Nimedanganya nimeishia kupata mfadhaiko!

Nimedanganya nimeishia kupata mfadhaiko!

Aziz Ki Mayele

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2015
Posts
899
Reaction score
1,955
Nina wiki kama tatu nyumbani kwa wazazi kuwasalimia, hua sipendi kabisa kukutana na watu hasa ndugu walio na maswali mengi ya kama unaoa lini? Hujaoa tuu? Siku hizi unafanya nini? Unaishi wapi nk nk

Kuna jamaa wa rika langu ambae namwita baba kiukoo, hupenda mazungumzo na mimi na pindi anisikiapo nimekuja hachelewi kuja nyumbani kwa wazazi wangu ili tushinde tunapiga stori na kuniulizia ulizia mambo yangu.. Sasa leo asubuhi ikaingia simu mpya, sikupokea lakini iliporudia nikapokea na kisha nikagundua ni yeye akasema anakuja home amesikia nimekuja . Nikamwambia Faza sipo bado niko mkoani nikijua atakatisha mpango wake huo ikizingatiwa anajua ratiba ya wazee wangu na members pale home leo hua wanahudhuria ibadani

Muda sio mrefu nikasikia watu wanaongea nje .. kuchungulia dirishani nikamuona jamaa akiongea na shangazi yangu nisiyetaka kabisa kukutana nae kutoka kijijini, jamaa akimwambia watakua wameenda tuu kanisani, ilibidi nikaushe tuu chumbani kwa kua nishawambia sipo nikiamini wataingia ndani na kupoa sebuleni wawasubirie na nikweli wakafanya hivyo, ghafla jamaa akaaga huku akimwambia shangazi aendelee kuwasubiria.

Baada tuu ya jamaa kuondoka nilianza kisikia vishindo kama mtu anasurvey ndani, nikapiga hesabu za kunyanyuka kwenda kufunga mlango wa chumbani nikahisi anaweza kuniwahi akafungua tukakutana ikawa aibu ya milele, kwa hiyo nikajifanya kulala kama mtu mwenye usingizi mwingi. Kilipita kipindi kidogo cha ukimya kisha nikasikia na simu nje, kumuangalia nikagundua alitoka nje. Nikamshukuru Mungu kwamba hajaniona

Baada ya muda nikawa nawasiliana kwa SMS na kadada kangu ka Mwisho nikakaeleza mchongo mzima ulivyokua, huku nikipanga aje tufanye umafia awahi amzubaishe kwa salamu pale nitokee mlango wa jikoni kisha nisepe nirudi usiku. Tulifanikiwa na nikajipa umwamba kwa umafia.

Usiku nimerudi najifanya kumsalimia shangazi kama watu tuliopotezana lakini namuona kama hayuko sawa, Lahaula kumbe aliingia chumbani pale na kuniona.
 
Huyo shangazi yako ako na kasoro gani hata umkwepe hivyo?

Na hiyo nyumba yenu mkitoka nyote huwa mnaacha milango wazi pasipo kuifunga na kufuli au ufunguo?

Kwa jinsi unaeleza ni kama wamekuja wageni wawili na wageni hao wangeliweza ingia ndani ya nyumba pamoja na kuwa waliamini wenye nyumba wametoka kwenda kanisani...
 
Huyo shangazi yako ako na kasoro gani hata umkwepe hivyo?

Na hiyo nyumba yenu mkitoka nyote huwa mnaacha milango wazi pasipo kuifunga na kufuli au ufunguo?

Kwa jinsi unaeleza ni kama wamekuja wageni wawili na wageni hao wangeliweza ingia ndani ya nyumba pamoja na kuwa waliamini wenye nyumba wametoka kwenda kanisani...
Mkuu milango ilikua wazi kwa kua mimi nilikuwepo.. Ilikua umerudishwa tuu na nilikua nimeingia chumbani mara moja wakati nasikia sauti zao mara ya kwanza na kuchungulia dirishani

Nimegundua pia baada ya Mama kugundua shangazia alianza kupiga survey vyumbani huku akitambua kua hakuna mwenyeji amepata ghadhabu sana akimlaumu mzee kwamba inakuaje nduguyo anafanya haya, dogo kanitaarifu

Najisikia vibaya sana
 
Huyo shangazi yako ako na kasoro gani hata umkwepe hivyo?

Na hiyo nyumba yenu mkitoka nyote huwa mnaacha milango wazi pasipo kuifunga na kufuli au ufunguo?

Kwa jinsi unaeleza ni kama wamekuja wageni wawili na wageni hao wangeliweza ingia ndani ya nyumba pamoja na kuwa waliamini wenye nyumba wametoka kwenda kanisani...
Sio shangazi tuu ninaemkwepa .. Niko hivyo hua nakwepa sana sana watu, Sana Sana
 
Ndugu kapimwe akili mtu anakuambia amesikia umekuja halafu we unakataa unajua uongo mwengine kabla haujadanganya inatakiwa ujue unaemdanganya anajua nini na umdanganye nini..?
Ona tu aibu ulistahili na hapo utakuwa umepata la kujifunza.
 
Nakupongeza sana ulichofanya ni sahihi na hiii

Itakuwa ni funzo watu wanaopenda kufatilia maisha ya watu huyo mtu amekoma kukufatiliaaa
 
Daaah hii post yako kwa ulivyokuwa na tabia mbaya za kukwepa kwepa hadi watu wanaokupenda sana na bado unawadanganya NAHISI HADI HAPA UNAPOANDIKA HUU UZI BADO UNATUDANGANYA HADI SISI
 
hua sipendi kabisa kukutana na watu hasa ndugu walio na maswali mengi ya kama unaoa lini? Hujaoa tuu? Siku hizi unafanya nini? Unaishi wapi nk nk
Chief haya maswali yananikata kise... 😡😡😡
I loathe them to the nth power
 
Katika maisha yetu yakibongo,MTU ukifanikiwa kidogo Tu unaanza kujitenga nanduguzo nakudhani wanakufatilia,huo niuchuro naushamba,nahii hii hutokana nadhana Kua watakuomba misaada au kukuchawia hivyo hutaki nduguzako wajue kinachoendelea ktk maisha yako,lkn,kumbuka hao ndugu umaowakwepa Leo ndio haohao watalia naww kipindi umachishwa kazi,unaumwa haujiwezi,au umefariki,au emepatwa nnachangamoto yeyote ile,tujifunze kuwathamini ndugu zetu maana ndiko tuliko toka tunajuana toka day one,hata kama ndugu akikulilia shida msaidie huwezi jua ndie atakuja kukulelea wanao wakati ww umekata Moto Kwa ajali!!who knows??!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom