Nimeamua kuvunja ukimya

Nimeamua kuvunja ukimya

Tamalisa

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2015
Posts
2,542
Reaction score
907
Habari zenu wana jamvi,

Leo nimeamua kuvunja ukimya, nasema ukweli jamani ndugu zangu YESU ni mtamu, acheni nilewe huyu YESU mie. Yeye ni jana leo na hata mileleeee mwanzo na mwisho.

Hakuna kama yeye chini ya jua na kwingine kokote. Ni huyu Yesu aliyenipa elimu baada ya kufeli kwa mara ya kwanza form 4 na kukata tamaa kabisa, ni huyu Yesu, alinionesha njia hadi leo nina CV ya ukweli.

Ni yeye huyu aliyenipa kazi kwa muda mfupi tu baada ya kuhitimu masomo bila ujanja wowote ila kwa MAOMBI tu, ni yeye huyu aliyesimama na mimi pale kazini kupingana nao wale wote walionionyesha chuki na kunitengenezea mazingira ya mimi kufukuzwa kutokana na wivu wa elimu,.

Ni huyu YESU aliyempigania baba yangu kwa miaka 17 sasa akipita katik ajaribu lile.Ni huyu aliyenipa uzima hadi sasa naishi. Any way natamani na wewe umjue huyu MWANAUME ambaye;-

1. Sio msaliti
2. Mwaminifu 100%
3. Rafiki wa kweli nyakati zote
4. Mtimiza ahadi
5. Aliyeyashika maisha yako mkononi mwake
6. nk;

Jamani ndugu zangu tumwamini Yesu, dunia imeshatuchoka na hivyo inataka kututema tu, sasa sijui itakutema wapi, ni wakati wetu vijana tuamke na KUMPOKEA YESU AWE BWANA NA MWOKOZI WETU. AMEEN.

GOD BE WITH YOU
 
Uwongo dhambi kuna umri ambao kama miundombinu yako kimaisha na commitment bado iko complicated ukimpokea huyu mkuu utakuwa unadanganya...wako wapendwa kibao tunabanana nao kwenye vibanda umiza ila wakienda 'baibo' wanatubu!
 
Yesu ni mweza yoooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooote........amini ufanikiwe.....nisiapo jina la YESU.....natoka na machozi ya furaha.....nakumbuka mambo mengi magumu ambayo nimepitia mpaka leo nikawa mimi ambaye nipo nimepata kila kitu ambacho nimemuomba... nakupenda YESU.....
 
Amen, Mungu akutie nguvu katika safari hii ngumu ya wokovu ambayo si lelema bali kujikana nafsi. Ulitangaza vita na ibilisi tangu ulipokiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na mokozi wa maisha yako. Mungu awasaidie woote hapa JF siku moja wampokee Yesu.
 
Huwa nawaza sana hivi nikija kuokoka yaani zile totoz niwe nazicheki kwamacho tu!Daamh kumbe na kutamani nako hairuhusiwi???Sasa Yale mabindo mbinuko ndio basi???
 
Uwongo dhambi kuna umri ambao kama miundombinu yako kimaisha na commitment bado iko complicated ukimpokea huyu mkuu utakuwa unadanganya...wako wapendwa kibao tunabanana nao kwenye vibanda umiza ila wakienda 'baibo' wanatubu!

Mkaribishe kwanza maishani mwako, hafu ndo ulete hoja hapa
 
Amen,umefanya uamuzi wa busara,songa mbele mpendwa. Hakuna kama Yesu,yeye ndie jana, leo na hata milele.

Alikufa msalabani juu ya dhambi zetu,na kila ajae kwake hatamtupa kamwe!
 
Huwa nawaza sana hivi nikija kuokoka yaani zile totoz niwe nazicheki kwamacho tu!Daamh kumbe na kutamani nako hairuhusiwi???Sasa Yale mabindo mbinuko ndio basi???

Wala usiwaze mkuu utakachokipata kwa huyu Mwanaume sijui hata utaelezea vipi
 
Amen, Mungu akutie nguvu katika safari hii ngumu ya wokovu ambayo si lelema bali kujikana nafsi. Ulitangaza vita na ibilisi tangu ulipokiri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na mokozi wa maisha yako. Mungu awasaidie woote hapa JF siku moja wampokee Yesu.

Vita ni kali lakini kwa kujitoa na maombi vita hii naishinda karibu tuungane na kumuaibisha Shetani
 
Mimi ni mkristo pia sikuulizi kwa nia mbaya.
Wewe unasema Yesu amefanya baada ya kuhitimu umepata kazi, Sasa kwahiyo watu ambao wanamwamini kama wewe(wengi ninaowafaham) wamehitimu na hametafuta kazi kama wewe hawajapata, kwahiyo je, wao ndo vipi? au huyo Yesu mbaguzi kakusaidia wewe upate kazi halafu wao hawana kazi kawaacha?

Na kingine umepata kazi kama unavyosema ikitokea umefutwa kazi utasema Yesu amekusababisha ufutwe au kitu gani(kwasabu si unasema yesu ndo kakufanya upate kazi?)??

Naomba unifafanulie hapo nikuelewe vizuri kabisa.!
 
Back
Top Bottom