakuwa mbaya Sana. Wamenielewa.

#Ni Yeye2020.
 
Kwani maendeleo ni CCM.
Ccm ni kikundi la wachumia tumbo tu
Wote wanafaidika kwa namna moja au nyingine.
Miaka 60 mmeleta maendeleo gani?
Kwahiyo kwa akili yako tokea tupate uhuru hakuna yaliyobadilika?
 
Bila wasanii
Screenshot_20200926-091125.jpg
 
Yapo lakini maendeleo ni kidogo sana kuliko muda mliotumia kuyaleta hayo maendeleo.
Kifupi spidi yenu ya kobe wacha waje wengine
Maendeleo makubwa ni yapi na yaliyo madogo ni yapi?

Remember Development is "gradual change " ndio maana Dunia huweka Development goals ambazo normally huwa na time intervals
 
Maendeleo makubwa ni yapi na yaliyo madogo ni yapi?

Remember Development is "gradual change " ndio maana Dunia huweka Development goals ambazo normally huwa na time intervals
Madogo ni kama haya tuliyonayo. 60 years watu hawana maji ya kunywa si mijini si vijijini. Hospital hakuna vifaa tiba wala dawa wala staff kuhudumia wagonjwa.

Mnataka miaka mingapi kurekebisha sheria ya watu kuwekwa jela kabla upelelezi hujakamilika?jela zinajaa bure kabisa
Mnataka muda gani kutoa uhuru wa mawazo kwa wananchi?
CCM mnatutania sisi wananchi.
 
Mkuu Mimi pia nimefanikiwa hilo, Mimi na mwenza wangu tayari tulishaweka agano mapemaaaaa kuwa rais ni Lisu, Mzee wangu hana shida yeye haipendi mbogamboga toka moyoni. Bi mkubwa yeye alikuwa mboga mboga ila kwa hali aliyopitia hii miaka mitano hataki hata kuwasikia. Bro wangu na sister wao wanamkubali Lisu sana. Kwaiyo paka hapo Nina uhakika wa kura 5 za Lisu kutoka familia yatu.
 
Back
Top Bottom