Nimechoshwa na distance love naombeni ushauri

Nimechoshwa na distance love naombeni ushauri

Zee la madawa

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2022
Posts
1,728
Reaction score
4,075
Hivi nyie wenzangu ambao mko kwenye distance love mnawezaje aisee yaani siku baada ya siku ndivyo ninavyozidi kuchukia distance love na kumchukia huyu binti bila sababu yoyote ile ila binti inaonesha kunipenda sana ila mimi kadri ya siku ndivyo navyozidi kumchukia na kuchukia hii distance love wakuu nifanyeje?

Nikimpiga chini nahisi nitamuumiza kwasababu yeye ndiye ana struggle sana penzi liendelee kuwepo ila mimi siku baada ya siku nazidi kumchoka wakuu naombeni ushauri nifanyeje?
 
Hali unayopitia mimi naifahamu vzr, tofauti ni kuwa mm ilitokea Kwa my wife wangu...nilichokifanya: nilimshauri aache kazi yake na sasa amejiajiri kwenye biashara ya familia ambayo inamlipa zaidi ya ajira yake..tatizo likaisha, mahusiano ya mbali hayana afya Kwa mustakabali wa familia.
 
Hivi nyie wenzangu ambao mko kwenye distance love mnawezaje aisee yaani siku baada ya siku ndivyo ninavyozidi kuchukia distance love na kumchukia huyu binti bila sababu yoyote ile ila binti inaonesha kunipenda sana ila mimi kadri ya siku ndivyo navyozidi kumchukia na kuchukia hii distance love wakuu nifanyeje?

Nikimpiga chini nahisi nitamuumiza kwasababu yeye ndiye ana struggle sana penzi liendelee kuwepo ila mimi siku baada ya siku nazidi kumchoka wakuu naombeni ushauri nifanyeje?
Hujatueleza huo umbali,hujaeleza muda mnaokutana una space kiasi gani,na je unavikwazo vya kipesa au kiruhusa,basi ukitueleza vizuri tunaweza kukushauri
 
Unajikuta mpweke moyoni na upwiru unakaba 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Taratibu unajikuta kwenye sintofahamu ya kuto kujua kama upo kwenye mapenzi au la!
 
Tafuta mchepuko wako mmoja tulia nae na utengeneze mazingira ajue hauna future nae, warembo hawana shida as long as unamuhonga vitu vya hapa na pale, ukimuacha huyo anayekupenda utakuja kuoa asiyekupenda uanze kupandisha nyuzi hapa jukwaa
 
Hujaeleza vizuri jambo lako tukusaidie sisi tuliopitia jambo hilo lakini Kama huyo mwanamke anakupenda usimwache kwa sababu ya distance r/ship. Kumpata akupandaye kwa dhati nyakati hizi za pesa kwanza ni ngumu. Tena ikibidi umuoe sasa alafu ufuate hatua za kisheria/kikazi/kiutumishi ili uhamie kwa mkeo au yeye akufuate.
 
mfuate au akufuate ulipo mna make love, uache kutuletea ujinga ujinga hapa!! Genye tu hapo ndo zinawatesa
Utoto kabisa analeta! Sa kwanini asimfate huko au amwambie huyo Binti wawatu akuje penye mahali mwamba yuko wa enjoy mahusiano yao... Au huyo dada yuko Sayari ya Mars na mwamba yuko Jupiter?
 
Wanawake wamejaa eneo ulilopo, ya nini kuhangaikia 1000km-distant relationship?

Ni kujichosha na kujiletea stress, maisha yenyewe mafupi haya. Mimi hata Ubungo-Chanika tu siwezi.
 
Wanawake wamejaa eneo ulilopo, ya nini kuhangaikia 1000km-distant relationship?

Ni kujichosha na kujiletea stress, maisha yenyewe mafupi haya. Mimi hata Ubungo-Chanika tu siwezi.
Huwezi kwa ajili ya nauli au
 
Back
Top Bottom