Nimechukua likizo sitaki mke wangu ajue

Nimechukua likizo sitaki mke wangu ajue

Wazo zi
Ukae Kigoma two weeks? Utaboreka esp kama unatoka kwenye jiji kubwa kama Dar. Cha kufanya, yeye mtangulize na treni mpaka aje afike Kigoma, two to three days zimekatikia njiani. Then wewe baada ya wiki, book ndege ya Ijumaa usepe then Jumapili unageuza au unageuza J3 na ndege ya asubuhi, wakati huo yeye ushampakiza kwenye treni 😀 where she will spend onother two to three days.[/QUOT Wazo zuri sananana
 
mheshimu mkeo....mwambie ukweli na atakubali....kuwa mwanamume....mwambie habari ya wiki 2 hamna.....kumbuka utafikia hotelini( mwanamume hupaswi kulala ukweni) ni gharama hizo.....so 3days + 2days za usafiri....jitahidi ukawaone wazaa chema chako....
 
Mkuu niachie basi hyo kazi private we deal na mkeo tu
 
Mimi nilimshirikisha mwanamke kila jambo bado nikaonekana mjinga na sina adabu bora kuficha kila kitu akae kama housegirl tuu. Unamwambia mipango yenu yote anaenda kwa wanaume wake kuwaeleza na wanapanga namna ya kunufaika na mipango hiyo wakisha kukuua. Wewe hujawajua wanawake bado...
 
Naam kama mke ni muelewa anaweza akatulia ila sasa anaweza kuja na mahitaji milioni kidogo. Sikajua jamaa anapiga pesa ndefu. Unakumbuka lile gauni nilikwambia, na ile michuchumio na ile pochi pia kuna vitenge nimeviona nataka pia halafu nywele zangu zimechoka nahitaji kwenda salon. Halafu Baba nanihii siku nyingi hujaninunulia gold nahitaji hereni, mkufu na cheni ya kiunoni.😱😱😱😱

Mwe miaka miwili na nusu ya ndoa kuna communication break down! Ingekuwa vyema ungemuelewesha sababu za wewe kutokwenda Kigoma wakati wa likizo.
 
mama yangu aliniambiaga kwamba mkeo sio ndugu yako.. na hata yeye na baba sio ndugu.. ila sisi wanawe ndio ndugu za baba na ndugu za mama pia.

kuna wanawake wa kuwaeleza vitu ila ni wachache sana.. na huyo wa kutaka kukaa kigoma wiki mbili eti mnasalimia tu.. upeo wake ni mdogo

Mimi nilimshirikisha mwanamke kila jambo bado nikaonekana mjinga na sina adabu bora kuficha kila kitu akae kama housegirl tuu. Unamwambia mipango yenu yote anaenda kwa wanaume wake kuwaeleza na wanapanga namna ya kunufaika na mipango hiyo wakisha kukuua. Wewe hujawajua wanawake bado...
 
Naam kama mke ni muelewa anaweza akatulia ila sasa anaweza kuja na mahitaji milioni kidogo. Sikajua jamaa anapiga pesa ndefu. Unakumbuka lile gauni nilikwambia, na ile michuchumio na ile pochi pia kuna vitenge nimeviona nataka pia halafu nywele zangu zimechoka nahitaji kwenda salon. Halafu Baba nanihii siku nyingi hujaninunulia gold nahitaji hereni, mkufu na cheni ya kiunoni.😱😱😱😱
Inamaana hamko compatable mkuu, mkiwa na malengo sawa tena unamwambia kabisa Aspirin kumbuka kuna ada za watoto viatu ninavyo bwana sihitaji kwa sasa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
mama yangu aliniambiaga kwamba mkeo sio ndugu yako.. na hata yeye na baba sio ndugu.. ila sisi wanawe ndio ndugu za baba na ndugu za mama pia.

kuna wanawake wa kuwaeleza vitu ila ni wachache sana.. na huyo wa kutaka kukaa kigoma wiki mbili eti mnasalimia tu.. upeo wake ni mdogo
Mume wangu ananieleza mshahara wake lakini katika hiyo pesa ana mpango wa kufanya A,B na C na mimi huwa ninaelewa kuwa haya ndiyo malengo yetu
 
mama yangu aliniambiaga kwamba mkeo sio ndugu yako.. na hata yeye na baba sio ndugu.. ila sisi wanawe ndio ndugu za baba na ndugu za mama pia.

kuna wanawake wa kuwaeleza vitu ila ni wachache sana.. na huyo wa kutaka kukaa kigoma wiki mbili eti mnasalimia tu.. upeo wake ni mdogo
Dunia ya sasa ilivyo na mambo mengi unakaa mahali wiki mbili unasalimia tuu si kawaida...
 
Ukiona Mwanaume anafanya mambo yake tena Kisirisiri huku akijisifu kuwa ama anamficha au hataki Mke wake ajue ujue huyo ana roho mbaya, dharau, mnafiki, hana heshima, ngumbaru, mpuuzi na wa hovyo hovyo. Hivi kama hawa Wanawake huwa hamtaki wayajue yenu huwa ' mnajitutumua ' nini Kuwaoa? Mwanaume mzuri na a real Gentleman hawezi kumficha lolote Mke wake kama kweli alimpenda Kidhati na ni Mama wa Watoto wake. Kuna muda huwa tunawalaumu Wanawake humu ila Mimi nadhani Sisi Wanaume tunachangia na ni sehemu ya udhaifu ambao tunauona kwa hawa Wanawake. Nimechukia kwasababu umesema unataka kumficha Mkeo ila laiti ungesema unataka kumficha Hawara yako hata Mimi ningekuunga mkono. Heshimuni Wake zenu tafadhali!

Kama kawaida yangu leo GENTAMYCINE ' nimenyoosha ' kwani sitaki ujinga.
unatakiwa uishi nao kwa akili
 
Naam kama mke ni muelewa anaweza akatulia ila sasa anaweza kuja na mahitaji milioni kidogo. Sikajua jamaa anapiga pesa ndefu. Unakumbuka lile gauni nilikwambia, na ile michuchumio na ile pochi pia kuna vitenge nimeviona nataka pia halafu nywele zangu zimechoka nahitaji kwenda salon. Halafu Baba nanihii siku nyingi hujaninunulia gold nahitaji hereni, mkufu na cheni ya kiunoni.😱😱😱😱
Ukiona hivyo amemiss kuhongwa alikozoea kabla ya kuolewa. Usipotekeleza hayo anachepuka utasikia unakula papuchi ya bure tuu. Kasha miss kuhongwa anataka umuhonge...
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ila siyo kuwapuuza, kuwadharau na kutowathamini kama inavyotaka kufanya hiyo ' Njemba ' hapo juu.
Aisee mama unajua kikikusibu ndo unaelewa hizi ndoa za cku hizi ni balaa sana ukiwa unasoma comments za watu ndo utaelewa hali halisi.ila wanawake ni watu wa kuishi nao kwa akili sana
 
Kwahiyo Mimi ni Mama si ndiyo Mkuu? Umenikuta wakati mzuri GENTAMYCINE nimetoka kufanyiwa ' counseling ' ya Kutukuka na Roho Mtakatifu vinginevyo kwa ninavyojua enzi zangu sasa hivi ungekuwa ' umeshayakoga ' sana tu na kujuta kunifahamu.
 
yaani ukakae week 2 ukweni huku unakubali kupishana na Pesa ..aisee hata yesu angeshindwa hilo suala ..
piga kazi mkuu ...utakapoishiwa Pesa na kufilisika hao ndio huwa wakwanza kuleta dharau ndani..mwisho wasiku wanakukimbia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom