Kwa kipindi cha miezi miwili sasa imepita Tangu Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kutangaza ilichokiita Kujivua Gamba kwa Lengo Si la kuboresha Maisha ya Watanzania bali KUKINUSURU Chama Cha Mapindizi ( Sijui nani kawadanganya kuwa wananchi watalia na kuomboleza siku wakisikia CCM imekufa ).
Moja kati ya Mikakati yao ni kuwaomba ( Wenyewe wanadai kuwataka, lakini huwezi kumtaka mtu ajiuzulu halafu unakaa naye Kikao cha Kumuomba ajiuzulu) wale wote wanatuhumiwa kwa ufisadi uliokichafua Chama Cha Mapinduzi Machoni mwa Watanzania. Lakini CCM hao hao hakuna Mahali wamesema kwamba
1. Ni Lini Lowasa, Chenge na Rostam walituhumiwa kwa ufisadi
2. Ni Wapi Lowasa, Chenge na Rostam walituhumiwa Kwa Ufisadi
3. Ni Nani aliyewatuhumu Lowasa, Rostam na Chenge kwa Ufisadi wao
4. Ni Vipi Lowasa, Rostam na Chenge waliingia BOT na kukwapua Mabilioni ya Shilingi.
5. Ni kwa vipi Kujiuzulu kwa Hao watatu kutaleta Nafuu kwa maisha ya Watanzania
Mpaka hapo CCM itakapotoa majibu kwa Maswali hayo Mepesi Nitaendelea kuwatetea Lowasa, Rostam na Chenge
Asanteni
Namna uliyotumia kujieleza kwamba UNAWATETEA ndio inayokufanya na itakayokufanya usieleweke kwa wengi. Umeuliza maswali mepesi, basi ulipaswa utoe na utetezi mwepesi ulio sawa na maswali yako. Hujatoa utetezi wowote zaidi ya kuuliza tu maswali.
Isitoshe fahamu kwamba hao watu wanatuhumiwa na WANANCHI walio wengi, bila hivyo hata CCM wasinge vurugana kama sasa. Mi nakujibu
- Lowassa anatuhuma za kuingiza nchi hasara kubwa kwa kuruhusu kuingia mkataba na kampuni feki ya kufua umeme wakati akiwa Waziri Mkuu. Na ufisadi unaanzia hapo, mtu wa ngazi ya Waziri Mkuu wa nchi kukosa watu makini wa kuchunguza tu suala dogo la uwepo wa kampuni au la sio kitu kidogo. Na hapa ndio panaanza kuleta harufu ya ufisadi kwamba either yumo ktk mpango wa kupata fedha za hiyo kampuni feki, au yeye ni mmoja wa waanzilishi.
Utetezi wake ni kukataa tu kwamba hausiki. Mara ooh, tatizo ni uwaziri mkuu. Huu utetezi hauendani na tuhuma zenyewe. Ni utetezi mwepesi sana, kama vile kukana mahakamani kwamba hujahusika kuiba (kwa lengo la kupata dhamana) wakati ulionekana wazi wazi unaiba.
Na fahamu kwamba kuongoza umma ni dhamana kubwa sana, ukiboronga kwenye maeneo nyeti ambayo yanagharimu pesa nyingi za walipa kodi walalahoi, wananchi hawawezi kukuamini tena. Achia ngazi, usilazimishe uaminike hata kama unajua kuchapa kazi namna gani.
Lowassa huyu huyu anatuhuma kutoka hadi kwa Hayati Mwalimu Nyerere. Aliwahi kuulizwa "Kijana mdogo kama wewe umetoa wapi utajiri mkubwa huo ulionao, halafu unataka uongozi wa nchi?? Hufai kabisa"
Chenge anatuhuma za ufisadi kwenye rada, tuhuma ambazo zimeigharimu BAE kuilipa Tanzania mamilioni ya paundi. Na kama vile haitoshi, Uingereza wenyewe walishasema wazi Chenge bado hajasafishika. Vilevile huyu huyu Chenge hajasema zile pesa alizoweka benki kule karibu na visiwa vya Uingereza (zaidi ya Bilioni 1 za Tanzania) kazipataje, anaishia kusema tu "Ni vijisent)
Nakushangaa unaulizia mpaka Rostam Aziz. Hata mtoto wa darasa la tatu anaweza kukwambia sifa za Rostam. Yeye ndio anasemwa kama mfanikishaji namba 1 wa mkataba na kampuni feki niliyoeleza hapo juu kwa Lowassa. Anahusishwa hadi kwenye Kagoda.
Ngoja sasa nikueleze kujiuzuru kwao kunavyoweza kuleta unafuu wa maisha kwa mtanzania
- Kutatoa nafasi kwa uchunguzi wa kina kufanyika dhidi ya tuhuma zinazowakabili. Uchunguzi utakuwa huru, tofauti na wanapokuwa kwenye nyazifa zao. Hizi tuhuma zinaweza kuja kuzaa matunda ukipatikana ushahidi wa kutosha kuwaburuza mahakamani, na hatimaye Richmond wasilipwe na pengine wapigwe faini kubwa kama ilivyowatokea BAE. Hizo pesa haziwezi kuwaletea unafuu wa maisha wananchi???
- Kuondoka kwao kwenye nyadhifa zao (pengine wakiondolewa na walioshiriki nao kwenye ufisadi) kutatoa nafasi kwa watanzania wengine kushika hizo nafasi, ambao watatumia nasafi hizo kuwaletea wananchi wenzao unafuu wa maisha, sambamba na unafuu wa maisha yao binafsi
- Pia utakuwa mwanzo wa kuondolewa kwa mafisadi kwenye sehemu zingine, na hatimaye tukapata watu wazalendo wa kweli wa kutuletea maendeleo ya kweli