Nimechanganyikiwa, sikujua kama mwisho utakuwa hivi

kaa chini uzungumze na mumeo hamna kinachoshindikana chini ya jua usije ukasiliza maneno ya watu sio wote wanaokupenda jaribu kumshirikisha na Mungu

maana si kila muda unatakiwa uongee na mmeo masuala ya maisha na ndoa panga muda maalumu wa kuongea nae
 
Pole sana dada mpendwa,la msingi msifikie hatua ya kuachana kwani watoto watapata shida tumeyaona haya mtaani wazazi waloachana na jinsi watoto wanavyopata shida,fanya maombi zaidi mbele yake,ikiwezekana funga kwa ajili najua Mungu atakusikiliza kilio chako maana najua hao ni pepo wanamsumbua huyo mkuu najua atabadilika kwani wengi mtaani tumeshuhudia haya ila tu kama ukimtegemea Yesu kristo kua bwana na Mwokozi wako,Mungu akutangulie dada angu mpendwa.
 
Pole dada yangu tambua ya kuwa wakat mwingine maamuzi magumu lazma yachukue nafasi japokuwa yanaumiza
 
Pia wakati unafikiria ufanye uamuzi gani, fikiria kwanza kuhusu magonjwa ya zinaa hasa ukimwi usijeng'ang'ania watoto watalelewa na single parent afu mkajakufa wote na mkawaacha wakitaabika
 
Just to recap;
  • He abuses you, verbally, emotionally and even physicially
  • Hajatulia na Sio muaminifu, to the extent that wewe mwenyewe umeshamfumania more that once
  • He does not provide for the family, nor is he a hard worker. Anakopa, anaspend na wewe ndiye mlipaji?
Ndeonasiae
Maybe I should begin by asking you what exactly does marriage mean to you? Is it something to be tolerated, enjoyed or what? Anyhow I think you should ask for a separation, legal and physical . Have him use this time apart to prove to you, and the family( ie your kids)that he has changed and the so professed changes are sustainable. Achana na misamaha hii na machozi ya mamba , maana if ingekuwa sincere you wouldnt be where you at now! Im sorry to say this but he sounds toxic!. He goes out, messes up and the guilts you into accepting him back, which you do, but a little while later goes out and does the same thing, like a never ending cycle!
 
Just to recap;
  • He abuses you, verbally, emotionally and even physicially
  • Hajatulia na Sio muaminifu, to the extent that wewe mwenyewe umeshamfumania more that once
  • He does not provide for the family, nor is he a hard worker. Anakopa, anaspend na wewe ndiye mlipaji?
Ndeonasiae
Maybe I should begin by asking you what exactly does marriage mean to you? Is it something to be tolerated, enjoyed or what? Anyhow I think you should ask for a separation, legal and physical . Have him use this time apart to prove to you, and the family( ie your kids)that he has changed and the so professed changes are sustainable. Achana na misamaha hii na machozi ya mamba , maana if ingekuwa sincere you wouldnt be where you at now! Im sorry to say this but he sounds toxic!. He goes out, messes up and the guilts you into accepting him back, which you do, but a little while later goes out and does the same thing, like a never ending cycle!

is ur first language english????????
it does sound like that.....
 
is ur first language english????????
it does sound like that.....

The Boss
Yeah right:smiling:!!!!.....................Hamna mwaya, Ila ni kuwa I type faster and more accurately in english. My job consists of a lot of typing kwa kidhungu!
 
The Boss
Yeah right:smiling:!!!!.....................Hamna mwaya, Ila ni kuwa I type faster and more accurately in english. My job consists of a lot of typing kwa kidhungu!

are you in europe now?
were you?
 
me sikushauri uachane naye since mna watoto na wanamhitaji baba yao. bali unahitaji umwonyeshe kwamba u can survive bila yeye. yaani anza kumfungia pazia. ignore kila anachofanya, ishi hapo ndani kama vile yeye hayupo but at the same time mpe respect. usihoji kuingia wala kutoka kwake. piga pamba kali, kula vizuri always tabasamu. akileta biashara za kujaribu kukupiga mpeleke kwenye vyombo vya dola.


I like this comment lol!mdada unauonaje huo ushauri?sometimes watoto watakusumbua ukajuta kwa nini ulimuacha baba yao. Amua kuishi nae mzungu wa nne na usifuatilie mambo yake hayo ni mapito atajirudi na utabaki unahadithia
 
pole sana mpendwa kwa matatizo hayo. nakushauri uachane na huyo mtu mapema iwezekanavyo. sababu umezitoa mwenyewe:
  1. ni muongo
  2. ni tapeli na sio muaminifu
  3. he cheats on you
  4. he abuses you
  5. haskii shauri
  6. hajui kufanya biashara
  7. ameshindwa kuisupport familia yake financialy na hana nia ya kujaribu
  8. anaweka maisha yako hatarini hadi unashindwa kutembelea eneo lake la biashara
  9. anaweka familia hatarini kwa kukopa hovyo anashindwa kulipa, inakubidi utoke outside initial budget yako kulipa deni zake
Sasa uzuri ni:
  1. anawapenda watoto
that is all. faham hata mkiachana watoto ni wake bado na ataendelea kuwapenda. ila ni muhimu uwaprotect from the bad example that he is and to protect yourself from his health hazardous life sitle, from his verbal and emotional avuse, without mentioning the phisical abuse which is in itself enough to leave him
Mpendwa, kumbuka wakati wewe unahishi matatizo hayo kuna watu wanaenjoy mapenzi yao na wanshukuru Mungu kua na mume au mke. hata wewe unaweza kukaribisha furaha maishani mwako. sijui una miaka ngapi ila nahisi bado unaweza kupata mtu Mungu alikuandalia. Mungu anataka uwe happy, na familia yako, na what you have now is not the wonderful plan God has for you.
Move out of there as soon as you can.
 
Ndeonasia, please just let it go, that marriage is broken, he doesn't respect you, he abuses you and you are sticking for the sake of who?

Mimi nakushauri uondoke, usikae kwenye ndoa so u r able to live a 'glorious Tanzanian dream' which is to be married ....

You will always be fighting these other women and u might get diseases...toka sasa hivi whilst u can, if he comes to his senses and wipe his act u can get back...but what u have is just a piece of paper and not marriage

Aonywaye mara nyingi, akishupaza shingo, atavunjika ghafla! Wala hapati dawa...
 
achana nae he was not meant for you, 7 years hajabadilika hatabadilika kamwe, Do not west time for non sense. ni pepo huyo atakuuwa either kwa maladhi au atakupiga akutie ulemavu.
 
Sijui nianzie wapi?? naandika kwa masikitiko makubwa, miaka 7 iliyopita niliolewa na mwenzangu ambaye nilimpenda baada ya urafiki wa miaka kama 5 japo baadhi ya ndugu zangu hawakupenda niolewe nae coz hana kazi na wala hakusoma aliishia std7 na mimi ni graduate, hakuwa mtu wa kujishughulisha na biashara wala kuajiriwa bali mishen town tu, ila mimi nilimsaidia kamtaji sababu nilimpenda sikusikia wala kuona.
Mwenzangu huyu kiukweli kuna watu walikuwa wanasema hajatulia ila binafsi kwa upofu wa mapenzi sikulijali hili, lakini tatizo la shughuli kutokuwa na shughuli maalumu nililiona lakini mwenzangu alisisitiza kuwa hawezi kusoma labda biashara japo hakuonyesha juhudi niliamini angebadilika maisha yakaendelea. mie ni muajiriwa nakipato cha kuweza kuitimizia familia hata peke yangu. Niliingia kwenye ndoa nikiamini akiwa mume na baba angebadilika

Tumeingia kwenye ndoa ndio naanza kuona matatizo mengi hap tuna watoto wawili, si muaminifu kwa pesa za watu wala zangu akiazima basi inabidi nilipe kufunika aibu, ni muongo mara nyingi ni uongo usio na sababu sijui ninini?? yote tisa kumi kesi za wanawake ni kibao na ameshaattempt kuoa mara mbili yeye nikazikamata kwenye mtandao, anakaogonjwa na wanawake wazuri na weupe (hata mimi ni mweupe na mzuri lol) so kila nikimkamata ni ugomvi tu na mwisho anaomba mara msamaha lakini anarudia tena. Biashara nilimuanzishia japo biashara yenyewe alikuja kushindwa akafanya eneo la biashara ndio kituo cha kukutana na wanawake wake mpaka nikawa naogopa kupita hiyo mitaa.

Mbali na yote haya jamaa ni abuser, physically, verbally, and emotionally,, huwa napigwa mie nikijaribu kuargue kuhusu tabia yake au mambo ya ndani, pia ananihisi hisi na anapenda kunicontrol kama mtoto. kuna events nyingi sana nikiandika nitawachosha

Sasa wandugu imefikia kipindi mimi mapenzi yameisha na tunawatoto 2, tumejenga (90% ni mchango wangu), gari (90% mchango wangu) na kulisha familia 90% ni mimi, mapenzi yameisha kabisa sio mchezo sidhani kama yatarudi na ninataka kuachana naye, ndoa tulifunga kanisani, nimejaribu kumwambia nataka tutengane kwa muda analia anaomba nafasi ya mwisho anadia ananipenda na anawapenda watoto wake hawezi kuishi mbali nao ila mimi nahisi anaogopa ukali wa maisha na sio mapenzi kwangu, japo wanae kweli anawapenda sana. Natamani nisiondoke lakini ninavyomjua huwa anaomba msamaha zikipita wiki mbili mwezi vituko vinarudi pale pale so naogopa na umri unakimbia natakiwa niwe na misimamo mapema kwani naona hata kwa malezi ya watoto si vizuri kuwa na baba mwenye sifa ya uongo na utapeli mtaani au watu wanakuja hapo kudai watoto wataadapt hizo tabia. naomba nikiri udhaifu wangu katika kupenda naomba msinirushie sana mawe kwa hilo kwa nimeshajua wapi niliteleza.

Naombeni ushauri utakaonisaidia mimi na watoto wangu, based on your experiences maana naogopa hata kuwaambia ndugu zangu kwani watanichua haraka, wameshajitolea hadi nyumba ya mimi kuishi na wanangu, na vikao vimeshakaliwa vingi na kila siku wananiambia niachane nae lakini mimi nilikuwa kichwa hakijakaa vizuri bado, yani siamini kama nitaishi hivi maisha yangu bila mume coz sipendi wala sifurahishwi na

maisha ya kuwa single parent at my age of 32, na hili ndio linanifanya nifikirie sana kuhusu maamuzi yangu.


Yote tisa, kichapo siyo kizuri sana. Kama ana mkono wa kupiga huyo si mponaji labda amrudie Mungu wake. Chapa lapa akae peke yake kwamza apate akili.

Zaidi ya hapo mshirikishe Mungu, hashindwi na lolote, ni mwaminifu. Jitahidi ufunge kwa maombi ukimaanisha. Anatenda.
 
Pole Ndeonasiae kweli unapitia kipindi kigumu sana lakini kumbuka kile kiapo pale altareni siku ile ya kuwa "utampenda na kumvumilia kwenye shida na raha" naamini hiyo inajumuisha kuvumiliana kwenye "karaha" pia.,nadhani mumeo bado ana nafasi ya kurekebishika.,hebu jaribu kuwahusisha wazee wa kanisa mpendwa.
 
pole sana dada kwa uvumilivu wa kipindi kirefu huwa siku zote dalili ya mvua ni mawingu but huwa wanawake tunapenda sana kujipa mahope ya uwongo ooh mume wangu atabadilika , hata kabla msichana hajaolewa na anajua huyo mwanaume wake ni kimeo eti anakwambia atabadilika kakudanganya nani samaki hukunjwa angali mbichi wanaume wengi ni ngumu sana kubadilika huwa wanaprittend tu .nisiuze sana chai kazi ni moja una kazi nzuri huyo ndo mume wako wa kwanza (swtheart NO 1)sasa achana naye ameshakutia mikosi huyo lea watoto wako kaa karibu na familia yako coz ndo watu wanaojua thamani yako ndio maana hata wanakuonea huruma NA WANATAKA UTOKE HUKO na degree yako yote unambwelabwela tu tena WACHA USHAMBA TUPA KULE utaenjoy kishenzi no stress watoto ndo faraja yako thus all ,however 32 bado mrembo kabisa hachana na hilo kurundungu lililobebwa likashidwa kushikilia hata mabega. shwaaaaaani zakee

Acha ujinga dada sa ulichotoa hapa ni ushauri au ushakunaku na ushambenga? Hajakwambia umtukane mzazi mwenzie we ndo unajfanya kujuua kumbe yawezekana hata mume wa kucngziwa huna!

Cha msingi, kwako dada mtoa maada unachotakiwa kufanya kwanza relax na seek spritual interpretation relating to marriage etqts.
Basically understand dat initially u had hav been bound by LOVE-the reason as to why you married him. But the point is nyie sahz ni mwili+dam 1 so nicngependezwa km sahz ukachukua uamzi wa kuachana na mumeo, cha msingi chekecha mbongo yako na uelewe kuwa the man is frustrated na hata vtendo vyake vya kutoka nje ni kujarbu kujpa relief kimawazo practise ambayo ni negatv ktk ndoa yenu.
Mumeo unamzidi mbali sana c2 kwa elimu bali hata mchango kwa family yenu.
So kaa nae chini na tumia bible kumredrect mumeo kwa lugha ya unyenyekevu na mwambie kuwa yeye ndio chaguo lako na ndo maana Mungu amewabarik mkapata watoto.
Naamini atakucklza tu coz kama uliitii sauti ya kwanza toka moyon yakwamba huyu ndo atakuwa mume wangu kwa misingi ya Kikristo then I argue you plz b patient coz utakuwa umefanya kosa kubwa sana kuachika kwenye ndoa ya awali na ndiyo Mungu aliyoibariki.
Vumilia dada!
 
nitarudi kutoa usahuri baada ya kujua na wewe umemfanyia mangapi mabaya ambayo huenda yakawa yanachangia mvulugano huo maana umeeleza mabaya yote ya mumeo,hebu weka na hayo yako mabaya ili tujue jinsi ya kushauri bila kuegemea upande mmoja kama wengi walivyofanya
asante
 
Back
Top Bottom