Nimecheka, nikashangaa na kusikitika sana

Mzee Madoshi

Senior Member
Feb 16, 2011
134
41
Kutoka Raiamwema kwenye kichwa cha habari " Kikwete anusurika, awang'oa wenzake' kuna sentensi zimenichekesha na kunisikitisha sana kwa hawa wanasiasa wetu. Kuna huyu waziri katumwa na wenzake awakilishe maoni yao katika kikao cha NEC kutetea wabunge waruhusiwe kugombea NEC:

“Baada ya Kamati Kuu kumaliza kikao, hawakugundua na walijipanga upya kulikabili suala lao ndani ya NEC kama lingejitokeza. Nako kwenye NEC hawakuliona, walitaraji lingeandikwa wazi wazi. Kule ilikuja tu hoja ya wajumbe wapya wa NEC wafanye kazi zao kama shughuli za muda wote, wakaunga mkono.

Wassira anadaiwa kumuuliza mjumbe mwenzake wa Kamati Kuu na NEC, Abdulrahman Kinana; “Hivi hili suala la wabunge kutogombea u-NEC limefia wapi? Naye Kinana baada ya kucheka akamjibu; “aaah, mbona limeshapitishwa muda mrefu

Mawazo yangu
Sasa kama ameshindwa hata kujitetea mwenyewe na wabunge wenzake, je anawezaje kutetea wananchi wake?, lakini la kushangaza wale wabunge wote waliotaka hoja yao ipite walikuwa wanafikiria nini kumtuma huyu Mzee? Na labda kusikitisha zaidi, kama wanashindwa kuelewa mtego mdogo kiasi hiki uliowekwa na kina Nape, je mtu huyu anawezaje kushughulikia masuala makubwa au mikataba mikubwa ya kitaifa yenye mitego ya kibiashara na kisheria?

Wazungu huwa wanatukana weusi kuwa “If you want to hide something from a Black person, put it in a book.” La huyu bwana limepitiliza huu msemo……..
 
Shida ni kwamba maamuzi hayo yote yanakuja last minute, kwa mtindo wa zimamoto, wao wenyewe hawaelewi imekakaaje!
Uchaguzi wa 2005 wanajua wazi walishindwa, na hivyo wanajaribu kufanywa mabadiliko mengi na kuya'slot yote at one time, matokeo wengi wao hawaelewi kitu!
 
uelewa na watu ulionao ndio watakao kuelewesha au kukupotosha
 
Inawezekana kweli alikuwa kalala huyu ndugu, sasa hawa waliomtuma hawajui kwamba anatabia hiyo ya kusinzia? Hivi huyu Mzee ndio alionekana makini zaidi kwao
 
Shida ni kwamba maamuzi hayo yote yanakuja last minute, kwa mtindo wa zimamoto, wao wenyewe hawaelewi imekakaaje!
Uchaguzi wa 2005 wanajua wazi walishindwa, na hivyo wanajaribu kufanywa mabadiliko mengi na kuya'slot yote at one time, matokeo wengi wao hawaelewi kitu!

Inanikumbusha ile methali isemayo, mfa maji haachi kutapatapa, ila kwa hapa sijui ni yupi anayetapatapa. Je ni hawa kina Wasira na kundi lao, au hawa walioleta mabadiliko na kushinda kuyapitisha
 
kwani kila kinachoandikwa na magazeti ni kweli? Vyombo vya habari haviruhusiwa kuwa ndani ya kikao wanategemea kuokoteza habari nje ya mlango wa jengo mlimofanyika kikao. vilevile, wanaweza kuongeza chumvi kwani na wao ni binadamu.
 
Inawezekana kweli alikuwa kalala huyu ndugu, sasa hawa waliomtuma hawajui kwamba anatabia hiyo ya kusinzia? Hivi huyu Mzee ndio alionekana makini zaidi kwao

Kwa muda mrefu nimefanya utafiti sana kuhusu wabunge kulalalala hovyo bungeni na nimegundua jambo, jamani balaa lililokoko Dodoma siyo mchezo, kazi huwa inafanyika sana usiku kucha pale, machangu wa kumwaga, nymba ndogo zinaamia pale na mambo kibao tu ilimradi uzinzi umefanyika ucku kucha! sasa jamani tutegemee nini? Nchi ya wazinifu hii. :shetani:
 
kwani kila kinachoandikwa na magazeti ni kweli? Vyombo vya habari haviruhusiwa kuwa ndani ya kikao wanategemea kuokoteza habari nje ya mlango wa jengo mlimofanyika kikao. vilevile, wanaweza kuongeza chumvi kwani na wao ni binadamu.

Kama si kweli kuna sheria zinawabana, usifikiri vyombo vya habari niviropokaji kama wanavyovikandia. Elewa kabla ya kusikia itakusaidia kuamua
 
Huyu Wassira mie huwa simmumalizi, ukiangalia sura yake, maswali yake, pamoja na majibu ambayo huwa anatoa wakati mwingine huwa nafikiri kuwa "sura ya usoni hufanana fanana na picha ya akili ya mhusika"
 
Huyu Bwana mkubwa huwa analala mchana, sasa hivi vyao vya usiku wa manane kuna anachoambulia kweli?
 
hiyo ndo ccm na serkali ya JK kila kitu kinaendeshwa kiushikaji ushikaji. Nadhani wabunge walimtuma Wassira kwa vile anonekana yupo karibu na mkulu
 
Mkuu hata mimi nimecheka sana. Hiyo ndiyo reflection ya viongozi tulionao hapa kwetu. Hao ndio aina ya viongozi tunaowatuma nje kwenda kusaini mikataba kwa niaba ya nchi. Hao ndio aina ya viongozi tunaowapa rasrimali za nchi ili wazitunze kwa niaba yetu.
Afadhali wakati wa Chief Mangungo kwa kuwa alikuwa hajui kusoma ila hawa wa sasa wanajua kusoma ila wana kiwi ya macho.
 
Mkuu Mzee Madoshi, umecheka, ukashangaa na kusikitika sana, how? Unawasikitikia Wabunge wa CCM au Mwenyekiti wa CCM aliyeongoza vikao vyote viwili! Hivi haya maneno, kule ilikuja tu hoja ya wajumbe wapya wa NEC wafanye kazi zao kama shughuli za muda wote, wakaunga mkono kwani yalielekezwa kwa wabunge tu au wajumbe wote wa NEC pamoja na Mwenyekiti ambaye pia ni Raisi! Je huo umakini haukutakiwa kwanza kwa wajumbe wa Kamati Kuu ambao yaonekana wamekurupuka bila kutilia maanani kitanzi kilicho mbele yao mambo yatakapofumuka?

Mkuu, hebu tafakari kidogo;

  • Wassira anadaiwa kumuuliza mjumbe mwenzake wa Kamati Kuu na NEC, Abdulrahman Kinana; "Hivi hili suala la wabunge kutogombea u-NEC limefia wapi?
  • Naye Kinana baada ya kucheka anadaiwa kumjibu; "aaah, mbona limeshapitishwa muda mrefu!"

Taswira inayojengeka hapa ni kwamba CCM, kwa maana ya chombo makini, is nothing but a big joke! Kama wanavyochapa usingizi Wabunge wake huko mjengoni, ndivyo hivyo chama kwa ujumla wake kinavyochapa usingizi kwenye vikao vyake. Ndio maana maazimio mengi yanayopitishwa ndani ya hivyo vikao yanawaacha watu makini midomo wazi! Mwenzio Mag3, kusema kweli sikucheka, sikushangaa ila nimefurahia sana walichofanya wajumbe wa NEC! How? hata mimi sijui!
 
Kwa muda mrefu nimefanya utafiti sana kuhusu wabunge kulalalala hovyo bungeni na nimegundua jambo, jamani balaa lililokoko Dodoma siyo mchezo, kazi huwa inafanyika sana usiku kucha pale, machangu wa kumwaga, nymba ndogo zinaamia pale na mambo kibao tu ilimradi uzinzi umefanyika ucku kucha! sasa jamani tutegemee nini? Nchi ya wazinifu hii. :shetani:

Mkuu, umenikumbusha sakata la posho, ndiyo maana walikuwa wanataka posho ziongezwe.
 
Back
Top Bottom