Nimechanganyikiwa, sikujua kama mwisho utakuwa hivi

Ndeonasiae

Senior Member
Aug 15, 2011
102
48
Sijui nianzie wapi?? naandika kwa masikitiko makubwa, miaka 7 iliyopita niliolewa na mwenzangu ambaye nilimpenda baada ya urafiki wa miaka kama 5 japo baadhi ya ndugu zangu hawakupenda niolewe nae coz hana kazi na wala hakusoma aliishia std7 na mimi ni graduate, hakuwa mtu wa kujishughulisha na biashara wala kuajiriwa bali mishen town tu, ila mimi nilimsaidia kamtaji sababu nilimpenda sikusikia wala kuona.
Mwenzangu huyu kiukweli kuna watu walikuwa wanasema hajatulia ila binafsi kwa upofu wa mapenzi sikulijali hili, lakini tatizo la shughuli kutokuwa na shughuli maalumu nililiona lakini mwenzangu alisisitiza kuwa hawezi kusoma labda biashara japo hakuonyesha juhudi niliamini angebadilika maisha yakaendelea. mie ni muajiriwa nakipato cha kuweza kuitimizia familia hata peke yangu. Niliingia kwenye ndoa nikiamini akiwa mume na baba angebadilika

Tumeingia kwenye ndoa ndio naanza kuona matatizo mengi hap tuna watoto wawili, si muaminifu kwa pesa za watu wala zangu akiazima basi inabidi nilipe kufunika aibu, ni muongo mara nyingi ni uongo usio na sababu sijui ninini?? yote tisa kumi kesi za wanawake ni kibao na ameshaattempt kuoa mara mbili yeye nikazikamata kwenye mtandao, anakaogonjwa na wanawake wazuri na weupe (hata mimi ni mweupe na mzuri lol) so kila nikimkamata ni ugomvi tu na mwisho anaomba mara msamaha lakini anarudia tena. Biashara nilimuanzishia japo biashara yenyewe alikuja kushindwa akafanya eneo la biashara ndio kituo cha kukutana na wanawake wake mpaka nikawa naogopa kupita hiyo mitaa.

Mbali na yote haya jamaa ni abuser, physically, verbally, and emotionally,, huwa napigwa mie nikijaribu kuargue kuhusu tabia yake au mambo ya ndani, pia ananihisi hisi na anapenda kunicontrol kama mtoto. kuna events nyingi sana nikiandika nitawachosha

Sasa wandugu imefikia kipindi mimi mapenzi yameisha na tunawatoto 2, tumejenga (90% ni mchango wangu), gari (90% mchango wangu) na kulisha familia 90% ni mimi, mapenzi yameisha kabisa sio mchezo sidhani kama yatarudi na ninataka kuachana naye, ndoa tulifunga kanisani, nimejaribu kumwambia nataka tutengane kwa muda analia anaomba nafasi ya mwisho anadia ananipenda na anawapenda watoto wake hawezi kuishi mbali nao ila mimi nahisi anaogopa ukali wa maisha na sio mapenzi kwangu, japo wanae kweli anawapenda sana. Natamani nisiondoke lakini ninavyomjua huwa anaomba msamaha zikipita wiki mbili mwezi vituko vinarudi pale pale so naogopa na umri unakimbia natakiwa niwe na misimamo mapema kwani naona hata kwa malezi ya watoto si vizuri kuwa na baba mwenye sifa ya uongo na utapeli mtaani au watu wanakuja hapo kudai watoto wataadapt hizo tabia. naomba nikiri udhaifu wangu katika kupenda naomba msinirushie sana mawe kwa hilo kwa nimeshajua wapi niliteleza.

Naombeni ushauri utakaonisaidia mimi na watoto wangu, based on your experiences maana naogopa hata kuwaambia ndugu zangu kwani watanichua haraka, wameshajitolea hadi nyumba ya mimi kuishi na wanangu, na vikao vimeshakaliwa vingi na kila siku wananiambia niachane nae lakini mimi nilikuwa kichwa hakijakaa vizuri bado, yani siamini kama nitaishi hivi maisha yangu bila mume coz sipendi wala sifurahishwi na maisha ya kuwa single parent at my age of 32, na hili ndio linanifanya nifikirie sana kuhusu maamuzi yangu.
 

Bronty

Member
Sep 26, 2011
60
38
Pole sana ndeonasi, hayo ni maisha yatapita tu, madam ni mumeo na mmefunga ndoa kanisani hukulazimishwa na mtu huna budi kuvumilia, usione wamama wamekaa kwenye ndoa zao ukaona wanafanya kazi ndogo, wanapitia mapito makubwa zaidi ya hayo,usichoke kumkumbusha mlipotoka nina imani bado mapema anaweza badilika,kama ukiona huwezi kabisa nenda kwa mchungaji aliyewafungisha ndoa mweleze akupe ushauri
 

hayaka

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
474
100
me sikushauri uachane naye since mna watoto na wanamhitaji baba yao. bali unahitaji umwonyeshe kwamba u can survive bila yeye. yaani anza kumfungia pazia. ignore kila anachofanya, ishi hapo ndani kama vile yeye hayupo but at the same time mpe respect. usihoji kuingia wala kutoka kwake. piga pamba kali, kula vizuri always tabasamu. akileta biashara za kujaribu kukupiga mpeleke kwenye vyombo vya dola.
 

BiMkubwa

JF-Expert Member
Jan 9, 2007
529
97
Nimeolewa miaka 16 sasa ila issue yako ngumu. Siwezi kukushauri uachane naye maana sikujui na wala sijui mlipoanzia wala uwezo wako.
Sipendi kurupuka ktk kutoa ushauri pia. Ila uelewe palipo na tatizo suluhisho lipo, binafsi sidhani kama ni baba anayefaa hata kidogo. Inabidi ajirekebishe
 

backer

Member
Dec 22, 2010
86
8
duh,....! Pole sana, a very hard case to judge.humu ndo jamvin natumain utapata ushauri ulio bora kabisa ila tulia sana kwenye maamuzi.
 

MyTz

JF-Expert Member
Sep 20, 2011
333
62
pole mdada...
break up inakuhusu...
bora single parent, kuliko kumvumilia m2 ambaye mwisho wa siku atakuletea maradhi...
kuna vya kuvumilia, sio hili la uzinzi...mtauana kwa magonjwa muache watoto wanateseka, mpige chini fasta uendelee na maisha yako...
 

Ndeonasiae

Senior Member
Aug 15, 2011
102
48
Asanteni kwa michango yenu, tatizo kubwa mapenzi yameisha kabisa na ikumbukwe mapenzi ndio pekee yaliyotuunganisha, mimi simfuatilii tena na hata yeye anajua mapenzi yameisha,, na nataka kuondoka kweli ndani kabisa ya moyo wangu natamani kuondoka ila nikiwaangalia watoto roho inasita! sio yeye ninayemuhurumia bali ni watoto yani simtamani hata kumuona natamani aondoke asafiri aende mbali huko.
 

Mamaa Kigogo

Senior Member
Sep 26, 2011
105
43
pole sana dada kwa uvumilivu wa kipindi kirefu huwa siku zote dalili ya mvua ni mawingu but huwa wanawake tunapenda sana kujipa mahope ya uwongo ooh mume wangu atabadilika , hata kabla msichana hajaolewa na anajua huyo mwanaume wake ni kimeo eti anakwambia atabadilika kakudanganya nani samaki hukunjwa angali mbichi wanaume wengi ni ngumu sana kubadilika huwa wanaprittend tu .nisiuze sana chai kazi ni moja una kazi nzuri huyo ndo mume wako wa kwanza (swtheart NO 1)sasa achana naye ameshakutia mikosi huyo lea watoto wako kaa karibu na familia yako coz ndo watu wanaojua thamani yako ndio maana hata wanakuonea huruma NA WANATAKA UTOKE HUKO na degree yako yote unambwelabwela tu tena WACHA USHAMBA TUPA KULE utaenjoy kishenzi no stress watoto ndo faraja yako thus all ,however 32 bado mrembo kabisa hachana na hilo kurundungu lililobebwa likashidwa kushikilia hata mabega. shwaaaaaani zakee
 

JS

JF-Expert Member
Sep 29, 2009
2,066
494
Ndeo, mimi sina uzoefu na masuala ya ndoa lakini angalau nimeshawahi kushi na watu walioko kwenye ndoa kwa maana ya ndugu jamaa na marafiki. na nilivyojifunza ni kuwa mawasiliano baina yao husuluhisha mgogoro ulioko. sasa kwa case yako inaonekana hata huyo mume hana muda wa kukaa chini na wewe mkasuluhisha matatizo yaliyopo na hii yote ni kwa sababu he is the main actor in the game na wewe ndo victim. nenda kanisani mlikofungia ndoa kwa padre/mchungaji aliyewafungisha mpate ushauri nasaha. kama ni msikitini, nenda kwa sheikh umueleze kilakitu naamini viongozi wa hawa dini watakusaidia. i always beleive kuna kitu kinaweza kufanyika kusave the situation kuliko kubreak up kwani watakaosuffer ni watoto. try all the means and i know you both will walk out of it. vikishindikana basi kuachana ndo iwe ya mwisho kabisa kwenye line ya solutions on the table. goodluck darling......
 

Beautiful Lady

Senior Member
Jun 8, 2011
136
43
Pole sana. katika maisha ya ndoa usitegemee raha tu, kuna shida pia.Jaribu kuwashirikisha viongozi wenu wa kanisani mlikofungia ndoa wanaweza kuwasaidia.pia jifunze kumuombea mumeo.
 

tete'a'tete

JF-Expert Member
Feb 10, 2010
472
62
Pole sana naomba nikuweke kwenye maombi ya hatari na mungu atakuongoza tuuu...si kitu kirahisi kama watu wanavyodhani ila nakushauri sali sana..muombee mumeo yawezekana kuna mambo ya giza yamewazingira...by the way hapa duniani si watu wote watafurahi mlivyo na mme wenu na katika upendo mliokuwa mnao hapa mwanzo...sali sana haya ni mapito tuu...kuachana si solution watoto wataadhirika kisaikologia zaidi...pole sana.. wamama tunakutana na mengi kwenye hizi ndoa...
 

Mamaa Kigogo

Senior Member
Sep 26, 2011
105
43
Asanteni kwa michango yenu, tatizo kubwa mapenzi yameisha kabisa na ikumbukwe mapenzi ndio pekee yaliyotuunganisha, mimi simfuatilii tena na hata yeye anajua mapenzi yameisha,, na nataka kuondoka kweli ndani kabisa ya moyo wangu natamani kuondoka ila nikiwaangalia watoto roho inasita! sio yeye ninayemuhurumia bali ni watoto yani simtamani hata kumuona natamani aondoke asafiri aende mbali huko.

tafuta ujanja peleka watoto boarding kwanza then uanzishe mtiti haukufai kabisaa atakuletea magojwa mpe blak and white kwamba umejua sio mwanaume ni mwanaume suruhali tu .
 

Cantalisia

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
5,223
2,902
My Dia sina uzoefu wa ndoa ila nimeishi na wazazi wangu wenye ndoa huo upupu achana nao,ww bado age yako iko poa, kazi unayo,elimu unayo, na watoto mungu kakupa,huyo hana shukurani kbs mpaka anakupiga sepa mapema ipo siku atakushikia panga au kukuletea ukimwi ufe uache wanao wanapata shida na hilo dude, utaishi vp na mtu usiempenda!
 

Blaki Womani

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
11,237
13,376
pole sana Ndeo..........urafiki wa miaka 5 na ndoa ya 7yrs bado hajaweza kubadilika daahh........sipendi kusema kuachana lakini yanapozidi maamuzi magumu yanafanyika........pia kabla ya kuachana washirikishe wadhamini wa ndoa
 

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
32,740
22,973
jibu unalo. Kama hzo tabia kweli anazo na unawapenda wanao fanya maamuzi magumu uondoke.
Au mpaka akuletee maradhi? Afterall wewe ndo baba na ndo mama wa hyo familia.
Jithamini. Huyo mumeo anapenda fedha zako tu hakuna lolote.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

3 Reactions
Reply
Top Bottom