Nimechoka kupendwa!!!

Nimechoka kupendwa!!!

Ungeweka kapicha kako na kahao wadada wanaokupenda ili tufanye upembuzi yakinifu.
 
Mpaka muda huu naandika huu uzi, bado sijajua kwanini mabinti wengi wananipenda hadi inafikia hatua ya kugombaniwa mbele ya mkadamnasi. Labda nianze kwa kukri kwamba mimi sina uwezo wa kiuchumi wwte ule maana mpaka sasa nakula, naoga, nalala nyumbani.

Labda sababu familia yetu ipo vzri, mmmh bado nakataa maana home maisha ya kubangaiza tu hata chuo sikumaliza kwa sababu ya kukosa ada.

Labda mimi ni handsome,...Ila napenyewe nakataa. Mi wa kawaida sana japokuwa ni mrefu, mwembamba na pua kama ya kitusi, na mweusi kama mkaa. Mavazi yangu mitumba, chakula changu ugali kwa miguu na ngozi ya kuku.

Cha ajabu kuna mabinti warembo, wasomi wanaotoka familia za "VIP" hapa mtaani kwetu wananikubali vibaya. Wapo ambao wamekataa kuolewa na watoto wa madon wanakuja kwangu.

Mathalani, kuna binti ( Faith) anafatiliwa na mtoto wa don mkoa mzima amemkataa mbele yangu. Na jamaa ameniomba nimsaidie atanipa mtaji wa 10m. Sikuamini....nikasema Mungu akunyimi vyote.

Basi imebidi nimwambie Faith ili suala....we kumbe nilikosea...maana binti aliwaka sana akampigia simu jamaa na kumtukana sana.

Sasa nimejenga uadui na vijana wengi mtaani. Imagine, hadi wazee baadhi hawanipendi. Juzi namsalimia pastor wangu haitikii..imeniuma sana.

Labda niwatie moyo vijana wenzangu, demu akikutema shukuru Mungu. Huwezi jua anakuepusha na nini mbeleni.

Na pia ni vizuri....

Samahanini mb zinakata muda si mrefu...Ila msijali Faith atanitumia ntaendelea.



Sent using Jamii Forums mobile app
Ndiyo ubadilishe upendwe na wakaka uone pia upande ule..!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chochote ulichobarikiwa na mungu jtaid kukificha ili ujiepushe na shari za walimwengu, kua makini sana mkuu huu ulimwengu si mali yako hivo acha show off...
mi nilikua ka wewe bt nilikutana na majanga nikajifunza kuficha neema ulizopewa na mola wako hapo utaishi kwa amani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom