Nimeamua rasmi kuchukua kadi ya uanachama CHADEMA

Nimeamua rasmi kuchukua kadi ya uanachama CHADEMA

Mangisandy

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2012
Posts
2,644
Reaction score
2,273
Niliwahi kuwa mwanachama wa NCCR-Mageuzi wakati wa mzee Lyatonga lakini tukasambaratika, wengine wakaenda TLP. Mimi nikaachana na uanachama lakini baada ya kuona msimamo wa Mbowe, Lema kukaa mahabusu, risasi za Lissu na sasa sera makini za CHADEMA, natangaza rasmi kwamba kesho napokea kadi ya chama. Nitanunua nguo za chama, na nitazivaa hadharani.

Nitafanya kazi zote za mwanachama, ikiwepo kupiga kampeni, kama sitabughudhiwa! (Mimi ni mtumishi kanisani) kila mtu kuanzia humu jukwaani anitambue hivyo. Kesho naenda kwenye mkutano wa Lissu Arusha kwa nia ya kupokea kadi yangu rasmi. Kama kuna kada au kiongozi ambaye ananisoma hapa na anaona kuna majukumu nitakifaa chama, tupeane signal ili mawasiliano yaanze!
 
Kila la heri mkuu kazi njema,lakini kabla hujaruka mtaro hakikisha unaagana na nyonga
 
Back
Top Bottom